Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Asha Juma na Dinah Gahamanyi

time_stated_uk

  1. Tuna imani na Samia Hassan Suluhu

    Video content

    Video caption: Tuna imani na Samia Hassan Suluhu

    Jaji mkuu mstaafu mzee Joseph Sinde Warioba ameiambia BBC ana imani na Mama Samia na hana shaka lolote juu ya namna mabadiliko ya utawala yatakavyofanyika kwani katiba ya Tanzania iko wazi na itafuatwa. Zuhura Yunus alimtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kuzungumza naye na swali la kwanza alimuuliza ameupokeaje msiba wa rais Magufuli.

  2. Muhammadu Buhari: Rais Magufuli atakumbukwa daima

    Buhari

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amejiunga na serikali na watu wa Tanzania katika maombolezo ya kifo cha Rais John Pombe Magufuli, aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

    Kiongozi huyo wa Nigeria amesema Magafuli “urithi wa uzalendo na kujitolea kwa ajili ya Uafrika itaendelea kukumbukwa kote barani .”

    Rais Buhari anasema Hayati rais wa Tanzania “alitumia muda wake mwingi zaidi wa maisha yake kulitumikia taifa na ubinadamu .”

    Taarifa kutoka katika ofisi ya rais ya Nigeria inasema Bw Buhari “anaamini ujasiri na upendo kwa nchi wa Hayati rais wa Tanzania vilihamasisha mageuzi mbalimbali ambayo vizazi vitaendelea kuyakumbuka ”

    Kwa mujibu wa Bw Buhari, John Magufuli atakumbukwa kwa mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na “ kupunguza ukubwa na gharama za utawala, kusisitiza kuhusu bajeti inayowalenga watu, yenye vipaumbele vya wazi kuhusu elimu na afya, na kupambana wakati wote na ubadhirifu katika matumizi ya umma.”

    Kiongozi huyo wa Nigeria ametoa salamu za rambi rambi kwa familia ya marehemu “ kiongozi mwenye maono wa Tanzania”, marafiki na washirika wake, pamoja na wananchi wote wa Tanzania.

    Rais Buhari amesema anaimbea roho ya marehemu ipumzike kwa Amani.

  3. Spika wa bunge aagiza kamati za bunge mikoani kurejea Dodoma

    Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai

    Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ameagiza Kamati zote za Bunge zilizokuwa katika ziara za ukaguzi wa miradi ya maendeleo mikoani kurejea Dodoma mara moja.

    Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutangazwa kwa kifo cha Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam.

    Mheshimiwa Job Ndugai, amesema kuwa amepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Magufuli.

    ‘’Tumempoteza Rais wetu kipenzi aliyejitoa kuwatumikia Watanzania wote kwa uadilifu, umahiri, bidii na moyo wa uzalendo wa hali ya juu. Kwa niaba ya Bunge natoa pole kwa Janeth Magufuli na familia ya marehemu, makamu wa rais pamoja na Watanzania wote kufuatia msiba huu mzito wa kitaifa.’’

  4. Wasanii wa muziki Tanzania wamlilia Magufuli

    Diamond Platnumz

    Baadhi ya Wasanii wa muziki nchini Tanzania wamekuwa wakielezea hisia zao za huzuni kuhusu kifo cha rais wa nchi hiyo Dkt John Pombe Magufuli ambaye amefariki dunia jana kutokana na maradhi ya moyo.

    Wasanii hao ambao ni pamoja na Diamond Platnumz, RayVanny, Jux, Marioo, Malkia Karen, Zuchu, Khadija Kopa, Christina Shusho, wamejikusanya na kuingia studio kuandaa wimbo wa pamoja wa kumuaga Rais Dkt. John Pombe Magufuli

    Baadhi ya wasanii hao walielezea hisia zao kuhusu kifo cha Bw Magufuli kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram:

    View more on instagram
    View more on instagram
    View more on instagram
    View more on instagram
  5. 'Nilikuwa na Magufuli dawati moja darasani'

    Watanzania wameamkia taarifa kuwa rais wao amefariki dunia.
    Image caption: Watanzania wameamkia taarifa kuwa rais wao amefariki dunia.

    Mwalimu aliyestaafu Kasara Mnaku amemkumbuka aliyekuwa mwanafunzi mwenzake – Hayati mzee John Magufuli, ambaye amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

    Katika mahojiano na mwandishi wa BBC Aboubakar Famau, Bwana Mnaku amesema:

    ''Tuliishi katika kijiji kimoja. Tulikuwa darasa moja na tukaketi dawati moja. Katika maisha yake ya awali, hadi alipokuwa rais, tulikuwa pamoja na alikuwa rafiki yangu. Kila alipohitaji ushauri angenipigia simu na tungezungumza''.

