Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu

time_stated_uk

  1. Tanzania: Likizo ya uzazi kuzingatia muda wa uangalizi kwa watoto njiti

    Florian Kaijage

    BBC Dar es Salaam

    th

    Serikali ya Tanzania, imesema likizo ya uzazi kwa wazazi wanaojifungua watoto njiti (ambao hawajatimiza siku) inaanza pale mtoto atakapomaliza kipindi cha uangalizi maalumu kadiri madaktari watakavyothibitisha.

    Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango wakati wa kilele cha siku ya wafanyakazi duniani iliyofanyika kitaifa jijini Arusha, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Alikuwa akijibu maombi ya viongozi wakuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi TUCTA.

    "Iwapo mfanyakazi atajifungua mtoto au watoto njiti, kipindi cha uangalizi maalumu hakitahesabiwa kama likizo ya uzazi, likizo ya uzazi itaanza pale mtoto atakapomaliza kipindi cha uangalizi maalumu kadiri madaktari watakavyothibitisha, vilevile mfanyakazi husika ataruhusiwa kutoka kazini saa 7:30 mchana kila siku kwa muda wa miezi sita baada ya kumalizika kwa likizo ya uzazi ili kumpa fursa ya kwenda kunyonyesha". Amefafanua.

    Kuhusu kanuni ya kukokotoa mafao ya pensheni kwa wafanyakazi wakati wa kustafu, maarufu kama Kikokotoo, makamu huyo wa rais amesema serikali imepokea hoja ya wafanyakazi kutoridhishwa na kikokotoo na inaifanyia kazi kwa mujibu wa taratibu.

    Ameweka bayana kuwa baada ya kulipokea suala hilo litapelekwa kwa wataalamu wa takwimu bima (Actuarial Science) ili watoe ushauri kulingana na mahitaji ya wafanyakazi na hali ya uhimilivu wa mifuko ya pensheni.

    Kwa utaratibu wa sasa mstaafu wa umri wa miaka 55 kwa hiari au miaka 60 kwa mujibu wa sheria analipwa asilimia 33 ya mafao kwa mkupuo mmoja na fedha zinazobakia analipwa pensheni ya kila mwezi kwa kipindi cha miaka 12 na miezi sita, kwa makadirio ya chini.

  2. Tanzania na Kenya zasuluhisha mzozo wa mauzo ya kuku baada ya miaka mitatu

    h

    Tanzania na Kenya zimefanikiwa kutatua mgogoro wa muda mrefu wa mauzo ya kuku na bidhaa za kuku baina ya nchi hizo mbili, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilisema katika taarifa yake Jumanne.

    Taarifa hiyo ilisema mzozo huo ulitatuliwa wakati wa mkutano wa mashauriano wa siku mbili uliofanyika makao makuu ya kaskazini mwa Tanzania jijini Arusha uliomalizika Jumanne.

    Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo Rabson Wanjala, kutoka Kenya ambaye alimuwakilisha Balozi wa Kenya nchini Tanzania, alisema nchi zote mbili zimejitolea kukuza uhusiano wa kibiashara, na kuongeza kuwa ahadi zao zinasisitiza juu ya umuhimu wa juhudi za ushirikiano ili kuhakikisha biashara inaongezeka katika ukanda huo.

    Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania Benezeth Lutege Malinda amesema Tanzania inashughulikia kikamilifu vikwazo vya kibiashara kwa kuhakikisha mashirika yote yanayowezesha biashara yanajikita katika kutatua masuala hususani vikwazo visivyo vya ushuru vinavyokwamisha biashara.

    "Tunaendelea kujitolea kukabiliana na changamoto hizi na kukuza mazingira mazuri ya biashara kati ya Kenya na Tanzania," alisema.

    Mwaka 2018 Tanzania ilichoma vifaranga 5,000 vya kuku vilivyodaiwa kuingizwa nchini humo kupitia mpaka wa Kaskazini wa Namanga kutoka Kenya.

