Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Asha Juma na Ambia Hirsi

time_stated_uk

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Kwaheri.

  2. Tanzania yazima mashine tano za kuzalisha umeme

    Alfred Lasteck

    BBC News, Dar es Salaam

    XX

    Mamlaka nchini Tanzania imezima mashine tano za kuzalisha umeme baada ya mahitaji ya nishati hiyo kuwa chini huku uzalishaji ukiwa ni mwingi.

    Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati yaliyofanyika jijini Dodoma, alinukuliwa ofisa wa shirika la umeme nchini humo, Tanesco aliyesema, “ Waziri Mkuu, kwa sasa hivi tunavyoongea tuna mitambo karibu mitano ipo nje, haifanyi kazi yoyote ni kwamba tu mahitaji yapo chini, na uzalishaji upo mwingi kwahiyo tumeiweka tu stand-by kwa ajili ya kusubiria mahitaji yakiwa juu ili tuiwashe…

    Kati ya mitambo mitano iliyotajwa kuzimwa na Tanesco, minne ipo katika Kituo cha Kinyerezi I na mmoja katika Kituo cha Ubungo III.

    Aidha, katika kuelezea uimarikaji wa huduma ya nishati nchini humo, Waziri Mkuu alisema mtambo mkuu wa Kituo cha Umeme cha Julius Nyerere umeongeza umeme nchini na kufanya jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na maeneo mengine nchini kuwa na umeme wa kutosha.

    Inaelezwa kuwa Kituo hicho cha Julius Nyerere kitakapokamilika kitazalisha megawati 2,115.

  3. Wakenya waonywa dhidi ya mvua zaidi

    .

    Mkurugenzi wa Mamlaka ya hali ya anga nchini Kenya David Gikungu amewaonya Wakenya kujiandaa kwa mvua kubwa ambayo inaweza kung’oa miti na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

    Bwana Gikungu pia alitoa ripoti ya viwango vya mvua ilionyesha maeneo tofauti mjini Nairobi.

    Alisema baadhi ya maeneo yatapokea mvua kidogo hali ambayo anasema huenda ikasababisha maporomo ya ardhi.

  4. Tanzania yakana madai ya unyanyasaji huku Benki ya dunia ikisitisha ufadhili

    Alfred Lasteck & Will Ross

    BBC News, Dar es Salaam & London

    Tanzania ni kivutio maarufu cha watalii
    Image caption: Tanzania ni kivutio maarufu cha watalii

    Serikali ya Tanzania imekanusha madai ya wanavijiji kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kwa lazima kama sehemu ya mradi wa upanuzi wa hifadhi ya taifa kusini mwa nchi hiyo.

    Siku ya Jumanne, Benki ya Dunia ilisema kuwa imesitisha ufadhili wake wa mradi wa utalii wa dola milioni150 katika Hifadhi ya Kitaifa ya Ruaha, ikisema ina wasiwasi mkubwa kuhusu madai hayo.

    "Serikali ya Tanzania haikiuki haki za binadamu wakati wa kutekeleza miradi yake yote, ikiwa ni pamoja na hii inayofadhiliwa na Benki ya Dunia," msemaji wa serikali Mobhare Matinyi aliiambia kituo cha shirika la utangazaji la serikali TBC.

    "Kilichotokea ni kwamba Benki ya Dunia ilipokea baadhi ya ripoti kutoka kwa mashirika ya kiraia ambayo yalitilia shaka mradi huo, wakidai baadhi ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika eneo hilo.

    Taarifa hizo si za kweli." Mradi huo unaojulikana kama Usimamizi Resilient wa Maliasili kwa Utalii na Ukuaji (Regrow), unalenga "kuboresha usimamizi wa maliasili na mali za utalii" kusini mwa Tanzania, Benki ya Dunia ilisema hapo awali.

    Bw Matinyi aliambia gazeti la ndani kwamba Benki ya Dunia kufikia sasa imetoa dola milioni 125 ya ufadhili wake kwa Regrow, ambayo ilizinduliwa mwaka wa 2017.

    Taasisi ya Taaluma ya Marekani ya Oakland iliripoti kwamba wanakijiji walibakwa na walinzi na walikuwa wakifukuzwa kutoka kwa ardhi yao kwa sababu hifadhi hiyo ilikuwa ikipanuliwa.

