Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu na Yusuf Jumah

time_stated_uk

  1. Na hadi hapo tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo.Hadi hapo kesho panapo majaaliwa

  2. Tesla yawafuta kazi 10% ya wafanyakazi wake

    th

    Tesla itapunguza zaidi ya 10% ya wafanyakazi wake wa kampuni hiyo ya magari ya umeme.

    Katika arifa, iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya habari ya Electrek, mmiliki na bilionea Elon Musk aliwaambia wafanyakazi hakuna kitu anachochukia zaidi kuliko hatua hiyo "lakini lazima ifanyike".

    Kampuni hiyo kubwa zaidi ya kutengeneza magari ilikuwa na wafanyakazi 140,473 duniani kote kufikia Desemba, kulingana na ripoti yake ya hivi punde ya kila mwaka.

    Tesla haikujibu mara moja ombi la BBC la kutoa maoni.

    Mfanyikazi wa Tesla ambaye alikuwa ameambiwa kwamba anapoteza kazi yake aliambia BBC kwamba alikuwa amefungiwa barua pepe zake kama vile wafanyikazi wengine wote walioachishwa kazi.

  3. Rainford Kalaba: Nahodha wa zamani wa Zambia yuko katika hali 'mbaya lakini dhabiti' baada ya ajali mbaya

    th

    Nahodha wa zamani wa Zambia, Rainford Kalaba yuko katika hali "mbaya lakini dhabiti" kufuatia ajali mbaya ya barabarani siku ya Jumamosi, kulingana na chama cha soka cha nchi hiyo (Faz).

    Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 37 alikuwa abiria katika gari aina ya Mercedes Benz ilipogongana na lori lililokuwa likija katika mji wa Kafue kusini-mashariki mwa Zambia.

    Dereva wa kike wa gari alilokuwa akisafiria Kalaba aliaga dunia

    Faz inasema Kalaba, ambaye yuko hospitalini, alipata "majeraha ya ndani".

    Ripoti ya polisi iliyotolewa baada ya ajali hiyo ilisema uchunguzi wa awali unaonyesha ajali hiyo ilitokana na hatua ya gari hilo la mercedes "kulipita vibaya" lori hilo.

    Habari kuhusu Kalaba zinafuatiliwa kwa karibu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mshambuliaji huyo aliichezea TP Mazembe kati ya 2011 na 2023.

    Kulikuwa na mkanganyiko juu ya hali ya Kalaba mara baada ya ajali hiyo wakati Mazembe ilipotuma taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambazo klabu hiyo imezitolea ufafanuzi.

  4. Safari za ndege zasitishwa na kutatizika baada ya shambulio la Iran dhidi ya Israel

    th

    Abiria wa mashirika ya ndege wanakabiliwa na kuahirishwa au kutatizwa kwa safari za ndege kuelekea Israel na nchi jirani baada ya mashambulizi ya anga ya Iran mwishoni mwa juma.

    EasyJet imesitisha safari za ndege kwenda na kutoka Tel Aviv hadi na ikijumuisha Jumapili, 21 Aprili.

    Wizz Air ilisema itaanza tena safari za kuelekea Israel Jumanne, 16 Aprili baada ya kusimamisha safari za ndege kuelekea Tel Aviv siku ya Jumapili na Jumatatu.

    Hata hivyo, ilionya: "Abiria wanaweza kupata mabadiliko fulani ya ratiba."

    Wizz Air ilisema kuwa "inafuatilia kwa karibu hali hiyo na mamlaka husika na kuwafahamisha abiria wake kuhusu mabadiliko yote ya ratiba".

    "Abiria wote walioathiriwa na mabadiliko ya ratiba watapewa chaguzi za kuweka tena nafasi au kurejeshewa pesa," iliongeza.

    Israel ilifunga anga yake Jumamosi jioni baada ya Iran kufanya shambulio la kwanza kabisa la moja kwa moja dhidi ya nchi hiyo. Iran ilirusha ndege zisizo na rubani na makombora kuelekea Israel kulipiza kisasi shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Tehran mjini Damascus tarehe 1 Aprili, ambalo liliua baadhi ya makamanda wakuu wa Iran.

    Israel haijasema ilitekeleza shambulio hilo la ubalozi mdogo, lakini inaaminika kuwa ndiyo iliyohusika .