  3. Mafuriko Kenya: Watalii wakwama katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara baada ya mvua kubwa kunyesha

    .

    Watalii wanahamishwa kutoka mbuga maarufu ya Maasai Mara nchini Kenya baada ya mafuriko kukumba sehemu kubwa ya mbuga hiyo.

    Zaidi ya nyumba 10 za kulala wageni na kambi zimefurika baada ya Mto Talek ulio karibu kuvunja kingo zake siku ya Jumanne.

    Pia kuna hofu kuwa huenda baadhi ya wanyama walisombwa na mafuriko hayo.

    Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Kipkoech Lotiatia, aliambia BBC kuwa hifadhi hiyo iliharibiwa vibaya.

    "Maji yamepungua lakini baadhi ya nyumba za kulala wageni na kambi bado ziko chini ya maji," Bw Lotiatia alisema.

    Haijulikani ni watu wangapi wamenaswa katika hifadhi hiyo, lakini takriban 36 wameokolewa hadi sasa kwa ndege na wengine 25 na timu ya uokoaji ya mashua, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema.

    "Katika baadhi ya kambi, mahema yamesombwa na maji, na daraja la Mara, linalounganisha Mara Trianglena Greater Mara, limesombwa na maji," shirika hilola misaada liliongeza.

    TH

    Watalii wengi wa kigeni na wa ndani hutembelea hifadhi hiyo kujionea wanyamapori wake wakiwemo simba, chui na duma.

    Bw Lotiatia awali aliwaambia wanahabari kwamba timu za uokoaji zilikuwa zikitumia helikopta mbili za dharura kuwahamisha watalii na wafanyikazi.

    Uongozi wa Masai Mara haukujibu mara moja ombi la BBC la kutaka maoni yao.

    Mto Talek ulipasua kingo zake Jumanne alasiri kufuatia mvua kubwa iliyonyesha juu ya mto huo.

    Hali imekuwa mbaya zaidi kutokana na maji yanayotiririka kutoka mto Mara, karibu na mpaka wa Serengeti na Tanzania, kufuatia mvua nyingi katika eneo hilo.

    "Baada ya siku kadhaa za mvua zinazoendelea kunyesha, mito yetu imejaa maji, na kuathiri kambi na maeneo kadhaa katika Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara," serikali ya kaunti ya Narok ilisema kupitia taarifa.

    Barabara na madaraja pia yamezamishwa na maji, na kuathiri jamii zinazoishi huko.

    Pia unaweza kusoma:

    Barabara 3 zilizofunikwa na mafuriko mjini Nairobi zafungwa

  4. DRC: Waasi wa M 23 wadai kuuteka mji wa kuchimba madini wa Rubaya ulioko Masisi

    .

    Waasi wa M23 wanasema wameuteka mji wa uchimbaji madini katika eneo la Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini, baada ya mapigano makali na jeshi Jumanne na Jumatano asubuhi.

    Rubaya ni mojawapo ya maeneo muhimu ya uchimbaji madini ya coltan duniani, madini haya adimu ni muhimu katika uzalishaji wa simu za mkononi, kompyuta, na magari ya umeme.

    "Tumechukua eneo hilo [Rubaya] si kwa sababu ya utajiri wake, lakini kumfukuza adui yetu ambaye analenga kufanya mauaji ya kimbari. Lengo letu si migodi bali kuokoa maisha ya watu”, Willy Ngoma msemaji wa jeshi la waasi aliambia BBC.

    Hata hivyo, jeshi la Kongo halikuzungumzia madai ya waasi hao.

    Rais wa jumuiya ya kiraia ya Masisi, Voltaire Sadiki, aliiambia BBC kwamba waasi wameteka mji wa Rubaya, na "kuamuru raia wenye bunduki kuwakabidhi na kuendelea na maisha yao", alisema.