    Taasisi ya Oakland pia ilidokeza ripoti, kutoka kwa mbunge wa Tanzania na shirika la jamii, kwamba walinzi walidaiwa kuwaua wanakijiji.

  5. Argentina yataka waziri wa Iran kukamatwa kwa shambulio la bomu

    xx

    Argentina imeitaka Interpol kutoa notisi ya kukamatwa kwa waziri wa mambo ya ndani wa Iran, Ahmad Vahidi.

    Ombi hilo linakuja chini ya wiki mbili baada ya mahakama nchini Argentina kushikilia Iran kuhusika na shambulio la mwaka 1994 katika kituo cha jumuiya ya Wayahudi mjini Buenos Aires, ambapo watu 85 waliuawa.

    Bw Vahidi alikuwa Pakistan mapema wiki hii kama sehemu ya ujumbe wa Iran ambao sasa uko Sri Lanka.

    Argentina ilisema pia ilizitaka nchi hizo mbili kumzuilia Bw Vahidi.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Argentina ilisema katika taarifa kwamba Interpol imetoa kinachojulikana kama "noti nyekundu".

    Ingawa ilani nyekundu inawatahadharisha polisi katika nchi wanachama kuhusu wakimbizi wanaosakwa na kimataifa, haijumuishi hati ya kukamatwa.

    Interpol haiwezi kuwalazimisha polisi kumkamata mtu ambaye notisi nyekundu imetolewa, ni jukumu la nchi wanachama kuamua kumkamata.

  6. Kwa Picha: Tazama uharibifu uliofanywa na Farasi mjini London baada ya kuwaangusha waliokuwa wamewapanda na kutoroka

    Farasi watano wamefanya uharibifu mbaya ikiwemo kusababisha majeraha mjini London baada ya kuwaangusha waliokuwa wamewapanda na kutorokea katikati barabara za mji wa London mapema leo asubuhi.

    Wakati wa tukio hilo Farasi hao wanaaminika kugongana na magari kadhaa walipokuwa wakikimbia.

    .
    Image caption: Farasi mweupe aliwekwa alama nyekundu, ambayo inaweza kuwa damu
    .
    Image caption: Basi la watalii limeharibika kioo cha mbele baada ya mmoja wa farasi kugongana nacho
    .
    Image caption: Gari hili linaaminika kugongwa na mmoja wa farasi hao
    .
    Image caption: .Baiskeli hizi katika bustani ya Belgrave pia hazikuepuka
    .
    Image caption: Farasi mweusi anakimbia karibu na Teksi kwenye barabara za London
    .
  7. Mtoto wa Kiislamu adaiwa kuchapwa viboko kwa kuhudhuria ibada kanisani

    xx

    Watu saba wa familia moja ya Kiislamu mashariki mwa Uganda wamekamatwa na mamlaka kwa madai ya kumpiga msichana wa miaka 18 ambaye alihudhuria ibada ya kanisa, polisi wamenukuliwa wakisema.

    Msichana huyo anadaiwa kuchapwa viboko 100 na mjombake huku wajomba zake wengine watano wakimshikilia chini, tovuti ya habari ya Nile Post iliripoti.

    Picha zilizoonekana kuonyesha msichana huyo akipigwa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, na kuzua hisia kali miongoni mwa Waganda.

    Familia bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na tukio hilo. Wajomba wa msichana huyo walikamatwa pamoja na shangazi yake, ambaye ni mlezi wake mkuu, polisi walisema.

    Wataendelea kuzuiliwa wakisubiri uchunguzi, Samuel Semewo, kaimu msemaji wa polisi wa mkoa, alinukuliwa akisema na tovuti ya habari ya Daily Express.

    Bado haijabainika watashtakiwa kwa makosa gani, lakini Bw Semewo aliambia gazeti la Nile Post kwamba vitendo hivyo ni sawa na kushambulia au mateso.

    Pia aliliambia gazeti la Daily Monitor wanafamilia hao "walimpiga" msichana huyo "kwa viboko" na kwamba "alikuwa akiendelea kupata nafuu huku akisubiri kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu".

    Mwakilishi wa eneo hilo wa baraza la kitaifa la Waislamu alisema shambulio hilo linalodaiwa kuwa la kinyama na haliungwi mkono na kanuni za dini, gazeti la Daily Monitor liliripoti.