    Bw Mnaku Aliongeza: ''Tulipokuwa watoto tulikuwa na uhusiano wa karibu kweli na kusaidiana na tulipenda mno kusoma.Hili lilitusaidia kufika tulipofika, Nikawa mwalimu na yeye pia akawa mwalimu lakini hatimaye akaamua kuacha taaluma hiyo na kuhudumia nchi."

    Mwanafunzi mwingine aliyesoma naye, Elias Kwaswahili, amesema:

    ''Tuliishi kijiji kimoja cha Rubambangwe na sote tulisomea katika shule ya msingi ya Chato. Na baadaye tukakutana katika shule ya sekondari ya Lake Mwanza''.

    Elias Kwaswahili: ''Alikuwa mwanafunzi mzuri sana darasani hasa katika sayansi. Tuliona masomo ya sayansi yakiwa magumu hasa hisabati. Lakini alikuwa mzuri sana katika hesabu na hili ndili lililo msukuma kufanya masomo ya sayanasi. Hivyo ndivyo nilivyo mfahamu".

    Bwana Magufuli alikuwa na shahada ya uzamili ya kemia na aliwahi kufanya kazi kama mwalimu wa sayansi na hisabati. Alikuwa mbunge mwaka 1995 na kupanda cheo hadi kuwa rais mwaka 2015.

    Serikali imesema Bwana Magufuli amefariki dunia kutokana na maradhi ya moyo.

  6. Jinsi Magufuli anakavyokumbukwa katika kijiwe hiki cha kahawa,Geita

    Video content

    Video caption: Kifo cha Magufuli:Jinsi Magufuli atakavyokumbukwa katika kijiwe hiki cha kahawa,Geita
  7. Kifo cha Rais Magufuli: Rais wa Malawi asema Magufuli alikuwa kiungo muhimu

    "Ni pigo kwa Afrika," asema Rais wa Malawi Lazarus Chakwera baada ya kupokea taarifa za kifo cha Rais wa Tanzania John Magufuli, 61.

    "Rais Magufuli walikuwa ishara kuu ya ufufuo wa uchumi wa Afrika, na kifo chake ni pigo kubwa kwa bara hili," Bw. Chakwera aliongeza katika ujumbe wake wa Twitter.

    View more on twitter
  8. Kifo cha Rais John Magufuli:CCM kufanya kikao maalum machi 20

    MAGU

    Wakuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wanatarajia kufanya kikao maalumu Jumamosi Machi 20, kufuatia kifo cha mwenyekiti wa CCM na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

    Philip Mangula makamu mwenyekiti Tanzania bara na Mzee Ali Mohamed Shein makamu mwenyekiti Tanzania visiwani wamekubaliana kufanya kikao maalumu na kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa Jumamosi katika ukumbi wa Lumumba jijini Dar es salaam.

    Aidha chama kitakuwa katika maombolezo kwa siku 21 sambamba na tangazo la serikali.

    Maelezo zaidi:

  9. Kifo cha Rais John Magufuli: Wafahamu viongozi wa Afrika waliofariki madarakani

    Mazishi ya aliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills
    Image caption: Mazishi ya aliyekuwa rais wa Ghana John Atta Mills

    Ni nadra kwa kiongozi wa nchi yoyote kufariki akiwa angali madarakani. Katika kipindi cha miaka 20 iliopita mkosi huo umeathiri mataifa mengi barani Afrika .

    Lakini ni kwa nini vifo kama hivi vinatokea sana barani Afrika?

    Soma zaidi:

  10. Kifo cha Rais Magufuli: Kauli na semi za Magufuli ambazo zitakumbukwa na wengi

    Magufuli
    Image caption: Alipopewa tiketi ya CCM kuwania urais, Julai 14 2015
    Magufuli
    Image caption: Kuhusu hofu ya Corona na uvaaji wa barakoa Tanzania
    Magufuli
    Image caption: Kuhusu umoja wa Watanzania
    Magufuli
    Image caption: Kuhusu wizi wa dhahabu na madini kutoka Tanzania, Julai 2017
  11. Kifo cha Rais Magufuli: Rais Ndayishimiye amlilia Magufuli

    mm

    Raisi wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameelezea kusikitishwa na kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

    Ametuma salamu za rambirambi na dua kwa serikali,familia na watanzania kwa kumpoteza kiongozi shupavu na mzalendo wa kweli.

    View more on twitter
  12. Kifo cha Rais Magufuli: Mechi za kirafiki zasimamishwa Tanzania na Kenya kupisha maombolezo

    Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF limesimamisha mechi zake zote za ndani kwa wiki mbili ili kuungana na watanzania katika maombolezo.