    Siku ya Jumanne wakati mapigano yalipokuwa yakiendelea huko Rubaya, Rais Felix Tshisekedi wa DR Congo alikuwa Paris ambako alikariri kwa nguvu kwamba jeshi la Rwanda liko nyuma ya M23, na Rais wa Ufaransa Macron aliitaka Rwanda kuondoa wanajeshi wake kutoka DR Congo.

    Rwanda inakanusha kuunga mkono M23 na Rais Paul Kagame amemshtumu Bw Tshisekedi kwa kushindwa kushughulikia masuala ya wakimbizi wa Kongo katika eneo hilo na M23 kama matatizo ya Kongo.

    Rubaya, mwendo wa saa mbili kwa gari kuelekea magharibi kutoka Goma, iko katikati ya uchimbaji haramu wa madini ya coltan, madai ya ajira ya watoto, na biashara haramu ya makundi mbalimbali yenye silaha.

    Licha ya kuwa na maliasili nyingi, wakazi wa Rubaya, na DR Congo kwa ujumla, wanaishi katika umaskini, ripoti za wataalamu mbalimbali zinasema.

    Soma zaidi:

    Mambo matano muhimu kuhusu mzozo wa Mashariki mwa DR Congo

  5. Barabara kuu ya China yaporomoka na kusababisha vifo vya watu 24

    .

    Watu 24 wamefariki dunia baada ya sehemu ya barabara kuu ya mlimani kuporomoka katika jimbo la Guangdong nchini China, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa.

    Wengine 30 walipelekwa hospitalini baada ya kipande cha 17.9m (futi 58) cha barabara ya mwendokasi ya Meilong kubomoka saa 02:10 saa za eneo siku ya Jumatano.

    Mamlaka bado haijaeleza sababu ya tukio hilo.

    Picha kwenye vyombo vya habari vya serikali zilionyesha uharibifu mkubwa kwenye mlima wenye misitu chini ya barabara kuu.

    Watu 30 hospitalini "hawako hatarini kwa sasa", vyombo vya habari vya serikali vinaripoti. Serikali ya mkoa imetuma wahudumu wa dharura 500 kwenye eneo la tukio.

    Vyombo vya habari vya serikali hapo awali viliripoti kuwa watu 19 walikufa lakini viongozi wa eneo hilo baadaye walisema watu 24 waliuawa, na idadi ya waliojeruhiwa bado ni 30.

    Picha ambazo zilionekana kuchukuliwa muda mfupi baada ya kuporomoka kwa barabara zilionyesha miali ya moto na moshi mweusi ukifuka kutoka chini ya barabara kuu.

    Jumla ya magari 20 yalianguka katika sehemu iliyoporomoka ya barabara, mamlaka ilisema.

    Video nyingine iliyoonyeshwa na vyombo vya habari vya serikali ilionyesha rundo la magari yaliyokuwa yameungua yakiwa yamefunikwa na udongo.

  6. Rais William Ruto awataka madaktari kusitisha mgomo wao na kurejea kazini

    .

    Rais William Ruto amewataka madaktari kusitisha mgomo wao huku serikali ikijitahidi kutimiza matakwa yao yote katika wakati ambao haujabainishwa siku zijazo.

    Katika hotuba yake ya Siku ya Wafanyakazi kwenye bustani ya Uhuru Gardens jijini Nairobi, Ruto aliwaambia madaktari kuwa serikali haiwezi kutimiza matakwa yao yote kikamilifu kutokana na matatizo ya kifedha.

    “Tumewasilisha kile ambacho serikali iko tayari kufanya; 17 kati ya madai 19, mengine hayawezekani kwa sababu ya matatizo ya kifedha,” alisema.

    “Nawaomba madaktari warudi kazini, tutasuluhisha, turekebishe uchumi na kila mtu atapata haki yake siku za usoni. Lazima tuwe waaminifu kwa kila mmoja hata kama inauma, hakuna haja ya kusema uwongo."

    Tangu Machi 14, madaktari wamekuwa wakigoma na kupinga hatua ya serikali kushindwa kuwapa kazi madaktari tarajali na kutekeleza Mkataba wa Majadiliano ya Pamoja (CBA) wa 2017 kuhusu masharti ya kazi ya madaktari.