  8. Video: Tazama polisi wakimfukuza dereva aliyekuwa akiendesha gari bila kibali

    Video content

    Video caption: Tazama polisi wakimfukuza dereva wa gari kwa muda mrefu hadi wakamkamata
  9. Wachezaji wawili wa Ligi Kuu ya England wakamatwa kwa tuhuma za ubakaji

    Mpira

    Wanasoka wawili wa Ligi Kuu ya Uingereza wamekamatwa kwa tuhuma za ubakaji.

    Wawili hao, wote wakiwa na umri wa miaka 19, waliachiliwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi.

    Wachezaji hao wapo katika klabu moja, ambayo ilikataa kuzungumzia madai hayo.

    "Maafisa wamewakamata wachezaji wawili kufuatia ripoti ya ubakaji," msemaji wa polisi alisema.

    “Kijana wa miaka 19 alikamatwa kwa tuhuma za kushambulia na kusaidia ubakaji. Mwanaume wa pili mwenye umri wa miaka 19 alikamatwa kwa tuhuma za ubakaji. "Wote wawili wameachiliwa kwa dhamana ya polisi."

    Madai hayo yaliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la The Sun, ambalo lilisema shambulio hilo linadaiwa kutekelezwa siku ya Ijumaa.

    Haijajulikana iwapo wachezaji hao wamesimamishwa kazi kusubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi.

    Ligi Kuu ilianzisha mafunzo ya lazima ya idhini ya ngono kwa wachezaji na wafanyakazi mnamo 2022 kufuatia matukio ya hali ya juu yaliyohusisha wanasoka wa daraja la juu.

    Mnamo Novemba uchunguzi wa Panorama uligundua vilabu vya Ligi ya Premia viliendelea kuchezesha wanasoka wawili, huku wakijua walikuwa chini ya uchunguzi wa polisi kwa unyanyasaji wa kingono au majumbani.

  10. Marekani yawawekea vikwazo wakuu wa wanamgambo Afrika Magharibi

    xx

    Viongozi kadhaa na wanachama wa makundi ya wapiganaji wa Kijihadi huko Afrika Magharibi wamewekewa vikwazo na Marekani kwa kuwashikilia raia wa Marekani.

    Wanajumuisha viongozi wa kundi lenye uhusiano na al-Qaeda la Jama'at Nusrat al-Islam wal-Muslimin (JNIM) na al-Murabitoun yenye makao yake nchini Mali.

    "JNIM inategemea utekaji nyara na kuzuiliwa kimakosa kwa raia ili kupata nguvu na kuzua hofu, na kuleta uchungu na huzuni kwa waathiriwa na familia zao," afisa wa Hazina Brian E. Nelson alisema katika taarifa.

    “Hazina itaendelea kutumia zana zote tulizonazo kuwawajibisha wale wanaotaka kuwaweka raia wetu mateka,” aliongeza.

    Wanamgambo walioidhinishwa walisaidia, kufadhili, au kuunga mkono utekaji nyara au kuwekwa kizuizini kimakosa kwa raia wa Marekani katika Afrika Magharibi, taarifa ya Hazina ya Marekani ilisema.

    Hazina ya Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje, ambazo ziliweka vikwazo hivyo, zilisema "mali na maslahi yote ya mali" zinazoshikiliwa na watu waliolengwa nchini Marekani "ilizuiwa".

    Wamarekani pia wamepigwa marufuku kufanya miamala na wanamgambo waliowekewa vikwazo,kutoka mataifa ya Mali, Algeria, Burkina Faso na Mauritania.

    Vikwazo hivyo vinakuja wakati eneo la Sahel lenye matatizo la Afrika Magharibi likipambana na wimbi la uasi kutoka kwenye makundi yenye uhusiano na Islamic State na al-Qaeda.

  11. Pochettino asema Chelsea 'ilikata tamaa' katika kipigo cha Arsenal

    Wachezaji wa Chelsea

    Kocha Mauricio Pochettino anasema timu yake ya Chelsea "ilikata tamaa" wakati wa kipigo cha 5-0 kutoka kwa Arsenal kwenye uwanja wa Emirates.

