Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

  1. Na mpaka hpo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Ni wakati wa kufanya maamuzi magumu, Rais Ruto anawaambia Wakenya

    g

    Rais wa Kenya William Ruto amesema utawala wake umekabiliwa na hali ngumu huku ukijitahidi kutekeleza ahadi zilizotolewa kwa Wakenya.

    Akihutubia Wakenya kuhusu hali ya taifa taifa katika Bunge la nchi hiyo, Bw Ruto ameitaja hali ngumu ya uchumi inayopelekea kupanda kwa garama ya maisha kama kikwazo cha utekezaji wa ahadi zake kwa Wakenya na akawataka wakaze mikanda.

    Akizungumzia kuhusu garama ya maisha inayotokana na mfumuko wa bei za bidhaa Bw Ruto amesema kuwa inasababishwa na suala la usalama wa chakula.

    "Gharama ya maisha sio jambo la kufikirika. Lipo katika familia zote. Mojawapo ya hatua muhimu zaidi katika kushughulikia gharama ya juu ya maisha ni mkakati wa kusaidia uzalishaji wa kilimo katika sekta mbalimbali za mazao ya chakula na biashara pamoja na minyororo ya thamani ya mifugo,” amessema Rais Ruto.

    "Nimejitolea kuweka aibu ya njaa nyuma yetu mara moja na kwa wote. Tulianzisha mpango wa usajili wa wakulima na ruzuku ya mbolea nchini kote ambao umewezesha kupatikana kwa mifuko milioni 5.5 kwa wakulima kote nchini Kenya. Tumeendelea kupunguza gharama ya mbolea kutoka KSh6 500 hadi 2500‘’, aliongeza.

    Akizunguzia suala la gharama ya unga wa mahindi, Bw Ruto amesema serikali yake imefanikiwa kupunguza bei ya unga wa mahindi hadi shilingi 145 kwa kilo.

    Amesema serikali yake imetambua matatizo ya kiuchumiyanayotokana na sababu za nje ya nchi shinikozo za kifedhana imeanza safari ya kuyapatia suluhu.

  3. Watu wa Ogiek wanafurushwa kinyume cha sheria - wanasheria

    xx

    Serikali ya Kenya inawafurusha kinyume cha sheria jamii ya wawindaji kutoka katika ardhi yao ya asili ili kufaidika na miradi ya kupambana na hewa chafu, wanasheria wa haki za binadamu wanasema.

    Mamia ya watu wa Ogiek wanaondoshwa katika Msitu wa Mau, wanasema wawakilishi wao.

    Kiongozi wa jamii hiyo, Daniel Kobei alisema Askari wa msitu wakiwa na silaha "wanavunja nyumba kwa shoka na nyundo."

    Serikali ya Kenya kwa upande wake inasema operesheni hizo ni za kulinda mazingira.

    Soko la kimataifa la kaboni huruhusu nchi kuzalisha hewa chafu na kulipa nchi zenye misitu ili kufyonza hewa hiyo kupitia miti.

    Hatua ya uondoshaji ilioanza tarehe 2 Novemba inaendelea na ilianza bila onyoa, kwa mujibu wa Kobei. Hadi sasa takriban watu 700, nusu wakiwa wanawake na watoto wameathirika.

  4. Mahakama ya Kenya yasitisha tozo mpya ya vitambulisho

    Gloria Aradi

    BBC News, Nairobi

    Mapema mwaka huu Upinzani uliongoza maandamano makubwa kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.
    Image caption: Mapema mwaka huu Upinzani uliongoza maandamano makubwa kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.

    Mahakama Kuu ya Kenya imezuia tozo mpya ya vitambulisho vya taifa ambayo ilikuwa imezua gumzo kali.

    Ombi la daktari wa upasuaji Magare Gikenyi lilisema kuwa serikali iliwasilisha tozo hiyo kwa "njia isiyo na msingi na ya kiholela".

    Ombi hilo lilisema kuwa tozo hiyo itawazuia "raia wa kawaida" kupata vitambulisho vya kitaifa.

    Vitambulisho vilikuwa vikitolewa bila malipo lakini ada ya shilingi 1,000 za Kenya ($6; £5) ilianzishwa bila maelezo yoyote.