    Huku mgomo huo ukiingia siku ya 49 hii leo, Rais Ruto, aliwataka madaktari kuzingatia athari za mgomo wao katika huduma za afya nchini na kurejelea majukumu yao kwa kile alichotaja kuwa ustawi wa umma.

  7. Rais Ruto aagiza kuongezwa kwa kima cha chini cha mshahara katika hotuba ya siku ya wafanyakazi

    .

    Rais William Ruto nchini Kenya ametoa wito wa kuongezwa kwa kima cha chini cha mshahara ili kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa ipasavyo kutokana na mchango wao katika uchumi wa taifa.

    Katika hotuba yake wakati wa sherehe za 59 za Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi, Rais Ruto alimwagiza Waziri wa Wafanyakazi Florence Bore kuongoza mchakato wa kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa angalau asilimia sita.

    “Ninaziomba mamlaka husika, haswa Wizara ya Wafanyakazi, kuitisha kikao na kamati inayofaa kujadili na kutekeleza nyongeza ya mishahara ya angalau asilimia 6,” Rais Ruto alisema wakati wa hotuba yake.

    "Utaniambia jinsi hesabu itafanywa na jinsi tutakavyosonga mbele."

    Nyongeza ya kima cha chini cha mshahara inahusisha mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na viwango vya mfumuko wa bei, gharama ya maisha, na viashirio vya ukuaji wa uchumi.

  8. Mama wa mateka Muisraeli aomba makubaliano ya kusitisha mapigano

    ,

    Mama wa mwanamume Muisraeli mwenye asili ya Marekani anayezuiliwa huko Gaza ameiambia BBC kwamba Israel na Hamas lazima wakubaliane haraka mpango mpya wa kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka.

    Mtoto wa Rachel Goldberg-Polin Hersh, ambaye alitimiza umri wa miaka 23 siku nne kabla ya kutekwa nyara kutoka kwa tamasha la Nova mnamo 7 Oktoba, alionekana akiwa kifungoni katika video mpya iliyotolewa wiki iliyopita.

    Alieleza jinsi alivyohisi alipoitazama kwa mara ya kwanza.

    "Mara tu niliposikia sauti yake nilianza kulia, kwa sababu sijasikia sauti yake kwa nusu mwaka.

    "Kumwona akisogea, na kuona kwamba ameathirika kimatibabu, na dhaifu. Baba yake Jon na mimi tulikuwa tunalia tu, na nilikuwa nimeushika moyo wangu."

    "Sijui hata nilichokuwa nikisema. Nilikuwa nikipiga kelele tu na kulia, na Jon alikuwa analia".

    Hersh Goldberg-Polin alikuwa kwenye tamasha la muziki la Nova katika eneo la msitu karibu na Ukanda wa Gaza wakati watu wenye silaha wakiongozwa na Hamas walipovamia uzio wa mpaka wa Israel, na kuua takriban watu 1,200 na kuwakamata mateka 253, kulingana na hesabu za Israel.

    Zaidi ya 360 kati ya waliouawa walikuwa wakihudhuria tamasha hilo.

    Hersh alikimbia kilomita kadhaa na kutafuta hifadhi katika makazi kando ya barabara na wengine kadhaa wakati wa shambulio hilo, lakini watu wenye silaha walikusanyika nje na kuanza kurusha maguruneti.

  9. Barabara 3 zilizofunikwa na mafuriko mjini Nairobi zafungwa

    .
    Image caption: Mafuriko

    Takriban barabara tatu ndani ya jiji la Nairobi zimefungwa kwa kiasi na magari kuelekezwa kwingine baada ya mvua kubwa iliyonyesha Jumanne usiku kusababisha mafuriko.

    Mamlaka ya Barabara za Mijini (KURA) ilitangaza kuwa Barabara ya Enterprise, Eastern Bypass na Thika Bypass zilikuwa zimefungwa kwa madereva, na polisi walikuwa wakisaidia kuelekeza trafiki ipasavyo.