    Walikwenda mapumziko ya kipindi cha kwanza wakiwa nyuma kwa bao 1-0, lakini The Blues waliruhusu mabao manne katika kipindi kigumu cha dakika 18 katika kipindi cha pili na kuishia katika kipigo chao kizito zaidi katika mchezo wa London derby tangu 1986.

    Pochettino alikuwa amefanya mabadiliko matatu kwenye safu yake ya ulinzi kwenye mchezo huo, akiamua kuwapumzisha Trevoh Chalobah na Thiago Silva, huku Malo Gusto alipata jeraha wakati wa mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Manchester City Jumamosi.

    "Sio ngumu kuelezea," Pochettino alisema. "Kila mtu aliona hatukushindana tangu mwanzo wa mchezo.

    "Baada ya kukubali timu ilikuwa hafifu. Nimesikitishwa sana na jinsi tulivyoanza kwa sababu tunatakiwa kuwa na nguvu kamili na kushindana vyema.

    "Hatukuwa wakali na hatukuzingatia hali ambayo ni rahisi kupata suluhu. Ndio maana nimekatishwa tamaa."

    Chelsea walingia kwenye mechi hiyo baada ya kucheza mechi nane bila kushindwa kwenye Ligi ya Primia na nafasi ya nje ya kufuzu kwa Uropa msimu ujao.

    Lakini kipigo cha Jumanne, kikubwa zaidi msimu huu, kinawaacha nafasi ya tisa kwenye jedwali.

    "Tulikuwa tunazungumza wakati wa mapumziko ili kuanza kwa njia tofauti," aliongeza Pochettino. "Lakini hatukufanya hivyo. Tuliporuhusu bao la tatu timu ilikata tamaa. Ilikuwa ngumu kwao.

    "Tulishindana vyema dhidi ya Manchester City, ulikuwa mchezo mzuri sana. Lakini hatukushindana siku tatu baadaye. Labda hatukuwa freshi.

    "Sio sawa kuzungumzia wachezaji tunaowakosa. Tangu msimu uanze tumekuwa tukikosa wachezaji wengi kila baada ya wiki moja.

    "Timu ilionesha kutokuwa na uwezo wa kuzuia mashambulizi, hilo ndilo tatizo."

  12. Mafuriko yasababisha uharibifu mkubwa nchini Kenya

    xx

    Barabara zimegeuka kuwa mito katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, huku afisa wa ngazi ya juu akisema mafuriko "yameongezeka na kufikia viwango vya kutisha".

    Mvua kubwa imenyesha nchini Kenya katika siku za hivi karibuni, na kusababisha uharibifu mkubwa.

    Umoja wa Mataifa unasema kuwa takriban watu 32 wamepoteza maisha na zaidi ya 40,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mvua na mafuriko.

    Edwin Sifuna, ambaye ni Seneta wa Kaunti ya Nairobi, alizua taharuki kwenye mtandao wa kijamii wa X huku akichapisha picha zinazoonyesha mtaa mzima uliosombwa na mafuriko.

    Katika kilipu hiyo ya video, wakazi wanaonekana wakiwa wamenaswa kwenye paa la nyumba yao.

    Mamia ya wengine jijini Nairobi na maeneo ya karibu pia walikumbwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku kucha.

    "Tunahitaji huduma zote za dharura za kitaifa kuhamasishwa ili kuokoa maisha," Bw Sifuna alisema.

    Jumatano asubuhi, Shirika la Reli la Kenya lilisema mafuriko hayo yameathiri njia za reli, na hivyo kufanya kuwa vigumu kwa treni kufanya kazi.

    Kampuni hiyo ilisema hofu ya usalama iliilazimisha kusitisha huduma zake.

    Barabara kuu, zikiwemo ile ya Mombasa na Thika, zilijaa maji ya mafuriko, na kusababisha msongamano wa magari nyakati za asubuhi

    Barabara yenye shughuli nyingi ya Namanga, inayoelekea mpaka wa Tanzania, ilifurika baada ya Mto Athi ulio karibu kuvunja kingo zake Jumatano asubuhi.

    Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya linasema timu zake za kukabiliana na mafuriko zinafanya kazi katika maeneo mengi yaliyoathiriwa na mafuriko, zikihamisha familia kwenye usalama na kutoa afua nyingine za kuokoa maisha.

