Siku ya watoto wa kurandaranda yaadhimishwa

watoto wa kurandaranda mitaani
Maelezo ya picha, watoto wa kurandaranda mitaani

Watoto wa kuranda randa hawatoki barabarani, bali katika jamii

Muswada wa Sheria ya haki za kibinadamu unasema: kila mtu ana haki ya uhai, makazi, elimu na afya bora. Shirika la Street Children and Youth ni mradi uliobuniwa miaka mitano iliyopita kutokana na ongezeko la familia za kurandaranda.

Zaidi ya mataifa hamsini duniani yakiongozwa na Uingereza, siku ya jumamosi wameadhimisha siku ya kimataifa ya watoto wa kurandaranda. Sherehe nchini Kenya ilifanyika katika kitongoji duni cha Mathare jijini Nairobi.

Lengo kuu ya siku hii ni kwa pamoja tusimame na familia za kurandranda, tuwape matumaini, tuwaonyeshe ya kwamba sisi tunawajali kama wanainchi wenzao na pia kuhakikisha wanahisi kama wao wamo katika jamii yetu.

Siku hii inaadhimishwa tarehe kumi 12 Aprili kila mwaka lakini nchini Kenya imeadhimishwa jumamosi tarehe 11 aprili kwa sababu sera za nchi haziruhusu uadhimishaji wa siku za kimataifa jumapili.