    "Kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana kote nchini, barabara zifuatazo katika Kaunti za Nairobi na Kiambu zimeathirika pakubwa na kusababisha kufungwa kwa sehemu: Barabara ya Enterprise, Eastern bypass na Thika bypass.

  10. Kendrick Lamar azidisha ugomvi dhidi ya Drake kwenye wimbo wake mpya Euphoria

    Msanii wa Marekani Kendrick Lamar ametoa wimbo unaomshambulia nyota mwenzake wa rap Drake, na kuzidisha ugomvi wao wa muda mrefu.

    Wimbo huo unaoitwa Euphoria, ni jibu la dhihaka za wiki kadhaa za Drake, ambaye amemshambulia kwa maneno Lamar kwenye mfululizo wa nyimbo zake.

    Zaidi ya dakika sita, Lamar anamwita Drake "mdanganyifu na mwongo wa kawaida", na anakosoa ujuzi.

    Pia anamshutumu nyota huyo wa Canada kwa kujiuza, akisema anafanya muziki tu ili "kutuliza" mashabiki.

    Na anawaacha wasikilizaji na majibu kuhusu bila hisia zake dhidi ya Drake."Hii haijawa ukosoaji wa vita, sio juu ya ujanja, sio juu ya nani mkuu," anarap.

    "Siku zote imekuwa juu ya upendo na chuki, sasa wacha niseme mimi ndiye mwenye chuki mkubwa.""Nachukia jinsi unavyotembea, jinsi unavyozungumza, nachukia jinsi unavyovaa.

    "Ugomvi wa rappers hao ulianza 2013, wakati Lamar alipokuwa mgeni katika sanaa ya muziki huo.

    Wakati wa onyesho katika Tuzo za BET, alijigamba kwamba ujuzi wake "ulimrudisha rapa mmoja katika nguo zake za kulalia.

    Mstari huo ulitafsiriwa kuwa unamrejelea Drake, ambaye mchanganyiko wake wa kufoka wa R&B ulikuwa umebadilisha sauti ya hip-hop.

  11. Mtafuta hifadhi wa kwanza aliyefeli apelekwa Rwanda chini ya mpango wa hiari

    .
    Image caption: Mtafuta hifadhi huyo huenda akasafiri kwa ndege hadi Kigali, mji mkuu wa Rwanda

    Uingereza imemrejesha mtafuta hifadhi kwa mara ya kwanza nchini Rwanda chini ya mpango wa kuwaondoa kwa hiari, inafahamika.

    Chini ya mpango huo, uliotangazwa mwezi uliopita, wahamiaji ambao madai yao yamekataliwa wanapewa hadi pauni 3,000 kuhamia nchi hiyo ya Afrika mashariki.

    Ni tofauti na mpango wa kurejeshwa kwa lazima ambao serikali ilitangaza miaka miwili iliyopita.

    Mpango huo, ambao umekumbwa na ucheleweshaji, unatarajiwa kuanza katikati ya Julai.

    The Sun, ambalo liliripoti kisa hicho kwa mara ya kwanza, lilisema mtu huyo ambaye hakutajwa jina alisafirishwa kutoka Uingereza siku ya Jumatatu kwa ndege ya kibiashara.

    Maafisa hawangetolewa kwa maelezo yoyote, zaidi ya kusema mtafuta hifadhi alikuwa amekamilisha haki zote za kuwa nchini Uingereza.

    Serikali ya Rwanda ilithibitisha kuwa mtafuta hifadhi aliyefeli aliwasili Jumanne kwa ndege kutoka London.

    Labour ilisema hatua hiyo ilionyesha mawaziri "walikuwa na tamaa" ya kupata ndege kuelekea Rwanda kabla ya uchaguzi wa mitaa wa Alhamisi nchini Uingereza.

  12. Mamilioni wanatumia WhatsApp kwa siri licha ya kupigwa marufuku

    .

