Maalim Seif Sharif Hamad azikwa kijijini kwake Pemba
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mtambwe Nyali mkoa wa Kaskazini Pemba.
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Maalim Seif Sharif Hamad azikwa kijijini kwake Mtambwe
Chanzo cha picha, ACT-Wazalendo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amezikwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mtambwe Nyali mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mwili wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, uliagwa mapema leo asubuhi katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.
Viongozi mbalimbali wa kitaifa walishiriki ibada hiyo akiwemo Rais mstaafu Jakaya Mrisho kikwete na Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe.
Chanzo cha picha, ACT-Wazalendo
Baadhi ya waliohudhuria ibada hii wamesema kuwa wamesikitishwa sana na msiba huu, baadhi yao wamewahi kusaidiwa kwa namna moja ama nyingine na Maalim Seif.
Mamia ya wazanzibari walimiminika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo mjini Ujunga ambapo ndipo mwili ulipokelewa kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya dua kabla ya kusafirishwa kijijini kwake Mtambwe.
Kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad kinaonekana kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa visiwani humo na watanzania kwa ujumla.
Hospitali ya Aga Khan kuchunguzwa kwa madai ya kutoza gharama za juu
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limefungua jalada la uchunguzi dhidi ya hospitali ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam kwatuhuma kuwa imekuwa ikitoza gharama kubwa za matibabu kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma hospitalini hapo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi, kanda maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi la Polisi limepokea malalamiko kutoka kwa wananchi dhidi ya Hospitali ya Aga Khan ya Jijini Dar es Salaam kutoza gharama kubwa za matibabu kwa wagonjwa wa matatizo kifua (Pneumonia) ambayo husababisha matatizo ya upumuaji.
Aidha wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika Hospitali hiyo, pindi wanapofariki dunia kumekuwa na tabia ya kuzuia miili ya marehemu na kudai kiasi kikubwa cha fedha kinyume na maelekezo ya Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto.
‘’Management ya hospitali hiyo imekuwa na tabia mbaya ya kuzuia miili ya marehemu wanaokuwa wamefariki pale na baada ya kuzuia wanalazimisha kutoa bili kubwa ambayo haiendani na tiba ambayo kimsingi mgonjwa alikuwa anapata’’.
‘’Wamekuwa wakifanya hivi kwa muda mrefu na wakati Fulani kupelekea wahusika kuuza vitu vyao ili kukomboa miili.’’ Alisema kamanda Mambosasa.
Hata hivyo Mambosasa amesema kuwa uchunguzi utakapokamilika na kubaini tuhuma hizi hatua kali za kisheria zitachukuliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto dhidi ya Hospitali hiyo.
Wanajeshi saba waadhibiwa kwa kosa la kuwapiga waandishi wa habari Uganda
Wanajeshi waliokamatwa kwa kosa la kuwapiga waandishi wa habari wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi.
Wanajeshi saba walikamatwa nchini Uganda kwa kuwapiga waandishi wa habari hapo jana.
Waandishi hao walikuwa wakimsubiri kiongozi wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi, aliyepeleka malalamiko yake kwenye Kemisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Kololo.
KapteniJessy Odwenyi, Koplo Nimusiima Justine, Pte Wasswa Peter, Pte Tsame Imran, Pte Kisakye Victoria, Pte Opiyo Isaac, cpl Zirimenya Kassim.
Kapteni Odwenyi amepewa hukumu ya kubakikizuizini kwa siku 90 katika kambi ya jeshi ya Makindye,L/CPLZimerenyaKassim amehukumiwa kuwa kizuizini kwa siku 60 huku Kapteni Nimusiima Justine akipatiwa karipio kali na onyo huku Kisyake Victoria na Opiyo Isaac wakihukumiwa kifungo cha siku 62 kwenye gereza la kijeshi.
Televisheni yafungiwa Zanzibar kwa kukiuka muongozo
Tume ya Utangazaji Zanzibar imekifungia kituo cha televisheni cha Tifu kwa muda wa siku saba baada ya kudaiwa kukiuka utaratibu wa urushaji vipindi wakati wa kuomboleza msiba wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Katibu mtendaji wa Tume hiyo, Omar Said akitoa taarifa hiyo alisema kwamba tume hiyo imelezimika kuchukua uamuzi huo baada ya kubaini kwamba kituo hicho kinakwenda kinyume na miongozo iliyotolewa, Mwananchi limeripoti.
Alisema kufuatia taarifa iliyotolewa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi hapo jana kuhusu msiba wa Makamu wa kwanza wa Rais, tume ilitoa muongozo wa urushaji matangazo na vipindi kwa kipindi hiki cha muda wa siku saba za maombolezo kwa vituo vya televisheni, redio na mitandao ya kijamii.
Kituo cha Tifu kilionekana kwenda kinyume na muongozo huo, hivyo Tume imelezimika kuchukua hatua ili kutoa fundisho.
