Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli ameaga dunia

Rais John Pombe Magufuli

Chanzo cha picha, AFP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameaga dunia.

Kifo cha Magufuli kimetangazwa rasmi Jumatano usiku na makamu wake Samia Hassan Suluhu.

Amesema kwamba rais Magufuli aliaga dunia katika hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es Salam mwendo wa saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki kutokana na matatizo ya moyo.

Akithibitisha kifo hicho makamu wa rais Samia Suluhu amesema kwamba rais Magufuli alianza kuugua mnamo tarehe 14 mwezi Machi na kulazwa katika hospitali hiyo ambapo alifariki.

Magufuli ambaye ni rais wa tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania amefariki akiwa na umri wa miaka 61.

Kwa mujibu wa makamu huyo wa rais Magufuli alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wa moyo kutoka hospitali ya Jakaya Kikwete.

Ruka Twitter ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Makamu huyo wa rais ametangaza siku 14 za kuomboleza . Amesema kwamba katika kipindi hicho chote bendera zote nchini humo zitapepea nusu mlingoti.

Amesema kwamba Magufuli amekuwa akiugua tatizo la moyo kwa zaidi ya miaka 10.

Tangazo la kifo chake linajiri zaidi ya wiki mbili tangu alipoonekana hadharani na kuzua uvumi kwamba alikuwa akiugua virusi vya corona.

Rais John Pombe Magufuli

Hatahivyo makamu wake aliwataka raia wa Tanzania kupuuzilia mbali uvumi huo.

Kulingana na katiba ya Tanzania, makamu wake atachukua uongozi na kuendeleza kipindi cha muda uliosalia.

Tayari baadhi ya viongozi kutoka mataifa mbali mbali wameanza kutuma risala za rambirambi kwa raia wa jamhuri ya Tanzania na familia ya Magufuli.

Ruka Twitter ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Uchunguzi wa BBC