    Mamilioni" ya watu wanatumia mbinu za kiufundi kufikia WhatsApp kwa siri katika nchi ambazo imepigwa marufuku, bosi wa mtandao huo amesema.

    "Utashangaa ni watu wangapi wamegundua," Will Cathcart aliiambia BBC News.

    Kama programu nyingi za Magharibi, WhatsApp imepigwa marufuku nchini Iran, Korea Kaskazini na Syria.

    Na mwezi uliopita, China ilijiunga na orodha ya wale wanaopiga marufuku watumiaji kujiunga na mtandao huo ulio salama.

    Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Qatar, Misri, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu, huweka vikwazo kwa vipengele kama vile simu za sauti.

    Lakini WhatsApp inaweza kuona ni wapi watumiaji wake wapo, kutokana na nambari zao za simu zilizosajiliwa."

    Tuna ripoti nyingi za watu wanaotumia WhatsApp na tunachoweza kufanya ni kuangalia baadhi ya nchi ambazo tunazuiwa na bado tunaona makumi ya mamilioni ya watu wakitumia WhatsApp," Bw Cathcart aliambia BBC News.'

    Acha kitu' China iliiamuru Apple kuwazuia watumiaji wa iPhone wa China kupakua WhatsApp kutoka kwa AppStore mwezi Aprili, hatua ambayo Bw Cathcart anaiita "ya kushangaza" - ingawa nchi hiyo haikuwa soko kuu la programu hiyo."

    Hilo ni chaguo Apple imefanya," alisema."Hakuna njia mbadala."

    Namaanisha, hiyo ni hali ambayo wamejiweka katika nafasi ya kuweza kukomesha kitu"Watumiaji wa Android, hata hivyo, bado wanaweza kupakua WhatsApp bila kupitia maduka rasmi.

    Lakini kwingineko Bw Cathcart alisema kuongezeka kwa mitandao ya kibinafsi (VPNs) na huduma ya wakala ya WhatsApp, iliyozinduliwa Juni mwaka jana, kumesaidia kufanya WhatsApp ipatikane.

  13. Uingereza yawawekea vikwazo wanasiasa wa Uganda kutokana na madai ya ufisadi

    .
    Image caption: Bunge la Uganda

    Uingereza imewawekea vikwazo wabunge watatu wa Uganda siku ya Jumanne, ikiwashutumu kwa ufisadi.

    Watatu hao ni spika wa bunge Anita Miongoni pamoja na mawaziri wawili wa zamani wa eneo la kaskazini mashariki la Karamoja, Mary Kitutu na Agnes Nandutu.

    Kitutu na Nandutu wanashutumiwa kwa kuiba maelfu ya mabati kutoka kwa mradi wa ujenzi wa nyumba unaofadhiliwa na serikali unaolenga kusaidia jamii zilizo hatarini katika eneo lililotengwa la Karamoja, na kuzielekeza kwa wanasiasa na familia zao.

    Spika wa bunge, Kati, anadaiwa kufaidika na mpango huo, Uingereza ilisema. "Uingereza inatuma ujumbe wa wazi kwa wale wanaofikiri kunufaika kwa gharama ya wengine ni jambo linalokubalika.

    Ufisadi una madhara na utawajibika," naibu waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Andrew Mitchell alisema katika taarifa yake.

    "Hatua za watu hawa, katika kuchukua misaada kutoka kwa wale wanaohitaji zaidi, ni rushwa katika hali mbaya zaidi na haina nafasi katika jamii."

  14. Marekani kuainisha upya bangi katika mabadiliko ya kihistoria

    .
    Image caption: Wataalamu wanasema kuainishwa upya kutapunguza soko la bangi ambalo bado linaendelea kustawi nchini Marekani.

    Mamlaka ya utekelezaji wa Dawa za Kulevya nchini Marekani inapanga kuainisha upya bangi kama dawa isiyo hatari sana, ikiwa ni mabadiliko ya kihistoria katika sera ya dawa za Marekani.

