Saeb Erekat: Afisa wa juu wa Palestina alazwa hospitalini Israel

Saeb Erekat alipandikizwa mbavu miaka mitatu iliyopita, hali iliyomfanya kupata ugumu kupona Covid-19

Chanzo cha picha, Reuters

Afisa wa juu wa Palestina Saed Erekat yuko katika hali mbaya baada ya kuugua ugonjwa wa Covid-19 na amewekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua, hospitali inayomtibu nchini Israel imeeleza.

Siku ya Jumapili Erakat mwenye miaka 65 alikimbizwa katika kituo cha afya cha Hadassah mjini Yerusalemu kutoka nyumbani kwake Yeriko, katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

Hali yake kuwa ni ''mgonjwa lakini si mahututi'', na kuwa alipatiwa oksijeni.

Jumatatu asubuhi, hospitali ilisema hali ya Bw. Ereket ilikuwa ilibadilika na kuwa '' mbaya''

"Kwa sababu ya shida ya kupumua, aliwekwa kwenye mashine ya msaada wa kupumua na kuwekwa dawa ya usingizi," iliongeza taarifa hiyo.

Hospitali imesema kumtibu Bw. Erekat ilikuwa ''changamoto kubwa'' kwa kuwa aliwahi kufanyiwa upasuaji kupandikiza mbavu miaka mitatu iliyopita, na alikuwa na ''mfumo wa kinga ulio dhaifu na maambukizi ya vijidudu mbali na kuwa na virusi vya corona''.

Bwana Erekat ni Katibu Mkuu wa chama cha Palestine Liberation Organisation (PLO), akihudumu kama mshauri wa Rais Mahmoud Abbas na amekuwa mpatanishi mkuu wa mazungumzo ya amani ya Palestina na Israel kwa kipindi cha miongo miwili na nusu.

Alitangaza kuwa na maambukizi ya virusi vya corona tarehe 9 mwezi Oktoba.

Aliandika katika ukurasa wa twitter kuwa '' na dalili kali kutokana na kushuka kwa kinga kutokana na kupandikizwa mbavu''. Lakini aliongeza kuwa ''hali imedhibitiwa, asante Mungu''.

Siku ya jumapili , PLO ilisema kwamba amehamishwa hadi katika kituo cha matibabu cha Hadassah kutokana na hali mbaya anayokabiliwa nayo katika mfumo huo wa kupumua.

Mashahidi waliambia Reuters kwamba walimuona Erakat akiwa amebebwa akiingizwa katika ambyulansi ya Israel .

Ndugu yake Saber aliambia AFP kwamba hali yake nzuri. Mkurugenzi wa kituo cha Afya cha Hadassah , Profesa Zeev Rothstein , alisema siku ya Jumapili: Bwana Erakat anapokea uangalizi wa hali ya juu kama wanavyofanyiwa wagonjwa wote wa corona katika hospitali ya Hadassah, na kwamba wafanya kazi wa hospitali hiyo watafanya kila kitu kuhakikisha kuwa anapona.

" Hadassah, tunawatibu wagonjwa wote kana kwamba ni mgonjwa wa pekee''

Tangu mwanzo wa mlipuko wa corona zaidi ya wagonjwa 58,500 walithibitishwa kuwa na maradhi hayo na takriban wagonjwa 478 wamethibitiswa kufariki katika eneo la West Bak, ikiwemo mashariki mwa Jerusalem, na ukanda wa Gaza kulingana na shirika la Afya Duniani WHO.PICHA>>>>

Siku ya Jumapili , serikali ya Israel ililegeza masharti ya kutotoka nje ambayo yamekuwa yakihudumu kwa mwezi mmoja, baada ya kushuka kwa idadi ya maambukizi mapya.

Watu nchini Israel sasa wanaruhusiwa kwenda zaidi ya kilomita moja kutoka nyumbani kwao kwa masuala yasio muhimu , huku shule za chekechea zikitarajiwa kufunguliwa na mikahawa ikiruhusiwa kuuza chakula cha kupeleka nyumbani.

Fukwe za bahari, mbuga za wanyama pori pia zimefunguliwa wageni.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alisema siku ya Alhamisi kwamba masharti hayo yamefaulu lakini kulegezwa kwa masharti hayo ya kutotoka nje lazime kufanyike polepole.