Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Lizzy Masinga

time_stated_uk

  1. Na hapa tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, tukutane tena kesho. Asante!

  2. Rais wa zamani wa Ghana, Jerry Rawlings aaga dunia

    Rais wa zamani wa Ghana, Jerry Rawlings

    Afisa wa juu wa kikosi cha anga cha Ghana, aliongoza mapinduzi mara mbili, kwanza mwaka 1979, akikabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia,na kisha miaka miwili baadae.

    Alikuwa kiongozi wa jeshi la Junta mpaka wakati wa uchaguzi uliohusisha vyama vingi mwaka 1992, alipokuwa rais wa kwanza mteule. Aliondoka madarakani mwaka 2001 baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.

    Mtu mwenye haiba, aliingia madarakani mnamo 1979 akipambana na ufisadi

    Ripoti kutoka Ghana zinasema kuwa rais huyo wa zamani alifariki hospitalini katika mji mkuu, Accra, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

    Katika miezi michache ambayo aliongoza nchi mnamo 1979, alikuwa na jukumu la kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya wakuu kadhaa wa zamani wa serikali na majenerali wa jeshi kwa madai ya ufisadi na usimamizi mbaya.

    Alionekana pia kama mwokozi wa maskini na alitumia muda wake madarakani kama mjamaa aliyejitolea.

    Baadaye alianzisha mageuzi ya soko huria na akaanzisha kipindi kirefu cha utulivu wa kisiasa, ambao unaendelea leo, baada ya msururu wa mapinduzi katika miaka ya 1960 na 1970.

  3. Felicien Kabuga: Afikishwa mahakama ya kimataifa kwa mara ya kwanza

    Yves Bucyana

    BBC Swahili

    Kabuga mwenye umri wa miaka 85, kulingana na mahakama,alikamatwa Ufaransa mnamo Mei baada ya zaidi ya miaka 20 akiwa mafichoni.

    Muda mwingi uliochukuliwa na Msajili wa Mahakamaaliyesomamadai dhidi ya Felicien Kabuga, ambaye alichagua kukaa kimya lakini hiyo ilimaanisha hakukubalimashtaka dhidi yake.

    Kesi hiyo ilipoanza janaJumatano, Jaji Mkuu Iain Bonomy alimwambia Kabuga kwambaana hakiya kutoa maoni yake mahakamani, kukaa kimya, au kutetewa.

    Kabuga mwenye umri wa miaka 85, kulingana na mahakama,alikamatwa Ufaransa mnamo Mei baada ya zaidi ya miaka 20 akiwa mafichoni.

    Alikuwa akitafutwa na mahakama ya kimataifa kwa shutuma ya kuhusika katika mauaji ya kimbari.

    Akisoma madai ya upande wa mashtaka, msajili wa mahakamaalisema Kabuga, akitumiauwezo na nguvu aliyokuwa nayo kwenye redio ya RTLM, "alihimiza njama ya kuwaangamizaWatutsi”

    Kwamba Kabuga ndiye alikuwa mdhamini mkuu wa redio hiyo na kwamba alikuwa anajua vizuri kila kitu alichokuwa akifanya, na pia kila kitu kilichokuwa kinazungumzwa na Redio hiyo.

    Alisema kwamba ‘’kwa namna ya pekee kwanzia tarehe 6 mwezi wa April,RTLM ilitamka wazi kuangamizwa kwa Watutsi na kwa kutaja baadhi yao wakiwa mafichoni, iliwauawe.

    Aliongeza: "Felicien Kabuga alikuwa akijihusishanashughuli zote za RTLM, kuajiri na kufukuza waandishi wa habarina kufuatilia utendaji kazi wa Radio hiyo.

    Kabuga alikuwa 'amechoka sana'

    Wakati walikuwa bado wanasoma mashtaka dhidi ya Kabuga, wakili wa mshtakiwa alisema mteja wake "amechoka sana" na kuomba mapumziko mafupi, ambayo hakimu aliruhusu.

    Kabuga, wakati huo huo, alikuwa akisikiliza madai hayo, yakitafsiriwakwa kinyarwanda huku akionekana bila wasiwasi wowote au hofu juu ya mashtaka hayo makubwa dhidi yake.

    Ameshtakiwa kwa kuongoza mikutano iliyopangamauaji , kutoa msaadawavifaa vya kuua, kusambaza magari na kusambaza pombe kwa wanamgambo ‘ Interahamwe’ ambao walifanya mauajikatika mtaa waKimironkomjiniKigali na Gisenyi.

    Kabuga alikuwa akitafutwa na mahakama ya kimataifa kwa shutuma ya kuhusika katika mauaji ya kimbari

    Msajili wa mahakama amesema Kabuga hakuwahi kukataza watu kufanya mauaji,kupeleka mbele ya vyombo vyasheria wala kusimamisha msaada wa hali na mali kwa wauaji. Pia alisema kwamba kuna matamshi ya Kabuga mwenyewe akihamasisha mauaji.