    Gharama ya kubadilisha vitambulisho pia imeongezeka mara 20 hadi shilingi 2,000.

    Wakenya tayari wanajitahidi kukabiliana na gharama ya maisha, na kuanzishwa, au kuongezwa kwa malipo tofauti huku serikali, ikijaribu kuongeza mapato yake.

    Baadhi ya Wakenya wamelalamikia malipo ya juu zaidi kwa huduma za serikali ambazo wanaamini tayari zinafadhiliwa na kodi wanayolipa.

  5. Uingereza inashutumiwa kwa 'kutoeleza ukweli halisi' baada ya msomi wa Chevening kuhofiwa kuuawa Gaza

    Tom Bateman

    Mwandishi wa Mashariki ya Kati

    FCDO
    Image caption: Dkt Maisara Al Rayyes (Kulia) na mchumba wake wote ni wasomi wa zamani wa Chevening

    Daktari mmoja wa Kipalestina aliyefuzu kutoka kwa mpango wa kifahari wa ufadhili wa masomo katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza anahofiwa kuuawa pamoja na baadhi ya jamaa zake katika shambulio la anga la Israel huko Gaza, wenzake wanasema.

    Dkt Maisara Al Rayyes, 30, alipigwa picha na Waziri wa Mambo ya Nje James Cleverly baada ya kukutana naye pamoja na wahitimu wengine wa mpango huo miezi miwili iliyopita.

    Alikwama chini ya vifusi vya jengo la ghorofa sita ambalo lilibomolewa katika Jiji la Gaza Jumapili usiku.

    FCDO

    BBC imefahamu kuwa suala la jinsi Uingereza ilivyoshughulikia wa kisa chake limeibua hasira miongoni mwa baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya mambo ya nje, huku kukiwa na malalamiko mengi juu ya kushindwa kuangazia kwa uwazi idadi ya vifo vya raia huko Gaza.

    Pia kumezua mzozo mkali kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa zamani na wanachama wa masomo.

    Dtk Al Rayyes alikuwa mhitimu wa mpango wa Chevening Scholarship, mpango wa wasomi unaoendeshwa na Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, na Jumuiya ya Madola na Ofisi ya Maendeleo (FCDO).

    Ofisi ya Mambo ya Nje siku ya Jumatano ilisema "imefadhaika" natoa rambirambi kwa familia iliyosalia na "Jumuiya ya Wahitimu wa Chevening" juu ya kifo cha Dk Al Rayyes lakini haikutoa maelezo yoyote juu ya kile kilichompata, au wapi.

    Chapisho hilo lilizua ukosoaji mkubwa kutoka kwa watumiaji kwenye X, ambayo hapo awali ilijulikana kama Twitter, ikiwa ni pamoja na wafanyikazi wenzake wa zamani wa matibabu ambao waliishutumu Uingereza kwa kujaribu kuzuia ukosoaji wowote wa Israeli.

  6. Vita vya Gaza: Misri inalaani ukimya wa jamii ya kimataifa kuhusu ukiukaji wa sheria za kimataifa wa Israel.

    Kila saa, watoto 6 na wanawake 7 wanauawa Gaza, kulingana na Mamlaka ya Palestina.

    Misri imelaani vikali "kimya cha kimataifa" kuhusu ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu unaofanywa na Israel katika maeneo ya Palestina.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry alikuwa akizungumza Alhamisiwakati wa mkutano wa kibinadamu kuhusu Gaza huko Paris. Amesema: "Kile ambacho serikali ya Israel inafanya kinapita zaidi ya haki ya kujilinda," akishutumu "dhamiri ya kimataifa."

    Wakati hayo yakijiri Polisi wa Israel wawakamata viongozi wa kisiasa kabla ya maandamano ya kupinga vita mjini Nazareti.

    Polisi wa Israel wamemkamata Muhammad Baraka, mkuu wa Kamati Kuu ya Ufuatiliaji, kundi linalowakilisha raia wa Israel wenye asili ya Palestina.

    Baraka alikamatwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, katika mji wa Nazareth, wakati akielekea kushiriki maandamano ya kupinga vita dhidi ya Gaza, na kutaka kusitishwa kwa mapigano, wakati ambapo wawakilishi na wajumbe wa kamati hiyo walishutumu polisi. ya kunyamazisha sauti zinazopinga vita.

