Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

time_stated_uk

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja katika ukurasa wa BBC Swahili, Shukrani

  2. Motsepe kuwa rais wa Caf baada rufaa ya Ahmad kufeli

    Motsepe

    Patrice Motsepe anatarajiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (Caf) wiki hii, baada ya baada mahakama ya kusuluhisha migogoro ya michezo (Cas) hii leo kupunguza adhabu ya marufuku ya kujihusisha na mpira kwa rais wa zamani wa Caf Ahmad Ahmad kutoka miaka mitano hadi miwili.

    Safari ya bilionea huyo raia wa Afrika Kusini kuchukua hatamu ya uongozi wa Caf ilinyooka mwishoni mwa juma baada ya washindani wake watatu - Jacques Anouma, Augustin Senghor na Ahmed Yahya - kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho.

    Kigingi cha mwisho kwa Motsepe, 59, kutawazwa siku ya Ijumaa ilikuwa uwezekano wa Ahmad kurejea ulingoni, endapo mahakama ingemuondolea kabisha marufuku inayomkabili.

  3. ACT Wazalendo yaomba Tanzania kutatua mzozo wa mahindi Kenya

    Zitto

    Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo , Zitto Kabwe ametoa wito kwa serikali ya Tanzania kujadiliana na serikali ya Kenya kuhusu mzozo wa soko la mahindi ya Tanzania nchini Kenya.

    Kauli ya Bw. Zitto inakuja siku chache baada ya Kenya kupiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka nchi jirani za Tanzania na Uganda.

    Katika taarifa Zitto alisema ’’Sisi kama viongozi wa Kisiasa wajibu wetu ni kwa Watanzania’’

    Aidha alisema kutokana na jukumu hilo wanalazimika kuisukuma serikali ya Tanzania imalize mzozo huo kupitia mazungumzo ya Kidiplomasiana serikali ya Kenya.

    View more on twitter

    Aidha msemaji wa serikali ya Tanzania, Dkt.Hassan Abbas amesema "hakuna taarifa rasmi ila ni kweli kuna magari yamezuiwa katika mpaka wa Namanga lakini katika mipaka mingine magari yanapita."

    Aliongeza kusema kuwa ameona maelezo tu katika mtandao wa kijamii ila hakuna taarifa rasmi.

  4. Tanzania 'kuchunguza wizi wa kikombe cha Ekaristi'

    Police are still investigating how the cup disappeared from the church
    Image caption: Polisi bado wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka kutoka kanisani

    Kikombe cha Ekaristi Takatifu kutoka kanisa moja la katoliki nchini Tanzania kimeibiwa, kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi.

    Wizi wa kikombe hicho cha Ekaristi kilicho na thamani ya dola 2,150 ulitokea Jumapili iliyopita katika Parokia ya Mkoka, iliyopo mji Mkuu wa Dodoma.

    Polisi wanachunguza jinsi kikombe hicho kilivyotoweka katika majengo ya kanisa.

    Aidha hakuna kitu kingine kilichoibiwa kutoka kanisani humo.

    Na mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kutokana na wizi huo, gazeti hilo limemnukuu mkuu wa usalama wa eneo hilo.

  5. Shujaa wa Kenya Westgate 'aungwa mkono kwa kiti cha seneti'

    Abdul Haji

    Mfanyabishara Abdul Haji, aliyepata umaarufu kwa kukabiliana na wanamgambo waliovamia duka la Westgate katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, mwezi Septemba 2013, ameidhinishwa kumrithi baba yake Yusuf Haji kuwa seneta wa Garissa, gazeti la Standard limenukuu taarifa ya familia yake.

    Wakati wa shambulio hilo, Bw Haji aliingia ndani ya duka hilo kumtafuta ndugu yake akiwa amejihami kwa bastola tu ambayo alifundishwa na baba yake kutumia kwa uwindaji alipokua mtoto.

    Akiwa pamoja na kundi dogo la maafisa wa polisi waliokuwa wameavalia nguo za nyumbani, alisaidia kuokoa makumi ya watu kutoka kwenye duka hilo.

    Abdul Hajj

    Familia yake sasa limemuidhinisha kukamilisha muhula wa pili wa baba yake katika bunge la seneti, gazeti hilo liliripoti.

    Seneta Haji alifariki mwezi uliopita mjini Nairobi na uchaguzi mdogo umepangiwa kufanyika mwezi Mei.

  6. Boti iliyo na tani kadhaa za mafuta yakwama Mauritius

    Wafanyakazi wa chombo hicho wameokolewa
    Image caption: Wafanyakazi wa chombo hicho wameokolewa

    Boti ya uvuvi iliyo na bendera ya China imekwama katika miamba ya matumbawe nchini Mauritius, karibu kilomita 10 kutoka mji mkuu wa, Port Louis.

    Chombo hicho, LURONGYUANYU 588, kilikwama Pointe aux Sables maili chache kutoka ufukweni.