    Wakazi wa baadhi ya mashamba jijini Nairobi pia wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kuzama kutokana na mafuriko. Mvua inatabiriwa kuendelea kunyesha.

    xx
    Mwanamume mmoja jijini Nairobi amezama kwenye maji alipokuwa akiogelea kuwaokoa wakaazi waliokuwa wamekwama kwenye nyumba zao.
    Image caption: Mwanamume mmoja jijini Nairobi amezama kwenye maji alipokuwa akiogelea kuwaokoa wakazi waliokuwa wamekwama kwenye nyumba zao.
  13. Mwanasoka wa zamani Carlos Tevez alazwa hopitalini baada ya kuumwa kifua

    Carlos Tevez anafanyiwa uchunguzi hospitalini baada ya kupata maumivu ya kifua
    Image caption: Carlos Tevez anafanyiwa uchunguzi hospitalini baada ya kupata maumivu ya kifua

    Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Argentina Carlos Tevez amelazwa hospitalini baada ya kuumwa kifua.

    Tevez alipelekwa hospitalini mjini Buenos Aires siku ya Jumanne na atasalia hapo hadi vipimo vya afya vitakapokamilika.

    Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United, Manchester City na West Ham mwenye umri wa miaka 40 sasa ni kocha mkuu wa timu inayoshiriki ligi kuu ya Argentina Independiente.

    Independiente alisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa X, kwamba vipimo vya awali vya Tevez katika Hospitali ya Trinidad huko San Isidro "vilikuwa vya kuridhisha" lakini atalazwa hapo kwa wakati huu kama "tahadhari".

    Tevez, ambaye aliichezea Argentina mechi 76 kati ya 2004 na 2015, alichukua jukumu la kuinoa Independiente mnamo Agosti 2023.

    Hapo awali alikuwa kwa muda mfupi Rosario Central, baada ya kustaafu kama mchezaji mnamo Juni 2022 baada ya kipindi cha tatu na Boca Juniors.

    Tevez alicheza mechi 201 kwenye Ligi Kuu ya England kati ya 2006 na 2013 na kufunga mabao 84.

    Alishinda taji la Ligi Kuu mara mbili akiwa na United (2007-08 na 2008-09) na mara moja akiwa na City (2011-12).

  14. Nigeria yafunga shule za kifahari kutokana na unyanyasaji

    Maafisa wa Nigeria wamefunga shule ya kifahari katika mji mkuu, Abuja, kutokana na visa vya uonevu vinavyohusisha baadhi ya wanafunzi, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Video nyingi za wanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Lead British wakiwashambulia wanafunzi wenzao ziliibuka na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Jumatatu.

    Video hizo zilizua shutuma kali mtandaoni huku wazazi wenye hasira wakionekana kuvamia shule.

    Siku ya Jumanne, wakuu wa shule walitangaza kufungwa kwa shule hiyo kwa siku tatu ili kuwawezesha kuchunguza suala hilo.

    Kabiru Musa, afisa mkuu wa elimu, aliambia tovuti ya habari ya Punch kwamba Waziri wa Masuala ya Wanawake nchini Uju Kennedy-Ohaneye aliamuru kufungwa kwa shule hiyo.

    Katika taarifa yake, shule hiyo ilisema "ina wasiwasi mkubwa" kuhusu visa vilivyoripotiwa vya unyanyasaji, na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.

    Shule hiyo, iliyoanzishwa mwaka wa 2007, inatoa mtaala wa Uingereza uliochanganywa na mfumo wa elimu wa Nigeria.

    Imekadiriwa kuwa mojawapo ya shule za ada ya juu zaidi nchini Nigeria, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

  15. Mvulana wa Kenya aliyenaswa na mafuriko aokolewa kutumia helikopta

    ,
    Image caption: Mvua kubwa imeendelea kusababisha maafa nchini Kenya na kuacha uharibifu mkubwa

    Mvulana aliyekuwa peke yake mwenye umri wa miaka mitano ambaye alikuwa amezingirwa na mafuriko Jumanne aliokolewa na helikopta ya polisi huko Yatta, yapata kilomita 120 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

    Mvulana huyo "alikuwa ameachwa nyuma na babake wakati kina cha maji kilipoanza kupanda," polisi walisema.