    TFF

    Aidha Kenya imehairisha mechi ya pili ya kirafiki dhidi ya Tanzania iliyopangwa kuchezwa Alhamisi hii jijini Nairobi.

    Kocha Jacob Mulee,ameeleza kuwa mechi hiyo imeitishwa kufuatia kifo cha raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli.

    Hakuweka wazi ikiwa mechi hiyo itachezwa siku gani.

    Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa sehemu ya maandalizi ya Kenya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Misri na Togo zilizopangwa baadae mwezi huu.

  13. Kifo cha Magufuli: Vichwa vya habari magazetini

    Magu
    Magazeti
    Image caption: Watanzania waliamkia taarifa za kifo cha Rais Magufuli
  14. Kifo cha Magufuli: Wanyarwanda wako pamoja na Tanzania wakati huu mgumu

    maguu

    Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametuma salamu zake za rambirambi kupitia kurasa ya Twitter.

    "Tunasikitika kumpoteza kaka na rafiki yangu, Rais Magufuli , Mchango wake katika taifa lake na kwa bara la Afrika hautasahaulika.

    Salamu zangu za dhati ziende kwa familia na Watanzania.

    Wanyaruanda wako pamoja na Watanzania katika wakati huu mgumu.

    View more on twitter

    Rais Magufuli alifanikiwa kurudisha uhusiano mzuri na taifa la Rwanda na Tanzania baada ya mvutano wa miaka miwili kati ya mataifa hayo uliokuepo wakati wa utawala wa rais Jakaya Kikwete.

    Katika safari yake nchini Rwanda, bwana Magufuli alisema alialikwa maeneo mengi na hakwenda lakini wakati rais Kagame alivyomualika ,aliamua kwenda”.

    Rais Kagame alimpa rais Magufuli ng'ombe watano wakati alipotembelea Rwanda ikiwa ishara ya urafiki wa kweli na imara.

  15. Kifo cha Magufuli: Mfahamu Samia Suluhu Hassan, Rais ajaye wa Tanzania

    SAMIA NA MAGUFULI

    Mama Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa Makamu wa Rais toka mwaka 2015 sasa atakuwa mrithi wa rais John Magufuli ambaye amefariki jana Jumatano Machi 17.

    Soma zaidi:Je, Samia Suluhu Hassan ni nani?

  16. Kifo cha Rais Magufuli: Bobi Wine atuma salamu za rambirambi kwa Watanzania

    Aliyekuwa mgombea urais wa chama cha upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine atuma salamu za rambirambi kwa raia wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

    View more on twitter
  17. Kifo cha Rais Magufuli: Wafahamu viongozi wa Afrika waliofariki madarakani

    Ghaphics
  18. Kifo cha Rais Magufuli: Afrika Kusini yaungana na Tanzania katika maombolezo

    south

    Raisi wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania, John Magufuli.

    Katika taarifa yake, raisi Ramaphosa amesema amezungumza na Makamo wa Raisi wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimweleza huzuni yake na kwa niaba ya raia wa Afrika Kusini.

    ‘’Afrika Kusini inaungana na serikali na watu wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu’’alisema.

    View more on twitter
  19. Kifo cha Rais Magufuli: Museveni asema Magufuli alikuwa kiongozi anayeongoza kwa uhalisia

    Museveni

    Rais wa Uganda, Yoweri Mseveni ametuma salamu za rambirambi katika ukurasa wake wa Twitter.

    Rais Museveni amesema, amesikitishwa sana na kifo cha Rais Magufuli.

    Alikuwa kiongozi ambaye anaongoza kwa uhalisia na aliyeamini katika kukuza uchumi wa Afrika Mashariki.

    Tunajumuika na Watanzania kuomboleza kifo cha mtoto wa Afrika.

    Roho yake ipumzike kwa amani.

    View more on twitter
  20. Kifo cha Rais Magufuli:'Nimempoteza rafiki, mwenzangu na mshirika mwenye maono'

    magu

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kwamba amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, na kutuma salamu za rambi rambi kwa mjane Janet Magufuli, serikali na watu wa Tanzania.

    Rais Kenyatta amesema Magufuli alikuwa was kiongozi wa Afrika mwenye maono. ‘Nimempoteza rafiki, mwenzangu na mshirika wa karibu, alisema.

    View more on twitter

    Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ametangaza siku saba ya maombolezo kitaifa nchini Kenya kwa heshima ya hayati Rais John Magufuli.

    Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bendera ya Kenya zitapeperushwa nusu mlingoti katika majengo yote ya serikali nchini Kenya na katika balozi zake nje ya nchi, hadi siku Magufuli atakapozikwa.