    Baadaye iliripotiwa kuwa Baraka alikuwa katika idara ya uchunguzi ya Bisan.

    Viongozi miongoni mwa raia wa Palestina wa Israel wamelaani kile walichokitaja kuwa "sera za kuadhibu" zilizowekwa na mamlaka juu yao kutokana na vita vya Gaza.

    g
  7. Habari za hivi pundeWizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema idadi ya waliofariki Gaza imeongezeka hadi 10,812

    Takriban watu 10,812, wakiwemo watoto 4,412, wameuawa huko Gaza tangu mashambulizi ya Oktoba 7 nchini Israel, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza inasema.

    Idadi ya Jumla ya awali iliyotolewa na wizara hiyo jana ilikuwa 10,569.

    Israel inapinga usahihi wa nambari hizo, lakini Shirika la Afya Ulimwenguni linaamini kuwa takwimu hizo ni za kuaminika.

  8. 'Mapigano ya halisi ya bunduki' karibu na hospitali ya Al Quds huko Gaza City

    Rushdi Abu Alouf

    Akiripoti kutoka Khan Yunus

    g
    Image caption: Eneo karibu na hospitali, kama lilivyoonekana tarehe 30 Oktoba

    Mapigano katika Mji wa Gaza yanazidi kuchacha. Kuna vita karibu na hospitali ya Al Quds huku vifaru vikisonga karibu na hospitali hiyo.

    Mawasiliano ni magumu, lakini nilikuwa nikizungumza na mtu asubuhi hii ambaye alisema ni "vita vya kweli vya kufyatua risasi" katika eneo hilo , anasema.

    Majengo mengi katika kitongoji hicho yalilengwa na jeshi la Israeli mwanzoni mwa mashambulio ya ulipizaji kisasi dhidi ya shambulio la Hamas mnamo 7 Oktoba.

    Eneo hili lililipuliwa kwa bomu kutoka angani kwa siku nyingi. Sasa linapigwa mabomu kutoka baharini na kwa vitengo vya mizinga ardhini.

    d
    Image caption: Matokeo ya uvamizi huo, Alhamisi asubuhi

    Wakati huo huo katika Ukingo wa Magharibi, idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Israel huko Jenin usiku kucha imeongezeka hadi wanane, wizara ya afya ya Palestina inasema.

    Wizara hiyo awali ilisema Wapalestina sita waliuawa wakati wa uvamizi huo.

    Jeshi la Israel limethibitisha kuwa lilikuwa likifanya mashambulizi ya kukabiliana na ugaidi huko Jenin na kwingineko katika Ukingo wa Magharibi, likisema kuwa wameharibu na kunyang'anya silaha.

    Tangu kuanza kwa vita, zaidi ya Wapalestina 150 wakiwemo watoto 44, wameuawa katika Ukingo wa Magharibi na vikosi vya Israel, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu OCHA inasema.

    Unaweza pia kusoma:

  9. Kwa picha: Wakazi wa kaskazini mwa Gaza wakiondoka kuelekea kusini

    Jeshi la Israel limesema leo kuwa limefungua tena barabara ya Salah al-Din Kreider kwa muda wa saa sita, kuwaruhusu Wapalestina walioko kaskazini mwa Gaza kuondoka kuelekea kusini.

    Jana, takriban watu 50,000 waliweza kuondoka kaskazini kwa njia hii, shirika la Umoja wa Mataifa la kibinadamu lilisema, ikiwa ni idadi kubwa zaidi katika siku moja.

    Hizi hapa picha za jinsi watu wanavyoondoka kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini.

    g
    h
    f
  10. Watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa kuwa Wakatoliki, wazazi wa ubatizo, Vatican inasema

    g
    Image caption: Papa Francis amejaribu kulifanya Kanisa liwe na ukarimu zaidi kwa watu wa jumuiya ya LGBT bila kubadili mafundisho ya Kanisa.

    Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa , ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilisema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.