    Shiriki la Kimataifa lisilo la serikali la Masuala ya Kibinadamu, ambalo lilinasa eneo alilokuwa mvulana huyo kwa kutumia ndege zisizo na rubani, liliwaarifu polisi, ambao kisha walituma helikopta ya uokoaji kutoka Nairobi.

    Jaribio la awali la kumwokoa mtoto huyo kwa boti lilishindikana kutokana na hali mbaya ya hewa, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema.

    "Mtoto huyo, ambaye alionekana kuwa na hofu baada ya kukwama kwa muda mrefu, aliokolewa salama na kupelekwa hospitali ya karibu kwa huduma," iliongeza.

    Mvua kubwa zimekuwa zikinyesha nchini Kenya na Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni na kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa.

    Nchini Kenya, mafuriko yamerekodiwa katika kaunti 23 kati ya 47 za nchi hiyo.

    Zaidi ya watu 188 wameokolewa tangu kuanza kwa mafuriko yanayoendelea, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema Jumanne.

    Iliongeza kuwa mafuriko hayo yamesababisha kaya 11,206 kupoteza makazi, kuzamisha ekari 27,716 na kuua zaidi ya mifugo 4,800.

  16. Umoja wa Ulaya wahimiza ufadhili kutolewa kwa shirika la UNRWA linalowapa misaada Wapalestina

    .

    EU imetoa wito kwa wafadhili wa kimataifa kurejesha ufadhili kwa mshirika mkubwa zaidi wa UN huko Gaza.

    Haya yanajiri baada ya uchunguzi kubaini kuwa Israel haikutoa ushahidi kwa madai yake kwamba maelfu ya wafanyakazi wa UNRWA walikuwa wanachama wa makundi ya kigaidi.

    Mataifa kadhaa yalisitisha ufadhili kwa shirika hilo baada ya madai kuwa baadhi ya wafanyakazi walishiriki katika mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel.

    Marekani inasema haitaanzisha tena msaada wake hadi UNRWA ifanye "mabadiliko ya kweli".

    UNRWA, ambayo inatoa huduma za afya, elimu na misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina, imeajiri watu 13,000 huko Gaza.

    Mkuu wa Umoja wa Ulaya wa masuala ya kibinadamu Janez Lenarcic alikaribisha ripoti ya Jumatatu kwa "kusisitiza idadi kubwa ya mifumo ya uzingatiaji ya shirika hilo pamoja na mapendekezo ya kuboreshwa zaidi".

    Alitoa wito kwa mataifa wafadhili kuunga mkono UNRWA, akiielezea kama "njia ya kuokoa wakimbizi wa Kipalestina".

    Soma zaidi:

    UNRWA ni nini na kwa nini ufadhili wake umesimamishwa?

  17. Kiboko 'dume' katika mbuga ya wanyama ya Japani apatikana kuwa jike baada ya miaka 7

    .

    Hifadhi ya wanyama nchini Japani imethibitisha kwamba kiboko aliyefikiriwa kwa miaka saba kuwa dume ni jike.

    Jaribio la DNA lilifanywa baada ya wafanyakazi wa hifadhi ya wanyama kugundua kuwa Gen-chan mwenye umri wa miaka 12 hakuonyesha tabia ya kiboko dume.

    Gen-chan aliwasili Osaka kutoka Mexico mwaka wa 2017, na hati zake zilisema alikuwa mwanaume.

    "Tutaendelea kufanya tuwezavyo kutoa mazingira mazuri kwa Gen-chan," mbuga ya wanyama ilisema.

    Hifadhi ya wanyama ya Osaka Tennoji ilithibitisha taarifa kuhusu jinsia ya Gen-chan iliyowekwa kwenye tovuti yao wiki iliyopita.

    Taarifa hiyo ilisema Gen-chan alifika kwa mara ya kwanza katika mbuga yao ya wanyama kutoka mbuga ya wanyama ya Africam Safari huko Mexico alipokuwa na umri wa miaka mitano, na kutangazwa kuwa dume.

    Taarifa hiyo iliongeza kwa sababu Gen-chan alikuwa bado ndama wakati huo, hawakutilia shaka hati hizo.

    Lakini walinzi wa mbuga za wanyama walitilia shaka jinsia ya Gen-chan kadiri alivyoendelea kukua na hawakuweza kutambua viungo vya uzazi vya kiume.