    Ilikuwa imebeba tani 130 za mafuta ya dizeli na tani tano za mafuta mengine lakini haikuwa na samaki, kulingana na Waziri wa Uvuvi, Sudheer Maudhoo.

    Boti hiyo ilikuwa imepangiwa kuhamisha mafuta kutoka kwa meli na kuchukua vifungu katika Port Louis.

    “kwa sasa inaelea juu ya maji na hakuna mafuta yaliyomwagika kufikia sasa,” waziri alisema.

    “Mipango ya dharura imefanywa endapo mafuta yataanza kumwagika kutoka kwa chombo hicho katika bandari ya Port Louis."

    Wafanyakazi 16 wa boti hiyo waliokolewa Jumapili jioni. Walikuwa raia 14 wa China baharia mmoja raia wa Indonesia na mwingine wa Ufilipino.

    Walinzi wa kitaifa wa pwani ya Mauritius wamesema walipokea ombi la msaada kutoka kwa boti hiyo ya uvuvi.

    Bahari yenye dhoruba ilifanya operesheni ya uokoaji kuwa ngumu hadi helikopta ya polisi ikaitwa.

  7. Mwanamke mwenye ukimwi anayewasaidia wengine 'kufa kifo kizuri'

    Thembi Nkambule

    Thembi Nkambule amekuwa akiwahudumia mamia ya watu wanaofariki kutokana na Ukimwi Eswatini - nchi ambayo mtu mmoja kati ya wanne ana HIV. Haya ndio mambo aliyojifunza juu ya maana ya "kifo kizuri".

    Soma zaidi

  8. Burna Boy kutumbuiza katika tuzo ya Grammy 2021

    Burna Boy

    Msanii wa Nigeria Burna Boy, atatumbuiza katika Tuzo ya Grammy 2021 itakayoandaliwa Marchi 14.

    Hii ni mara ya pili msanii huyo wa kuteuliwa kuwania Tuzo ya Grammy, mara ya kwanza aliteuliwa 2020 kuwania kitengo cha Wimbo Bora Duniani.

    Hapo awali ilijulikana kama kitengo cha kimataifa cha Albamu Bora ya Muziki duniani, lakini kitengo hicho kilipewa jina "kuifanya iwe ya kisasa zaidi na inayojumuisha wasanii zaidi.

    Burna Boy amepangiwa kutumbuiza na wasanii wengine walioteuliwa kuwania tuzo hiyo kama vile Camilo na bendi ya Afro-Peruvian Jazz Orchestra miongoni mwa wengine.

    Burnaboy

    Wengine walioteuliwa kuwania kitengo hicho ni pamoja na kundi la Tuareg Tinariwen, kundi la muziki wa Kiafrika lenye makao yake mjini New York Antibalas, Mbrazili mwenye asili ya Marekani Bebel Gilberto,na Mchezaji wa sitar wa Uingereza na India Anoushka Shankar.

    Soma zaidi:

  9. Wapenzi wa Rhumba wamuomboleza Josky Kiambukuta

    Siku moja baada ya kutangazwa kwa kifo cha Josky Kiambukuta Londa,msanii mkongwe wa muziki wa rhumba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mashabiki wake wamekuwa wakitumia mitandao kumuomboleza.

    Alipata umaarufu alipojiunga na bendi ya TPOK Jazz kati ya miaka 1960 na 1980 ambapo alichangia pakubwa katika utunzi na uimbaji wa nyimbo kadhaa maarufu ukiwemo ule wa Chandra.

    Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, alisema bara la Afrika limepoteza mmoja wa wasanii mahiri na kuwapa pole jamaa zake marafiki na mashabiki.

    View more on twitter

    Kwa mujibu wa familia yake Kiambukuta,72, alifariki siku ya Jumapili baada ya kuugua kwa muda mfupi katika hospitali moja mjini Kinshasa.

    Katibu Mkuu wa Muungano wa wafanyakazi nchini Kenya Francis Atwoli, aliandika: Lala salama...

    Ulitufanya tufurahie na wakati umewadia urudi nyumbani.... katika Twitter.

    View more on twitter
  10. Bilionea Mackenzie Scott aolewa na mwalimu

    MacKenzie Scott

    Bilionea MacKenzie Scott, mtalaka wa mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezoz ameolewa na mwalimu wa sayansi katika shule ya watoto wake .

    Bi Scott ni mmoja wa wanawake tajiri zaidi duniani na ametoa zaidi ya dola bilioni nne ya mali yake.

    Taarifa ya kuolewa kwake na Dan Jewett ilifichuliwa kupitia tovuti ya kutoa misaada.

    ‘’Dan ni mtu mzuri, nawatakia kila la heri,’’ Bwana Bezos alisema katika taarifa.

    Bi Scott, ambaye thamani ya utajiri wake ni karibu dola bilioni 53 kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya Forbes, amesema nia yake ni kutoa sehemu kubwa ya mali hiyo.

  11. Karibu katika matangazo ya mubashara leo Jumatatu 08.03.2021