    Idara hiyo, inayojulikana kama Dicastery of the Doctrine of the Faith, haikuwa wazi hata hivyo, katika kujibu swali la ikiwa wenzi wa jinsia moja wanaweza kuruhusiwa kupata ubatizo wa Kanisa kwa ajili ya mtoto aliyeasiliwa au ule uliopatikana kupitia mama mlezi.

    Askofu Jose Negri wa Santo Amaro nchini Brazili alituma kwa ofisi ya mafundisho maswali sita mnamo Julai kuhusu watu wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia (LGBT ) na ushiriki wao katika sakramenti za ubatizo na ndoa.

    Kurasa hizo tatu za maswali na majibu zilitiwa saini na mkuu wa idara hiyo, Kadinali wa Argentina Víctor Manuel Fernández, na kuidhinishwa na Papa Francis mnamo Oktoba 31.

    Ziliwekwa kwenye tovuti ya idara hiyo Jumatano kwa kutumia neno la Kiitaliano "transsexuals".

    Francis, mwenye umri wa miaka 86, amejaribu kulifanya Kanisa liwe na ukarimu zaidi kwa watu wa jumuiya ya LGBT bila kubadili mafundisho ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na msemo mmoja kwamba kuvutia watu wa jinsia moja si dhambi bali ni dhambi ni kitendo chenyewe cha kushiriki mapenzi ya jinsi moja.

    Katika kujibu swali la kama watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa, ofisi ya mafundisho ilisema wanaweza kwa masharti fulani na mradi tu "hakuna hatari ya kusababisha kashfa ya umma au kuchanganyikiwa miongoni mwa waumini".

    Unaweza pia kusoma:

  11. Israel yasema ilipigana kwa saa kumi kabla ya kuteka 'ngome' ya Hamas.

    g
    Image caption: Picha kutoka kwa video ya vita, iliyotolewa na IDF

    Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limetangaza kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba vikosi vyake viliteka ngome ya Hamas huko Jabalia kaskazini mwa Gaza.

    Lilisema lilitumia saa 10 kupigana, ambapo waliwashinda magaidi wa Hamas na kukamata silaha nyingi na kuharibu njia za chini ya ardhi za magaidi.

    Haya yanajiri wakati shirika la habari la Palestina Wafa likiripoti kuwa ndege za Israel zilishambulia kwa mabomu na kuharibu nyumba moja katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia na baadhi ya watu waliokuwemo wamekwama chini ya vifusi vya jengo hilo.

    Shirika hilo limesema pia kwamba watu wengi walijeruhiwa katika mji wa Gaza.

    BBC haikuweza kuthibitisha ripoti hizo.

    Jeshi la Israel hapo awali lilisema kuwa Hamas limepoteza udhibiti wa eneo la kaskazini la Gaza na kwamba vikosi vyake vimeingia katika mji wa Gaza.

    Unaweza pia kusoma:

  12. Afisa wa polisi aliyepewa £30,000 kama fidia kwa kuvuliwa nguo zake za ndani wakati wa mafunzo

    g

    Mahakama nchini Uingereza imemuamuru afisa wa polisi kulipwa fidia ya pauni 30,000 kwa kumvua nguo za ndani wakati wa mazoezi baada ya muathiriwa kusema kuwa 'aliokolewa'.

    Rebecca Kalam alikuwa ameishutumu idara ya polisi kwa kutumia lugha ya ngono na matusi . Kesi hiyo iliendeleana akashinda.

    Katika mahojiano ya kipekee na BBC, Rebecca Kalam alisema 'amehuzunishwa' kwamba unyanyasaji na ubaguzi aliokumbana nao haukukomea kwake tu.

    "Polisi wa West Midlands wamekubali kuwajibika kikamilifu kwa makosa yake mengi, lakini hakuna ulinzi wa wazi au mabadiliko ya miendendo kwa maafisa wake wa kike," alisema.

    Rebecca Kalam ni mkaguzi wa zamani wa uchunguzi na alijiunga na jeshi la polisi mnamo Septemba 2008.

    Alijiunga na Kitengo cha udhibiti wa Silaha mnamo 2012 na kustaafu kwa sababu za kimatibabu mnamo Julai 2023.

  13. Kundi la Hamas ladai kuharibu magari ya kivita ya Israel

    Hapo awali, Israel ilitoa taarifa kuhusu mapigano huko Gaza, ikisema imechukua udhibiti wa "ngome ya Hamas" kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, magharibi mwa Jabalia, baada ya mapigano ya masaa 10.