    Msemaji wa mbuga ya wanyama ya Osaka Tennoji aliiambia AFP siku ya Jumanne kwamba Gen-chan hakuwa na tabia za kiboko dume ikiwemo mahusiano kwa viboko jike, au kutawanya kinyesi huku akijisaidia haja kubwa kwa mkia ili kuashiria eneo.

    Kulingana na gazeti la Mainichi, makamu mkurugenzi wa mbuga hiyo ya wanyama Kiyoshi Yasufuku alisema: "Tunatambua umuhimu wa kuthibitisha jinsia, na tunataka kuhakikisha kwamba makosa kama hayo hayatatokea tena."

    Hifadhi ya wanyama ilithibitisha kuwa Gen-chan hatapewa jina jingine.

  18. Seneti ya Marekani yapitisha mswada unaoweza kupiga marufuku TikTok

    .

    Bunge la Seneti lameidhinisha mswada wa kihistoria wenye utata ambao unaweza kusababisha TikTok kupigwa marufuku nchini Marekani.

    Mswada huo unampa mmiliki wa TikTok Mchina, ByteDance, miezi tisa kuuza hisa zake au programu itazuiwa Marekani.

    Mswada huo sasa utakabidhiwa Rais wa Marekani Joe Biden ambaye, amesema atautia saini kuwa sheria punde utakapofika kwenye meza yake.

    Iwapo hilo litatokea, ByteDance italazimika kutafuta idhini kutoka kwa maafisa wa China ili kukamilisha mauzo ya kulazimishwa, ambayo Beijing imeapa kupinga.

    Hata hivyo, wachambuzi wanasema mchakato huo unaweza kuchukua miaka.

    TikTok haikujibu mara moja ombi la kuzungumza na BBC.

    Mtendaji mkuu wa TikTok, Shou Zi Chew, alisema mwezi uliopita kampuni itaendelea kufanya yote iwezayo ikiwa ni pamoja na kutumia "haki zake za kisheria" kulinda jukwaa.

    Soma zaidi:

    Ni kwanini Marekani ina wasiwasi kuhusu usalama wa TikTok ?

  19. Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi akamatwa kwa madai ya kupokea hongo

    .

    Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi akamatwa kwa tuhuma za kuchukua hongo, kwa mujibu wa chombo kikuu cha upelelezi nchini humo.

    Kamati ya Uchunguzi ilisema Jumanne kwamba Timur Ivanov anashikiliwa na uchunguzi unaendelea.

    Bw Ivanov aliyeteuliwa katika wizara ya ulinzi mwaka wa 2016, Bw Ivanov, 47, alihusika na miradi ya miundombinu ya kijeshi ya Urusi.

    Wanaharakati kwa muda mrefu wamekosoa viwango vya madai ya ufisadi nchini Urusi.

    Mnamo 2022, Wakfu wa Kupambana na Ufisadi, kundi lililoanzishwa na marehemu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, lilimshutumu Bw Ivanov kwa kushiriki katika "mipango ya ufisadi wakati wa ujenzi katika maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi".

    Hasa, ilisema alikuwa amefaidika kutokana na miradi ya ujenzi katika mji wa bandari wa Mariupol wa Ukraine, ambao sehemu kubwa yake iliharibiwa na mabomu ya Urusi katika miezi iliyofuata ya uvamizi wa Ukraine.

    Tangazo la Kamati ya Uchunguzi kuhusu kukamatwa kwa Bw Ivanov halikuonyesha jinsi naibu waziri huyo alivyojibu madai dhidi yake.

    Makosa kama hayo yanaadhibiwa kwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela.

    Awali, Bw Ivanov alikuwa naibu waziri mkuu wa eneo la Moscow, ambapo waziri wa ulinzi wa sasa Sergei Shoigu aliwahi kuwa gavana kwa muda mfupi, na anasemekana kusalia kuwa mshirika wa karibu wa Bw Shoigu.

    Kuzuiliwa huko kunaashiria hatua ya nadra dhidi ya miongoni mwa wasomi wa serikali ya Urusi, ambao wengi wao wanaaminika kutumia nyadhifa zao kujilimbikizia mali nyingi za kibinafsi.

    Naibu waziri wa ulinzi wa Urusi akamatwa kwa tuhuma za kuchukua hongo, kwa mujibu wa chombo kikuu cha upelelezi nchini humo.