    MsajiliamesemaKabugamwenyewealiomba ‘’ "adui auawe mahali popote alipo" na kwamba aliposema neno"adui ‘’alikuwa anajua vizuri kwamba hata wanamgambo Interahamwe walikuwa wanafahamu vizuri kwamba anazungumzia watu wa kabila la’’ Watutsi’’ .

    Kabuga aamua kukaa kimya

    Kwa upande wa mshtakiwa, wakili wa Kabuga, Me Altit Emmanuel, alisema walizungumza kwanza na mteja wake juu ya uamuzi wake wa kutosema lolote mahakamani.

    Alisema:’’ tulikuwa tumeshauriana ,hatazungumza lolote kutokana afya yake,naomba mkubali kwamba hatasema lolote , hii pia ina maana kwamba anakana mashtaka dhidi yake.’’

    KadhalikaBwana Altit amesisitizaafya ya mwili na akili ya Kabuga na hali yake kwa ujumla ichunguzwe kabla ya kesi kuanza.

    Mwendesha mashtaka Sege Brammertz amemuombajaji muda wa kujiandaa kwa kesi hiyo.

    Amesema wanataka kujiandaa vyema kwa kuzungumza tena na mashahidi na jinsi watakavyotoa ushahidi wao wakiwa nchini Rwanda , kutafsiri jalada la mashtaka na kuliweka katika lugha ya kinyarwanda kama ilivyopendekezwa na mtuhumiwa na kadhalika.

    Jaji Iain Bonomy alisema anakwendakusoma hoja za pande zote mbili na korti itatangaza uamuzi kuhusu lini kesi hiyo itaendelea.

  4. Mashirika yashindwa kupeleka misaada Tigray

    Rasilimali zimekuwa zikiongezwa kwa pande zote mbili hali inayoashiria kuwa mapigano yataendelea kwa muda

    Umoja wa Mataifa umesema mashirika ya misaada yanapata taabu kufikisha misaada katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia, ambapo serikali ya nchi hiyo inafanya operesheni zake dhidi ya vikosi vilivyo vitiifu kwa mamlaka za jimbo hilo.

    Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia, Catherine Sozi, ameiambia BBC kuwa kutoa misaada ya binadamu imekuwa vigumu tangu mzozo ulipoanza.

    Mashirika ya misaada imetahadharisha kuwa huduma za chakula na za kiafya zimezuiwa kuingia Tigray.

    Lakini, katika mtandao wa Twitter siku ya Alhamisi, Waziri Mkuu Abiy Ahmed alisema serikali ilikuwa ikitoa msaada katika maeneo ya Tigray yanayodhibitiwa na jeshi la nchi.

    Pande zote za mamlaka ya Tigray na serikali ya Ethiopia zimekuwa zikiongeza rasilimali zake –hatua inayoashiria kuwa mzozo huo utaendelea kwa muda.

    Kampeni za kuchangia damu- zilizoratibiwa na mamlaka zimekuwa zikifanyika katika baadhi ya maeneo Kusini mwa Ethiopia na makundi yanayounga mkono jeshi la taifa.

    Ni zaidi ya wiki moja sasa tangu mapambano yalipoibuka katika jimbo hilo la Kaskazini na athari zake zimeonekana mpaka nchi jirani ya Sudan- wakati maelfu ya watu wakivuka mpaka wakikimbia mapigano.

  5. Baba akamatwa baada ya mtoto wake kufa na kutupwa baharini

    Senegal imeshuhudia ongezeko la wahamiaji wakijaribu kwenda Ulaya

    Polisi nchini Senegal wamemkamata baba wa mtoto wa kiume wa miaka 15 aliyekufa maji baharini mwezi Oktoba wakati akijaribu kwenda Ulaya.

    Inadhaniwa kuwa baba alimlipa fedha msafirishaji kiasi cha pauni 340 kumpeleka mtoto wake Uhispania.

    Mtoto huyo kwa jina jingine Doudou,kisha angechukuliwa kwenda Italia katika kituo cha mafunzo ya mpira wa miguu.

    Aliugua, na kupoteza maisha akiwa njiano na mwili wake ulitupwa baharni.

    Kifo chake kilisababisha mshtuko nchini Senegal, ambayo hivi karibuni imeshuhudia ongezeko la wahamiaji wakijaribu kuvuka bahari kufikia Ulaya.

    Polisi wa Senegal walisema wamewakamata wahamiaji zaidi 1,500 katika siku za hivi karibuni.

  6. Msumbiji yakana taarifa kwamba raia walikatwa vichwa na wanamgambo wa Kiislamu

    Maelfu ya watu wamekimbia mashambulizi Cabo Delgado.

    Msumbiji imekana taarifa za raia kukatwa vichwa na wanamgambo wa Kiislamu

    Serikali ya Msumbiji imekana ripoti kuwa kumekuwa watu wamekuwa wakikatwa vichwa na wanamgambo wa kiislamu katika mji wa Cabo Delgado.