    Hamas sasa pia imetoa taarifa, huku tawi lake la kijeshi, Brigedi za Al-Qassam, likidai kuwa:

    • Iliharibu magari matatu ya Israeli na tingatinga karibu na kambi ya Al-Shati, inayojulikana pia kama kambi ya Pwani.
    • Imeharibu kifaru ya Israel kaskazini mwa Sheikh Radwan katika mji wa Gaza
    • Iliharibu Kifaru ya Israel karibu na eneo la Al-Tawam, kaskazini mwa Gaza City

    Wakati huo huo, Vikosi vya Al-Quds - kutoka kundi la Kipalestina la Islamic Jihad - vinadai kushambulia kwa mabomu magari ya Israel katika kambi ya Ansar mjini Gaza.

    Pia vinadai kurusha makombora katika mji wa Ashdod nchini Israel, ambapo ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika.

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha baadhi ya madai kutoka uwanja wa vita.

  14. Habari za hivi pundeKivuko cha Rafah kimefungwa leo asubuhi

    .

    Tunaendelea kukujuza taarifa kuhusu vita vya Israel na Gaza na habari za hivi punde ni kwamba kivuko cha mpaka cha Rafah bado kimefungwa kufikia asubuhi ya leo.

    Hamas wanasema wanataka watu zaidi waliojeruhiwa waruhusiwe kutoka Gaza kupitia kivuko hicho kabla ya raia zaidi wa kigeni kuruhusiwa kuondoka.

    Kivuko kati ya Gaza na Misri - ambapo misafara ya misaada imekuwa ikiingia na raia wa kigeni na watu waliojeruhiwa wakitoka - pia kilifungwa jana kwa watu, mashirika ya Umoja wa Mataifa yalisema.

    Walisema kimefungwa kwa sababu ambazo hazijathibitishwa.

    Tutakufahamisha habari zaidi kutoka kivuko cha Rafah kadri tunavyozipokea.

    Unaweza pia kusoma:

  15. Mzozo wa Israel na Palestina: Je, kuna maeneo salama Gaza?

    Video content

    Video caption: Mzozo wa Israel na Palestina: Je, kuna maeneo salama Gaza?

    Jeshi la Israel IDF limetoa maelekezo kwa raia kuhamia eneo la kusini mwa Gaza kwa usalama wao.

    Lakini uchunguzi wa BBC Verify umethibitisha kwamba kuna mashambulizi ya angani ambayo yamelenga maeneo ya karibu na sehemu ambazo raia waliambiwa wahamie.

    Elizabeth Kazibure anaeleza zaidi.

  16. 'Majasusi wa Kikomunisti' wa China watiwa kizimbani huko Taiwan

    .

    Taiwan inalenga watu wanaodaiwa kuwa ni "majasusi wa kikomunisti" wa China kabla ya uchaguzi muhimu wa rais, ambapo uhusiano wa kisiwa hicho na Beijing utapigiwa kura.

    Taiwan na China zimekuwa zikifanyiana ujasusi tangu mwaka 1949, wakati wazalendo wa China walipoanzisha serikali tofauti mjini Taipei wakipinga Uchina wa kikomunisti wa Mao Zedong.

    Inasema katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, mamlaka za Taiwan zimetoa mfululizo wa mashtaka na hukumu - uthibitisho kwamba mkakati wa kijasusi wa Beijing umeongezeka na kupanuka zaidi ya duru za kijeshi za wasomi.

    Kanali mstaafu wa jeshi la wanahewa Liu Sheng-shu alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela mwezi Oktoba kwa kuendesha kikosi cha kijasusi cha kijeshi huko Beijing.

    Takriban watu 16 wameshtakiwa kwa ujasusi wa China tangu mwanzo wa mwaka huu, ikilinganishwa na kesi 44 za ujasusi zilizosajiliwa na Ofisi ya Upelelezi ya Wizara ya Sheria ya Taiwan kati ya 2013 na 2019.