Mkuu wa jeshi la UPDF awaomba radhi waandishi Uganda,
Mkuu wa jeshi la UPDF Jenerali David Muhoozi ameomba msamaha kwa wandishi wa habari kufatia tukio la jana wakati poilisi wa jeshi la UPDF waliwatandika wandishi habari waliokuwa wakimsubiri kiongozi wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi, aliyepeleka malalamiko yake kwenye Kemisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa Kololo.
Jenerali David Muhoozi amesema uchunguzi umeanza kwa waliofanya kitendo hicho na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Chanzo cha picha, Getty Images
Jeshi litalipa gharama za matibabu ya wandishi habari hao.Wandishi waliojeruhiwa ni Cliff Wamala wa NTV, Josephy Dhabiti NBC,Rashid Nakayi GalaxyFm, Timoth Murungi New Vision, Irene Abaro Monitor, Josephine Namakumbi NBS na Jeff Twesigye NTV.
Jenerali Muhoozi amesema jeshi la UPDF halikuwatuma wanajeshi hao kuwapiga waandishi wa habari.
Ametoa wito kwa waandishi habari kuwa na vitambulisho vinavyoonesha wakiwa kazini kusaidia kuwatambua na mwisho amesema watafanya mpango kuzungumuza na waandishi wa habari ili kuboresha mahusiano kati ya pande hizo mbili.
'Hatutishwi na uamuzi wa Facebook'
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison amesema kuwa serikali yake haitishwi na kitendo cha Facebook kuzuia kupatikana kwa habari nchini humo.
Kampuni ya Facebook imezuia watumiaji wake nchini Australia kuchapisha au kutazama habari katika jukwaaa hilo jambo lililozua wasiwasi mkubwa miongoni mwa watumiaji wa mtandao huo wa kijamii kuhusu namna watakavyopata habari muhimu na kuchangamana pia.
Wale walio nje ya Australia pia hawawezi kusoma au kupata machapisho yoyote ya habari ya Australia kwenye jukwaa hilo la facebook.
Aidha kampuni ya facebook imechukua hatua hiyo baada ya kuwepo sheria ambayo nchi hiyo inapanga kuwatoza pesa wafanyabiashara wanaochapisha habari kwenye jukwaa hilo.
Aidha kampuni kama Google na Facebook wamesema sheria hiyo haielezi wazi jinsi mtandao huo utakavyofanya kazi na hivyo umelenga kuwaadhibu tu.
Lakini serikali ya Australia imesema kuwa inaendelea na sheria hiyo, ambayo ilipitishwa na baraza la bunge siku ya Jumatano.
Waziri wa habari nchini humo Paul Fletcher ameiambia BBC kuwa kampuni hiyo inahitaji kufikiria kwa uangalifu kuhusu hatua walioichukua.
Mwili wa hayati Seif Sharif Hamad ukielekea Pemba
Mwili wa marehemu Maalim Seif umewasili Zanzibar,
Mwili wa aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais Zanzibar umewasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja huku maelfu wakijitokeza kuomboleza msiba huo uliotokea jana.
Maalim Seif alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa anapata matibabu.
Awali Chama chake cha ACT Wazalendo kilitangaza kwamba Kiongozi huyo amepata covid-19.
Baada ya swala, mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kisiwani Pemba katika kijiji cha Mtambwe alipozaliwa Maalim.
Viongozi mbalimbali ikiwemo marais wastaafu wa Zanzibar akiwemo Dr Ali Mohammed Shein, Abeid Amani Karume na wengine wamehudhuria swala hiyo.
Simanzi wakati wakiaga mwili wa Maalim Seif, jijini Dar es Salaam
Maelezo ya video, Simanzi wakati wakiaga mwili wa Maalim, jijini Dar es Salaam Tahadhari zikichukuliwa wakati watu wakijiandaa kupokea mwili wa Maalim Seif
Maelezo ya video, Tahadhari zikichukuliwa wakati watu wakijiandaa kupokea mwili wa Maalim Seif Maalim Seif Sharif Hamad:Mamia wajitokeza kuupokea mwili wa Maalim, Unguja,
Mamia ya wazanzibari wanaendelea kumiminika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja vilivyopo mjini Ujunga ambapo ndipo mwili wa aliyekuwa makamo wa kwanza wa Urais Zanzibar utakapoletwa kwa ajili ya dua kabla ya kusafirishwa kijijini kwake Mtambwe, kisiwani Pemba.
Kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad kinaonekana kuleta simanzi kubwa kwa wakazi wa visiwani humo na watanzania kwa ujumla.
Kisiwani Pemba ambapo ndio alikuwa ngome yake Kuu wakati wa uhai wake, punde tu baada ya taarifa za kifo chake kuenea, baadhi ya maduka yamefungwa na shughuli nyingi za mji kusimama, hivyo kufanya mji huo kuzizima kwa saa kadhaa.
Ratiba ya mazishi inaonyesha kuwa, baada ya mwili wa marehemu utaswaliwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja na hatimae kwenda kupumzishwa huko kijijini kwao Mtambwe.