  5. Habari za hivi pundeWanajeshi wanne wa Israel wajeruhiwa katika mlipuko wa Hezbollah - IDF

    TH

    Kwingineko katika Mashariki ya Kati, Israel inasema wanajeshi wake wanne wamejeruhiwa, mmoja vibaya sana, katika mlipuko uliotokea usiku kucha katika "eneo la mpakani" kaskazini mwa Lebanon.

    Kundi la Hezbollah la Lebanon, ambalo mara kwa mara limekuwa likipambana na wanajeshi wa Israel kaskazini, linasema kuwa vikosi vyake vililipua vilipuzi baada ya wanajeshi wa Israel kuvuka mpaka katika ardhi ya Lebanon.

    Jeshi la Israel halikuthibitisha iwapo vikosi vyake viliingia Lebanon.

    Hezbollah ni kundi la wanamgambo wa Kishia wa Lebanon wenye uhusiano wa karibu na Iran na mshirika wa Hamas. Imekuwa ikifanya mapigano ya kuvuka mpaka na Israel karibu kila siku tangu vita vilipozuka kati ya Israel na Hamas.

  6. Israeli itaona shambulizi la Iran kama 'kitendo cha vita'

    th

    Mchambuzi wa zamani wa Nato Dkt Patrick Bury amekuwa akizungumza na BBC Radio 5 Live kuhusu shambulio la ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran dhidi ya Israel siku ya Jumamosi.

    Israel kwa kawaida hujibu masuala yake ya usalama kwa kusema, "'tunahitaji kuwa wakali'", Bury anasema.

    "Mawazo yao ni kwamba hiki ni kitendo cha vita," anasema, akiongeza kuwa Israeli labda "haijui yenyewe" jinsi watakavyojibu.

    Bury anasema "hajui" jinsi Israeli inaweza kujibu lakini anaongeza kuwa "mashambulizi ya mtandaoni, operesheni za siri [au] mauaji" zimekuwa njia zilizotumiwa na Israeli hapo awali.

    Bury pia anasema kumekuwa na mtafaruku mkubwa kati ya Israel na Marekani kuhusu vita vya Gaza, na mashambulizi ya Iran, ni "ushindi" kwa Israel kwani "imeilazimisha Marekani kurejea upande wa Israel zaidi".

    Israel itaamua kujibu kwa njia gani?

    Jeshi la israel linasemekana kuwasilisha chaguzi mbalimbali kwa ajili ya mashambulizi yanayoweza kutokea dhidi ya Iran - huku baraza la mawaziri la vita sasa likiyapa uzito katika mkutano uliopangwa kuanza sasa.

    Chanzo cha habari cha Israel kimekuwa kikitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba Israel haiwezi kuruhusu shambulio kubwa kama hilo - linalohusisha zaidi ya droni 300 na makombora, yaliyorushwa moja kwa moja kutoka Iran kwa mara ya kwanza - kupita bila aina fulani ya majibu.

    Baadhi ya wanasiasa wa Israel wanahoji kuwa ujumbe mzito unahitaji kutumwa ili Iran isirudie hatua yake.

    Hata hivyo, watu muhimu katika baraza la mawaziri la vita pia wamekuwa wakisisitiza fursa ya kuimarisha "muungano wa kimkakati" dhidi ya tishio kutoka kwa Iran - wakijenga uungaji mkono ulioonyeshwa na Marekani, Uingereza, Jordan na washirika wengine katika kuzuia mashambulizi.

    Wakati wa shambulio hilo, Israel inasema Iran ilijaribu kushambulia miundombinu muhimu kimkakati ikiwa ni pamoja na kambi ya jeshi la anga ya Nevatim - ambapo huhifadhi ndege zake za kivita - lakini ilishindwa kuwa na athari.

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  7. Macron asema sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris zinaweza kuhamishwa

    TH

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Paris zinaweza kuhamishwa kutoka Mto Seine ikiwa hatari ya usalama ni kubwa sana.

    Bw Macron alisema inaweza kufanywa tu katika eneo la Trocadéro", ng'ambo ya Seine kutoka Mnara wa Eiffel, badala ya kufunga sehemu iliyopangwa ya mto huo.

    Aliongeza kuwa inaweza hata kuhamishwa hadi Stade de France, na kurejelea sherehe za kitamaduni.

    Alisema atafanya "kila linalowezekana" kuwa na suluhu ya Olimpiki.

    Rais wa Ufaransa alikuwa akidokeza utamaduni wa kihistoria kwamba amani lazima iwepo wakati wa michezo ya Olimpiki.