    Haya yanajiri huku madai ya Uchina juu ya kisiwa hicho kinachojitawala yakigeuka kuwa ya vitisho zaidi, na kuongezeka kwa shinikizo la kijeshi na kisiasa.

    Beijing haijakataza uwezekano wa kutumia nguvu kuchukua kisiwa hicho, hata kama uungaji mkono wa Marekani kwa Taiwan umeongezeka zaidi.

    Ripoti zinaonyesha kuwa Beijing imekuwa ikipanua juhudi zake za kijasusi duniani, hasa dhidi ya Marekani. Na Washington pia imekuwa ikiongeza mkusanyiko wake wa kijasusi juu ya China.

    Taiwan ni shabaha rahisi ya majasusi wa China, anasema Grant Newsham, kanali mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani ambaye amehudumu kwa miongo kadhaa katika Indo-Pacific.

    Ukaribu na Uchina na ukweli kwamba WaTaiwani wengi wanazungumza lugha ya Kichina husaidia, lakini kisiwa hicho pia "hakina kanuni kazi sana" kuhusu kuadhibu ujasusi, anaongeza.

    "Hii ina athari kwa utayari wa kupeleleza Uchina, ikiwa unafikiria 'hatari za chini' sio mbaya sana."

    Bw Newsham pia anasema Taiwan haikuwa na mfumo thabiti wa kuzuia ufikiaji wa habari zilizoainishwa hadi hivi majuzi.

    "Ikiwa hutadhibiti taarifa nyeti na za siri vizuri sana... Unapaswa kutarajia huduma yoyote ya kijasusi ya kigeni inayostahiki kuipata. Hali imekuwa hivyo Taiwan kwa muda mrefu sana."

    Soma zaidi:

    Marekani inaihami vikali Taiwan kimya kimya

  17. Kenya inaongoza katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya Afrika

    .

    Watu katika baadhi ya nchi maskini zaidi na zenye matatizo duniani wameonekana kuwa watu wa kutoa misaada zaidi.

    Wakfu wa World Giving Index imesema Raia wa Indonesia,Ukraine na Kenya wana uwezekano mkubwa wa kuchangia misaada, kusaidia mgeni au kujitolea kwa wakati wao.

    Raia wa Uingereza ni miongoni mwa wanaochangia fedha nyingi zaidi lakini hawakotayari kusaidia watu ambao hawafahamu.

    Indonesia ndilo taifa ambalo linakisiwa kuwa watu wakarimu zaidi duniani, wakati inapokuja suala la kutoa na kuchangia Misaada. Hii ni kwa mujibu wa wakfu wa kutoa misaada ya kibinadam wa he Charities Aid Foundation (CAF).

    Ripoti hiyo ya CAF inayoratibu mpango wa uchangishaji kwa ajili ya misaada, ni moja ya utafiti wa kina uliowahi kutolewa, huku mamilioni ya watu wakihojiwa kote duniani tangu mwaka wa 2009.

    Uchunguzi wa mwaka huu ulikusanya maoni kutoka kwa nchi mia moja arubaini na mbili duniani ambako watu waliuzwa maswali matatu.

    La kwanza ikiwa je umewahi kumsaidia mgeni? umewahi kumpa fedha mgeni na swali la tatu ni je umewahi kujitolea kumsaidia mgeni katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita?

    Licha ya kuwa raia wa taifa la Uingereza ndio wanaochangia zaidi, harakati za kutoa misaada hasa fedha, taifa hilo limeshuka hadi nafasi ya hamsini na nane katika orodha ya mataifa ambayo raia wake wanajitolea kwa kazi za hiari na pia kushuka hadi nafasi ya 112 katika orodho ya nchi ambazo raia wake wanaweza kumsaidia mgeni.

    Mataifa yaliyopanda tena hadi nafasi kumi bora

    Katika orodha ya nchi karimu zaidi katika kanda ya afrika, Kenya inaongoza huku iikishikilia nafasi ya tatu duniani ikifuatwa na Liberia na Nigeria.

    Katika orodha ya nchi zinazochangia fedha zaidi harakati za kutoa misaada duniani, Myanmar inashika nafasi ya kwanza, ikifuatwa na Indonesia, Uingereza, Ukraine na Malta.