Mwishoni mwa mwezi January, chama cha ACT Wazalendo kilitangaza hadharani kuwa Maalim alipata maambukizi ya Corona. Hivyo, kumfanya kuwa kiongozi wa kwanza nchini Tanzania kuweka wazi hali yake ya maambukizi, ingawa Tanzania imekuwa ikisisitiza aidha kuwepokuwepo kwa Covid19 au kuidhibiti.
Hata hivyo, wakati maombelezi yakiendelea, wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wameonekana wakiwanyunyizia watu sanitaiza huku wachache Wakionekana kuchukua tahadhari ya kuvaa barakoa.
Mpaka kifo chake, Maalim alikuwa makamo wa kwanza wa urais Zanzibar chini ya serikali ya umoja wa kitaifa.
Maalim anazikwa wakati watanzania wapo katika kuomboleza msiba mwengine wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya rais John Magufuli.
Maalim Seif Sharif Hamad: Mamia wajitokeza kumswalia,
Wakazi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza kwa wingi kumswalia Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Seif Sharif Hamad .
Swala imefanyika katika msikiti wa masjid Maamur Upanga.
Viongozi mbalimbali pia wameshiriki ibada hiyo akiwemo Rais mstaafu Jakaya Mrisho kikwete na Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe.
Baadhi ya waliohudhuria ibada hii wamesema kuwa wamesikitishwa sana na msiba huu, baadhi yao wamewahi kusaidiwa kwa namna moja ama nyingine na Maalim Seif.
Maelezo ya picha, Mamia wamejitokeza kumswalia Maalim Seif Maelezo ya picha, Mwili wa Maalim Seif ukiwa umebebwa Maelezo ya picha, Wakazi wa Dar es salaam wakijiandaa kuupokea mwili Maelezo ya picha, Swala imefanyika katika msikiti wa masjid Maamur Upanga Chuma cha ajabu chapatikana DRC
Eneo la makutano ya barabara jijini Kinshasa limekuwa eneo lililovuta macho ya wengi baada ya kupatikana chuma cha ajabu, shirika la habari la Reuters limeripoti.
Watu wamekuwa wakichapisha picha ya chuma kinachong’aa ambapo vyuma kadhaa kama hivyo vimekuwa vikionekana duniani kote miezi ya hivi karibuni, cha kwanza huko Utah nchini Marekani mwezi Novemba mwaka jana.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
‘’Tuliamka tukaona chuma hiki cha pembe nne,’’ Serge Ifulu, mkazi wa eneo hilo, aliliambia shirika la Reuters.
‘’Tulishangazwa kwasababu ni chuma ambacho huwa tunakiona kwenye Makala kuhusu freemasons au illuminati.’’
Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Tanzania afariki dunia
Chanzo cha picha, Ikulu-Tanzania
Katibu mkuu kiongozi wa serikali ya Tanzania Balozi John Kijazi amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu, Balozi Kijazi alifariki majira ya saa tatu na dakika kumi usiku katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
Katika taarifa hiyo, Rais wa Tanzania John Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na kifo hicho na kumtaja Kijazi kama mtu aliyeyafanya majukumu yake kwa ukamilifu.
Taratibu za mazishi za kiongozi huyo mkubwa wa taifa zinatarajiwa kutangazwa baadaye.
Lakini Balozi John Wiliam Kijazi ni nani hasa?
Balozi Mhandisi John William Herbert Kijazi amekuwa mwakilishi wa Tanzania nchini India, Singapore, Sri Lanka, Bangladesh na Nepal mwenye makazi yake jijini New Delhi, India kuanzia mwaka 2007 - 2016 na hivyo kumfanya kuwa Mkuu wa Mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania nje ya nchi.
Kabla ya kuwa balozi, Mhandisi Kijazi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na baadaye Wizara ya Maendeleo ya Miundombinu kuanzia mwaka 2002 hadi 2006, baada ya kuteuliwa kuwa Balozi ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano waKimataifa na hatimaye kupangiwa kituo cha New Delhi, India.
Kati ya mwaka 1996 hadi 2002, Mhandisi Kijazi alikuwa Mhandisi Mwandamiziwa Ujenzi wa Barabara ndani ya Wizara ya Ujenzi kabla ya kupandishwa cheo na kuwaMkurugenzi wa Barabara za Mikoa ndani ya Wizara hiyo hiyo.
Balozi Mhandisi Kijazi alipata Shahada ya Sayansi ya Uhandisi wa Umma mwaka 1982 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na baadaye Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Barabara Kuu kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingerezamwaka 1992.
Balozi Mhandisi John Kijazi amemuoa Fransisca Kijazi na pamoja wamejali watoto watatu ambao ni David, Emmanuel na Richard Kijazi.
, Habari..karibu katika matangazo ya moja kwa moja katika kurasa wa BBC Swahili, leo ikiwa tarehe 18/02/2021