Othman Masoud Othman: Hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika serikali ya umoja wa kitaifa

Othman Masoud Othman: Hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika serikali ya umoja wa kitaifa

Ni mwaka mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa makamu wa rais wa kwanza wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, katika mahojiano maalumu makamu wa sasa wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman amemwambia mwandishi wetu Aboubakar Famau kwamba, mpaka sasa hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika serikali ya umoja wa kitaifa kwa sababu ya kukosekana kwa utashi wa kisiasa miongoni mwa viongozi.