    Katika ngazi ya kijimbo, bangi huainishwa kama dawa ya "Ratiba I", orodha ambayo imeshirikishwa na heroin, ecstasy na LSD.

    Badala yake, itajumuishwa miongoni mwa dawa za "Ratiba III", ambazo zina uwezekano mdogo wa kutumiwa vibaya.

    Hatua hiyo itakuwa mabadiliko muhimu zaidi ya sera ya dawa za Marekani katika zaidi ya miaka 50.

    Idara ya sheria ilituma pendekezo lake kwa Ofisi ya White House kuhusu Usimamizi na Bajeti (OMB) mnamo Jumanne, idara hiyo ilithibitisha katika taarifa.

    Pindi pendekezo hilo litakapochapishwa katika sajili ya ngazi ya kijimbo ya serikali kuu ya Marekani, kipindi cha maoni ya umma kitaanza, na kisha kitapitiwa na jaji wa utawala kabla ya mabadiliko hayo kurasimishwa na kuchapishwa.

    Wakati bangi, inasalia kuwa haramu katika ngazi ya serikali kuu, majimbo 38 yameihalalisha kwa madhumuni ya matibabu, na 24 yameihalalisha kwa matumizi ya burudani.

    Tangazo hilo lilituma bei za hisa za kampuni za tasnia ya bangi za Marekani kupanda kwa kati ya 15% na 67%. Makampuni ya Canada pia yalifurahia ongezeko kubwa.

    Je! ni dawa gani za ratiba I na III?

    Tangu 1971, bangi imekuwa dawa ya ratiba I, ikimaanisha kwamba - kwa maoni ya serikali ya shirikisho - "haina matumizi ya matibabu yanayokubalika kwa sasa na uwezekano mkubwa wa kuathiri.

    "Ratiba III, kwa upande mwingine, zinafafanuliwa na DEA kama dawa "zenye athari ndogo za kimwili na kisaikolojia".

    Bangi: Zijue nchi tano zilizoruhusu uzalishaji wa bangi Afrika

    Utafiti: 'Matumizi ya bangi yanadumaza akili' - Je inaathiri akili kivipi?

    Bangi za kutengeneza maabara zina madhara gani mwilini?

  15. Magoli 2 ya Vinicius yaisaidia Real Madrid kutoka sare na Bayern Munich

    .
    Image caption: Vinicius Junior amefunga mabao matano katika mechi nane zilizopita akiwa na Real Madrid

    Vinicius Junior alifunga mabao mawili na kuisaidia Real Madrid kutoka sare katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich.

    Mbrazil huyo alichukua fursa ya makosa mawili ya beki wa Bayern Kim Min-jae - kumpita kwa kasi na kuachia shuti lililompita kipa Manuel Neuer, kabla ya raia huyo wa Korea Kusini kumfanyia madhambi Rodrygo kwenye eneo la hatari na Vinicius kufunga penalti hiyo.

    Nahodha wa Uingereza, Harry Kane alikuwa amefunga penalti ya aina yake, akimshinda mlinda lango Andriy Lunin mapema kipindi cha pili baada ya Jamal Musiala kuangushwa na Lucas Vazquez kwenye eneo la hatari.

    Dakika chache kabla, mchezaji mwenza Leroy Sane alikuwa amepiga shuti kali ndani ya lango la Bayern, na kusawazisha bao la kwanza la Vinicius.

    Udhibiti wa mchezo ulibadilika baada ya Bayern kushindwa kuchukua fursa kabla ya Vinicius kupokea pasi safi kutoka kwa kiungo Toni Kroos .

    Wakiwa wameshambulia mara sita na kumiliki mpira kwa zaidi ya 60% katika dakika 20 za kwanza - nafasi nzuri zaidi za Bayern ziliwaangukia Sane na Kane – lakini Bayern walijikuta nyuma.

    Lakini kipindi kibaya cha dakika nne katika kipindi cha pili kiligeuza mchezo na wababe hao wa Ujerumani kurejesha kasi yao.