    Kamati ya Uchunguzi ilisema Jumanne kwamba Timur Ivanov anashikiliwa na uchunguzi unaendelea.

    Bw Ivanov aliyeteuliwa katika wizara ya ulinzi mwaka wa 2016, Bw Ivanov, 47, alihusika na miradi ya miundombinu ya kijeshi ya Urusi.

    Wanaharakati kwa muda mrefu wamekosoa viwango vya madai ya ufisadi nchini Urusi.

    Mnamo 2022, Wakfu wa Kupambana na Ufisadi, kundi lililoanzishwa na marehemu kiongozi wa upinzani Alexei Navalny, lilimshutumu Bw Ivanov kwa kushiriki katika "mipango ya ufisadi wakati wa ujenzi katika maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi".

    Hasa, ilisema alikuwa amefaidika kutokana na miradi ya ujenzi katika mji wa bandari wa Mariupol wa Ukraine, ambao sehemu kubwa yake iliharibiwa na mabomu ya Urusi katika miezi iliyofuata ya uvamizi wa Ukraine.

    Tangazo la Kamati ya Uchunguzi kuhusu kukamatwa kwa Bw Ivanov halikuonyesha jinsi naibu waziri huyo alivyojibu madai dhidi yake.

    Makosa kama hayo yanaadhibiwa kwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka 15 jela.

    Awali, Bw Ivanov alikuwa naibu waziri mkuu wa eneo la Moscow, ambapo waziri wa ulinzi wa sasa Sergei Shoigu aliwahi kuwa gavana kwa muda mfupi, na anasemekana kusalia kuwa mshirika wa karibu wa Bw Shoigu.

    Kuzuiliwa huko kunaashiria hatua ya nadra dhidi ya miongoni mwa wasomi wa serikali ya Urusi, ambao wengi wao wanaaminika kutumia nyadhifa zao kujilimbikizia mali nyingi za kibinafsi.

    Pia unaweza kusoma:

    Sababu tatu zinazomfanya Putin kuwa na nguvu zaidi ya awali

  20. Bunge la seneti Marekani laidhinisha kifurushi cha msaada wa $95bn kwa Ukraine na Israel

    .

    Bunge la Seneti ya Marekani limeidhinisha kifurushi cha msaada kwa taifa la kigeni cha $95bn (£76bn) ambacho kinajumuisha msaada wa kijeshi kwa Ukraine, Israel na Taiwan.

    Rais Joe Biden anatarajiwa kutia saini sheria hiyo kuwa sheria siku ya Jumatano.

    Baraza la Seneti Jumanne jioni liliunga mkono hatua iliyopitishwa na Baraza la Wawakilishi la Marekani siku ya Jumamosi.

    Msaada huo unajumuisha $61bn wa kijeshi kwa Ukraine, ambayo Pentagon inasema inaweza kuanza kuwasilishwa kwa taifa hilo lenye vita "ndani ya siku kadhaa".

    Mswada huo ulipita kwa kura mbili za 79-18.

    Bw Biden alipongeza kupitishwa kwake katika taarifa mwishoni mwa Jumanne, na kuiita "sheria muhimu [ambayo] itafanya taifa letu na ulimwengu kuwa salama zaidi tunapounga mkono marafiki wetu wanaojilinda dhidi ya magaidi kama Hamas na wadhalimu kama [Rais wa Urusi Vladimir] Putin. ".

    Siku ya Jumanne, Kiongozi wa Wengi katika Seneti wa chama cha Democratic Chuck Schumer alisema Marekani imeonyesha kwamba haitawapa kisogo washirika wake.

    "Baada ya zaidi ya miezi sita ya juhudi kubwa na misukosuko mingi njiani, Marekani inatuma ujumbe kwa ulimwengu mzima: hatutakugeuzia kisogo," alisema kwenye Bunge la Seneti.

    Seneti ilikuwa imepitisha kifurushi sawa cha msaada mwezi Februari, lakini kundi la wahafidhina wanaopinga uungwaji mkono mpya wa Ukraine walikuwa wamezuia mswada huo kupigiwa kura katika Baraza la Wawakilishi.

    Soma zaidi:

    Msaada wa $61bn wa Marekani unamaanisha nini kwa Ukraine?