    Katika ya nchi ambazo raia wao wako tayari kuwasaidia wageni, Jamaica inaongoza ikifuatwa na Liberia, Libya, Nigeria, Kuwait, Senegal, Kenya, Marekani na Sierra Leonne.

    Na katika orodha ya nchi ambazo raia wake wako tayari kujitolea muda wao Liberia inashika nafasi ya kwanza duniani ikifuatwa na Indonesia, Tajikistan, Kenya na Sri Lanka.

    Marekani imeshika nafasi tana mwaka huu, Canada ya nane, New Zealand nayo ikiwa katika nafasi ya kumi.

    Neil Heslop ambaye ni afisa mkuu mtendaji wa wakfu huo wa kutoa misaada wa Charities Aid amesema kuwa ripoti ya mwaka huu imetoa taswira tofauti katika nchi mbali mbali hasa Uingereza.

    Ameongeza Uingereza imesalia kuwa nchi karimu zaidi duniani kwa kuchangia hazina mbali mbali za kutoa misaada hata hali ikiwa ngumu.

    Amesema kutoa au kuchangia wakati wa dhiki ni njia moja ya kujenga mahusiano kati ya jamii mbali mbali kote duniani na kwamba kuna haja ya jamii zote kushirikiana.

    Tunahitaji kila mara kukuza utamaduni wa kutoa ili kutuleta sote pamoja na kupata pesa zaidi kutiririka ili kusaidia jamii zenye shida kote duniani.

    Ameongeza kuwa ni jukumu letu sote, lakini serikali inaweza kuchukua uongozi kwa kuandaa mkakati wa kitaifa wa na utoaji wa hisani.

    Pia unaweza kusoma:

    Nchi 10 bora kwa usawa wa kijinsia: Afrika ipo moja

  18. Mkuu wa haki za binadamu wa UN awashutumu Israel na Hamas kwa uhalifu wa kivita

    .

    Pande zote mbili katika mzozo wa Gaza na Israel zimefanya uhalifu wa kivita, kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu amesema.

    Akizungumza siku ya Jumatano katika kivuko cha mpakani cha Rafah, Volker Türk alisema: Ukatili ambao ulifanywa na makundi ya wapiganaji wa Kipalestina tarehe saba Oktoba ulikuwa mbaya, wa kikatili na wa kushtua.

    Aliongeza: "Ulikuwa uhalifu wa kivita kama vile kuendelea kuwashikilia mateka.

    "Adhabu ya pamoja ya Israel dhidi ya raia wa Palestina pia ni sawa na uhalifu wa kivita, kama vile uondoaji wa nguvu usio halali wa raia. Mashambulio ya mabomu ya ndani ya nchi ya Israel yameua, kulemaza na kujeruhi hasa wanawake na watoto."

    Türk alielezea shambulio la mabomu katika Ukanda wa Gaza kama "kusababisha madhara makubwa kwa maisha ya binadamu, na kwa raia".

    Unaweza pia kusoma

  19. Iran yamfunga jela miaka mitano mtalii wa Ufaransa Louis Arnaud

    .

    Mtalii wa Ufaransa aliyezuiliwa nchini Iran kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa tuhuma za usalama wa taifa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

    Louis Arnaud, mshauri wa benki, alikamatwa mnamo Septemba 2022 - akishutumiwa kwa kushiriki katika maandamano na kuchangia propaganda dhidi ya serikali.

    Amekuwa akishikiliwa katika gereza maarufu la Evin katika mji mkuu, Tehran, tangu wakati huo.

    Serikali ya Ufaransa siku ya Jumatano ilitoa wito wa kuachiliwa kwake mara moja.

    "Hukumu hii, ambayo haina chochote cha kuunga mkono na kukosekana kwa ufikiaji wowote wa wakili, haikubaliki," ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya nchi.

    Familia ya bwana Arnaud ilithibitisha hukumu hiyo na kusema kwamba hakuwa na hatia kwa mashtaka yote - ikielezea hukumu hiyo kuwa ni "mashambulizi dhidi ya haki za binadamu na uhuru wa mtu binafsi", kulingana na shirika la habari la AFP.

    Walisema katika taarifa yao kwamba alijiepusha na maandamano yaliyozuka kote nchini Septemba mwaka jana kufuatia kifo cha Mahsa Amini akiwa mikononi mwa polisi.