    Gavana wa eneo hilo lenye utajiri wa mafuta, Valige Tauabo, amesema kuwa hakuna matukio ya mauaji ya hivi karibuni katika wilaya yoyote ya mji huo, tofauti na ripoti zinavyoeleza.

    Aliongeza kuwa ripoti ya mwisho ya mauaji yaliyotekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu yalikuwa tarehe 6 mwezi Aprili.

    Vyombo vya habari viliripoti kuwa zaidi ya watu 50 walikatwa vichwa na wanamgambokatika uwanja wa mpira wa miguu katika kijiji, wilaya ya Miudumbe.

    Watu wenye silaha waliimba "Allahu Akbar" (Mungu ni Mkubwa), walifyatua risasi, na kuchoma moto makazi ya watu walipovamia kijiji cha Nanjaba, usiku wa Ijumaa, Shirika la habari la Msumbijililiwanukuu manusura wa tukio hilo.

    Gavana Tauabo alisema kumekuwa na tu "uvamizi wa waovu" ambao walikuwa wakifuatiliwa na jeshi.

    Aliongeza kuwa serikali inasikitishwa kuhusu kuenea kwa ghasia za silaha huko Cabo Delgado.

  7. Kassim Majaliwa athibitishwa kuwa Waziri MKuu

    Bunge la Tanzania limemuidhinisha, Mbunge wa Ruagwa Kassim Majaliwa kwa wadhifa wa Uwaziri Mkuu.

    Majaliwa amepata kura za wabunge wote 350 waliopiga kura , sawa na 100%.

    Amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini kwa miaka mitano iliyopita na kumpa tena nafasi nyingine.

  8. Rais Ouattara na upinzani ‘kupatana’ wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi

    Ouattara na mpinzani wake kuirudisha amani

    Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, na mpinzani wake mkuu, Henri Konan Bédié, wamesema wameamua kupatana baada ya wiki kadhaa za vurugu baada ya uchaguzi uliokumbwa na mzozo.

    Wawili hao wamesema wataendelea kuzungumza baada ya kukutana katika mji wa kibiashara, Abidjan, siku ya Jumatano.

    Serikali imesema kuwa watu 85 wameuawa katika vurugu za baada ya uchaguzi ambao Bw.Ouattara alishinda ili kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu.

    Viongozi kadhaa wa upinzani wamekamatwa baada ya kupinga uchaguzi na kuanzisha utawala wa upinzani.

    Maneno ya kwanza ya Rais Ouattara kwa Waandishi wa habari baada ya mkutano yalikuwa “uaminifu umejengwa upya”

    Lakini hawakupeana mikono mbele ya wapiga picha.

    Chama cha Bw. Bedie, PDCI, awali kilisisitiza masharti kadhaa kabla ya mkutano –ikiwemo kuondolewa kwa vizuizi vya kiusalama kwenye makazi ya viongozi wa upinzani na kusitisha kesi dhidi yao.

    Upinzani hauyatambui matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 31 mwezi Oktoba.

  9. Jiwe kubwa la almasi lagunduliwa Botswana

    Almasi

    Moja kati ya mawe makubwa ya almasilimechimbwa nchini Botswana na mchimbaji mdogowa Canada, ambaye ameendelea kugundua mawe makubwa.

    Kampuni ya Lucara Diamond Corp. imesema imebaini almasi nyeupe ya karati 998, na kufanya kuwa miongoni mwa mawe makubwa matano kuwahi kugunduliwa. Lucara amesema almasi hiyo itahitajika kuigawa vipande kabla ya kuisafisha.

    Mgodi wa Karowe umekuwa maarufu kwa kugundua mawe makubwa. Mwaka 2015, kampuni iligundua jiwe la karati 1,109 Lesedi La Rona , lililouzwa kwa dola milioni 53, na pia jiwe la karati 813 lililoweka rekodi ya kuuzwa kwa dola za Marekani milioni 63.

    Kwa mujibu wa gazeti la Bloomberg , Jiwe kubwa kabisa la almasi kuwahi kugunduliwa ni la karati 3,106 Cullinan, lililogunduliwa Nchini Afrika Kusini mwaka 1905.

    Kwa mujibu wa Forbes Lucara, ambayo iliuza mawe yake mawili mwakubwa kwaLouis Vuitton , imesema inafanya tathimini hatua zinazofuata na mshirika wake wa shughuli za kukata na kusafisha HB Antwerp.

  10. Habari za hivi pundeKassim Majaliwa ateuliwa kuendelea na uwaziri mkuu

    Rais John Magufuli amemteua tena mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuendelea na wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania.

    Asubuhi ya leo mpambe wa rais Magufuli amewasilisha bahasha ambayo ilikuwa na jina la Majaliwa ili kusomwa bungeni.

    Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Magufuli uliokamilika mwezi uliopita.

    Waziri Mkuu huyo mteule sasa anasubiri kuidhinishwa na bunge kwa kupigiwa kura na jina lake likipita bungeni ataapishwa rasmi kushika wadhifa huo.

  11. Habari! karibu katika matangazo ya moja kwa moja