Newcastle 2-1 Arsenal: Mapungufu ya Arsenal yaigharimu timu hiyo

Matt Ritchie amefunga bao lake la tatu katika ligi ya England msimu huu dhidi ya Arsenal

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Matt Ritchie amefunga bao lake la tatu katika ligi ya England msimu huu dhidi ya Arsenal

Newcastle imeinyuka Arsenal 2-1 na kuufunga mustakabali wake katika ligi ya England huku jinamizi la rekodi mbaya kwa Arsenal 2018 likiendelea kuiandama timu hiyo ya Arsene Wenger.

Gloi la Matt Ritchie kunako dakika 68th kumeipa timu ya Newcastle ushindi wa nne mtawalia wa ligi na kwa sasa ina pointi 41 huku ikiwa imesalia na michezo 5.

Arsenal, iliyofuzu kuingia katika nusu fainali ya ligi Uropa kwa ushindi wa 6-3 dhidi ya CSKA Moscow nchini Urusi siku ya Alhamisi, inasubiriwa kujinyakulia pointi katika ligi mwaka huu.

Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette, wanaocheza kwa mara ya kwanza pamoja walishirikiana katika bao la ufunguzi la Arsenal kunako dakika ya 14.

Mshambuliaji huyo raia wa Gabon alipokea mchango wake Shkodran Mustafi na kuusukuma mkwaju ndani ya wavu.

bao la Newcastle dhidi ya Arsenal

Chanzo cha picha, Reuters

Ayoze Perez alilisawazisha muda mfupi kabla ya nusu saa ya mchezo na kukimbia na kumpita Shkodran Mustafi, na kuiogoza krosi ya DeAndre Yedlin karibu na lango kuu.

Calum Chambers alistahili kuisukuma Arsenal mbele kuongoza katika mechihiyo kuelekea mwisho wa nsu ya kwanza ya mechi lakini mpira ulikwenda kombo alipopokea hedi ya Mustafi.

Mambo yalikwenda sare hadi kunako dakika ya 68 wakati Ritchie aliposukuma tobwe la ushindi.

Ilikuwa hali ya roho mkononi kunako dakika zamwisho za mechi hiyo wakatiArsenal ilipokuwa inajizatiti kutoka angalau kwa sare, lakini Newcastle iliendelea kushikilia usukani na kumalizia kwa ushindi huo muhimu.