    Waliiweka Real chini ya shinikizo na labda walikuwa na bahati mbaya kutokuwa kifua mbele .

    Kosa la Kim - kuvuta jezi ya Rodrygo bila sababu katika dakika ya 83 - liliwaruhusu Real kurejea mchezoni na sasa wanarudi katika uwanja wa nyumbani wa Bernabeu katika mechi ya mkondo wa pili Jumatano ijayo.

    .
    Image caption: Sane na Harry Kane
  16. Kusini mwa Lebanon: BBC yakuta uharibifu wa mashambulizi ya anga katika miji isiyo na watu

    .

    Mvutano unaoendelea na mashambulizi ya kuvuka mpaka ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya raia 70 nchini Lebanon yamegeuza maeneo ya kusini kuwa mahame.

    Wakazi wametoroka, na kuacha nyumba zao zikiwa hatarini kuharibiwa. BBC ilipiga doria na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ili kuona nini kimetokea.

    Bonde kubwa lililokuwa na godoro lililofukiwa chini ya vumbi na mawe ndilo lililobaki jengo lililosimama mahali hapa siku chache zilizopita.

    "Tunaita 'dimbwi'," afisa wa jeshi la Lebanoni huko Yarine - mji wa mpakani ulioko mstari wa mbele wa moja ya maeneo hatari zaidi ya vita katika eneo hilo.

    Yarine iko kilomita 1 tu (maili 0.6) kutoka Mstari wa bluu ulioanzishwa na Umoja wa Mataifa - mpaka wenye utata na usio rasmi kati ya Israel na Lebanon.

    Katika kila mji karibu na mstari huo, kuna vituko sawa: majengo yaliyopangwa au kutoweka kwenye mashimo; karibu nayo, majengo ambayo yameharibiwa.

    Katika Alma el Shaab, takriban kilomita 4 magharibi mwa Yarine, kuna mabaki ya kile kinachoonekana kuwa jumba la kifahari lililokuwa na magari yaliyoegeshwa - lililoharibiwa, mbali na uzio unaozunguka rundo la vifusi.

    Madirisha ya nyumba zilizokuwa karibu yote yamevunjwa kutokana na nguvu ya milipuko hiyo.

    Kwa nini Israel inafanya mashambulizi ya fosforasi nyeupe huko Gaza na Lebanon?

    Hezbollah ni nini?

    Lebanon: Mstari wa Buluu katikati ya mapambano ya Hezbollah na Israel

  17. Emmanuel Macron aitaka Rwanda 'kusitisha msaada' kwa waasi wa M23

    .
    Image caption: Emmanuel Macron na Felix Tshisekedi

    Rais wa Ufaransa ameitaka Rwanda "kusitisha kuwaunga mkono " waasi wa M23 wanaofanya uharibifu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi, ambaye yuko ziarani mjini Paris, Bw Macron alisema: "Rwanda lazima isitishe uungaji mkono wake kwa M23 na kuondoa majeshi yake katika eneo la Kongo."

    M23 ilianza harakati zake mwaka 2012 ili kulinda idadi ya Watutsi mashariki mwa DR Congo, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia mateso na ubaguzi.

    Umoja wa Mataifa, EU na Marekani zimesema kuwa Rwanda, ambayo pia inaongozwa na Watutsi, inawaunga mkono M23, Jambo ambalo Serikali mjini Kigali imekanusha mara kwa mara.

    Machi mwaka jana, alipotakiwa kulaani kitendo cha Rwanda kuunga mkono waasi, Bw Macron alisema "amekuwa wazi sana kuhusu kuilani M23 na wale wanaoiunga mkono".

    Mambo matano muhimu kuhusu mzozo wa Mashariki mwa DR Congo

    Je, Félix Tshisekedi ataleta vita au amani kwa DR Congo na Rwanda?

    Kanisa katoliki lina nguvu gani katika siasa za DR Congo?

  18. Natumai hujambo