    "Hakuna wakati alifanya kwa nia ya kisiasa au uzembe."

    Wapendwa wake waliwahi kueleza huko nyuma kwamba alikuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa kwa mmoja wa kundi la wabeba mizigo aliokutana nao katika safari zake walipozuiwa na vikosi vya Islamic Revolutionary Guard. Wengine wote waliokuwa kizuizini, wakiwemo wageni wengine, wameachiliwa.

    Familia ya Bw Arnaud iliongeza siku ya Jumatano kwamba amekata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

    Kufikia sasa hakuna maoni yoyote kutoka kwa mamlaka ya Iran.

    Serikali za Magharibi zinaishutumu Tehran kwa kuwaweka kizuizini wageni na raia wa nchi mbili kwa misingi ya uwongo ili kutumika kama silaha wakati wa mazungumzo.

    Gereza la Evin, ambako Bw Arnaud anazuiliwa, limekuwa likikosolewa kwa muda mrefu na makundi ya kutetea haki za binadamu. Human Rights Watch imeshutumu mamlaka katika gereza hilo kwa kutumia vitisho vya kuteswa na kufungwa kwa muda usiojulikana, pamoja na kuhojiwa kwa muda mrefu na kunyimwa huduma za matibabu kwa wafungwa.

    Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu la Iran (HRANA) linakadiria kuwa karibu watu 20,000 wamezuiliwa nchini humo kuhusiana na maandamano hayo.

    Pia unaweza kusoma:

    Iran yaweka kamera ili kuwanasa wanawake ambao hawajavaa hijabu

  20. Wakenya wakasirishwa na ongezeko la tozo katika baadhi ya huduma za serikali

    Wakenya wamekasirishwa na ongezeko la tozo lililofanywa na serikali kupitia Idara ya Uhamiaji na Huduma kwa Raia, katika baadhi ya huduma zake ikiwemo hati ya kusafiria, kitambulisho, kibali cha kazi, maombi ya cheti cha kuzaliwa na kifo na huduma nyinginezo.

    Katika notisi maalum ya gazeti la serikali ya Novemba 7, 2023, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani Prof. Kithure Kindiki alitangaza mabadiliko hayo ya tozo.

    Mfano ombi la kawaida la pasipoti ya kurasa 34 imepanda hadi Ksh.7,500 kutoka Ksh.4,500.

    Pasipoti ya kawaida ya kurasa 50 sasa itagharimu waombaji Ksh.9,500 kutoka Ksh.6,000 huku ada ya maombi ya pasipoti ya kawaida ya kurasa 66 ikipanda kwa Ksh.5,000 hadi Ksh.12,500.

    .

    Ada ya pasipoti ya kidiplomasia ya kurasa 50 imeongezeka maradufu hadi Ksh.15,000 kutoka Ksh.7,500 ilhali tozo ya pasipoti ya huduma ya kurasa 32 ikisalia kuwa Ksh.3,000.

    Kubadilisha pasipoti iliyopotea kutagharimu Ksh.20,000, ongezeko la Ksh.8,000 kutoka ada ya awali huku kubadilisha pasi halali iliyokatwa kutagharimu Ksh.20,000 kutoka Ksh.10,000.

    Bei ya vibali vya muda, vyeti vya utambulisho na hati za usafiri wa dharura itasalia kuwa vilevile Ksh.300, Ksh.3,000 na USD 20 (takriban Ksh.3031 kulingana na kiwango cha ubadilishaji cha sasa) mtawalia.

    Zaidi ya hayo, hati za kusafiria za wakimbizi zitatolewa bila gharama yoyote.

    Waombaji wa vitambulisho kwa mara ya kwanza watalipa Ksh.1,000 ili kupata hati ambazo zilitolewa awali bila gharama yoyote.

    Ubadilishaji wa vitambulisho vilivyopotea utahitaji malipo ya Ksh.1,000, kuashiria ongezeko mara kumi kutoka Ksh.100 .

    Hata hivyo kwenye mitandao ya kijamii kama vile Twitter, Wakenya walionyesha hisia tofauti kufuatia hatua hiyo.

    View more on twitter
    View more on twitter
    View more on twitter