    Katika mahojiano na BFMTV na RMC katika Grand Palais, moja ya kumbi za Olimpiki, Bw Macron alisema: "Tunataka kufanya kazi kuelekea suluhu ya Olimpiki na nadhani ni fursa kwangu kushirikiana na washirika wetu wengi."

    Sherehe ya ufunguzi tarehe 26 Julai inatazamiwa kuwa ya kwanza kufanyika nje ya uwanja wa michezo. Zaidi ya wanariadha 10,000 wanatarajiwa kusafiri kwa umbali wa kilomita 6 wa Seine kwa mashua 160 hivi.

    Hapo awali waandalizi walikuwa wamepanga kuwapokea watu wapatao 600,000 kutazama sherehe hiyo kutoka kwenye kingo za mito.

  8. Washirika wa Magharibi waitaka Israeli kujiepusha na hatua zitakazozidisha mgogoro

    th
    Image caption: Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito wa kuwepo utulivu

    Macho yote yanaelekezwa kwa Israel kuona jinsi inavyojibu mashambulio ya wikendi ya Iran ya droni na makombora lakini washirika wake wameitaka iepuke kuzidisha mzozo huo

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anasema Israel "imeshinda kwa kujilinda" katika ugomvi wake na Iran, na lazima kusiwe na ongezeko la mzozo katika eneo hilo.

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaungana na wito wa kudumisha utulivu na kusema nchi yake itafanya kila linalowezekana kuepusha kuongezeka kwa mgogoro.

    Na kama tulivyoripoti hapo awali,Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron aliiambia BBC kwamba alifikiri Israel "ilikuwa na haki kabisa" kujibu Iran - lakini akahimiza nchi hiyo kuwa makini na "kufikiri kwa kichwa, siokwa moyo".

    Urusi na China zataka kujizuia baada ya Iran kuishambulia Israel

    Pamoja na washirika wa Israel, nchi zinazotajwa kuwa na mafungamano ya karibu zaidi na Iran zimezitaka pande zote mbili kujizuia.

    Urusi ilijiepusha na kuikosoa hadharani Iran juu ya shambulio hilo, lakini ilishiriki wasiwasi juu ya hatari ya kuongezeka kwa mzozo.

    "Kuongezeka zaidi hakutakidhi maslahi ya mtu yeyote," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kuhusu vita katika Mashariki ya Kati.

    Wizara ya mambo ya nje ya China pia ilitoa wito wa utulivu na "kujizuia na kuepuka kuzidisha mivutano".

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  9. Afisa wa Iran aziambia nchi za Magharibi kuacha kutoa shutuma

    th

    Tehran imetoa wito kwa mataifa ya Magharibi "kuthamini kujizuia kwa Iran" dhidi ya Israel baada ya kuishambulia nchi hiyo siku ya Jumamosi kulipiza kisasi shambulio baya dhidi ya ubalozi wake mdogo mjini Damascus, Syria.

    Iran ilirusha zaidi ya droni 300 na makombora kuelekea Israel lakini takriban 99% ya mashambulizi hayo yalizuiwa, maafisa wa Israel wamesema tangu wakati huo.

    "Badala ya kutoa shutuma dhidi ya Iran, nchi [za Magharibi] zinapaswa kujilaumu na kujibu maoni ya umma kwa hatua ambazo zimechukua dhidi ya ... uhalifu wa kivita uliofanywa na Israel" katika vita vyake huko Gaza, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanani alisema.

    Kanani aliongeza kuwa nchi za Magharibi "zinapaswa kufahamu kujizuia kwa Iran katika miezi ya hivi karibuni".

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  10. Wanariadha wa Afrika wajipata katika uchunguzi wa mbio za nusu marathon za China

    th

    Waandalizi wa mbio za Beijing Half Marathon wameanzisha uchunguzi kuhusu madai ya upangaji wa matokeo ya mbio zinazohusisha wanariadha wa Ethiopia na Kenya.

    Katika picha ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanariadha wa Ethiopia Dejene Hailu na wanariadha wa Kenya Robert Keter na Willy Mnangat walionekana kumwachia kimakusudi mwanariadha wa China He Jie kushinda mbio za nusu marathon siku ya Jumapili.

    Waafrika watatu walionekana kupunguza kasi walipokaribia mstari wa kumalizia na kuashiria mara kwa mara He awafikie hadi kwenye utepe wa kumalizia .

    He, mshindi wa medali ya dhahabu ya mbio za marathon za Michezo ya Asia 2023, kisha alipongezwa na wanariadha watatu wa Kiafrika baada ya kushinda mbio hizo kwa sekunde.

    Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wa Uchina wamekosoa ushindi wake kuwa "wa aibu" na usio wa kiuanamichezo, huku kukiwa na uvumi kwamba matokeo ya kinyang'anyiro hicho yalichakachuliwa.

    "Tunachunguza na tutatangaza matokeo kwa umma mara tu yatakapopatikana," mwakilishi wa Ofisi ya Michezo ya Beijing aliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

    Mratibu wa mbio za marathon pia alithibitisha kuwa uchunguzi umeanzishwa, AFP iliripoti.

    He, Hailu, Keter au Mnangat hawajatoa maoni yao kuhusu uchunguzi huo.

  11. Shambulio la kombora lilikuwa 'kushindwa mara mbili' kwa Iran-asema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza

    th

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Cameron amekuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo Iran ilifanya mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel.

    Haya ndio mambo muhimu aliyoyasema:

    • Cameron hakuwa na shaka kwamba Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka kwa Iran - lakini alisema ushauri wa Uingereza sio kulipiza kisasi, akitoa wito kwa Israel kufikiria kwa "kichwa chake, na si kwa moyo wake"
    • Shambulio hilo kutoka kwa Iran lilikuwa "kushindwa mara mbili", kwa Iran -alisema, kwa sababu limeshindwa katika suala la uharibifu kwa Israeli na ilionyesha Iran kuwa "ushawishi mbaya katika eneo hilo"
    • Cameron alipongeza kuhusika kwa RAF katika kutungua ndege zisizo na rubani zilizokuwa zikielekea Israel Jumamosi usiku. Kama shambulio hilo lingefaulu, alisema, maelfu wangekufa
    • Alipoulizwa iwapo Uingereza imekuwa na ukali wa kutosha kwa Israel katika suala la kuwalinda raia wa Palestina huko Gaza, alisema juhudi za Uingereza zinalenga kuhakikisha mapiganoyanasitishwa na kupata misaada ya kuinia Gaza.

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  12. 'Watoto hawakulala usiku kucha' - Israel kuhusu shambulio la Iran

    Hugo Bachega

    Middle East correspondent, in Jerusalem

    th

    Hadithi ya shambulio la kipekee la Iran dhidi ya Israeli ingekuwa tofauti kama matayarisho ya Israeli hayangefaulu sana. Israel inasema 99% ya ndege 300 zisizo na rubani na makombora ya baharini na ya balestiki ambayo yalikuwa yamerushwa yaliangushwa na nchi hiyo na washirika wake.

    Siku ya Jumapili, Israeli iliporejea katika hali ya kawaida, hiyo ilikuwa chanzo cha sherehe - wakati kila mtu, hapa na mahali pengine, akingojea jibu mwafaka kutoka kwa Israeli.

    "Nguvu za Israeli ni kwamba tuna ngao, ulinzi dhidi ya vitisho hivi," Ariel mwenye umri wa miaka 54 ananiambia, huko Jerusalem. “[Shambulio la Irani] lilitarajiwa ... Israel labda itajibu. Natumai hakutakuwa na vita”

    Shambulio la Iran halikuwa jambo la kustaajabisha, kwani kwa takriban wiki mbili nchi hiyo ilikuwa imetangaza nia yake ya kujibu shambulio la anga kwenye makao yake ya kidiplomasia katika mji mkuu wa Syria, Damascus, ambalo liliua washauri kadhaa wa kijeshi, wakiwemo majenerali wawili wakuu - shambulio linaloaminika na watu wengi kufanywa na Israel.

    "Tulijua kwamba Iran ingeshambulia ... Tulikuwa na wasiwasi kidogo. Lakini tunajua tuna ngao kubwa,” Einat mwenye umri wa miaka 44 anasema. "Hatutaki mambo yawe mabaya zaidi [na majibu]."

    Marekani ilikuwa mojawapo ya nchi zilizosaidia katika ulinzi wa Israel, lakini maafisa wa utawala wa Biden wanasema hakutakuwa na uungaji mkono wa Marekani kwa jibu la Israel, na kwamba hatua ya Israel kwenye shambulio hilo tayari ilikuwa ushindi dhidi ya Iran.

    "Ilikuwa [usiku] wa kutisha, watoto hawakulala usiku kucha, walikuja kitandani kwetu, wakalala nasi," Moran mwenye umri wa miaka 41 anasema. "Tuna jeshi lenye nguvu zaidi ulimwenguni, na tunaamini itakuwa sawa. Natamani tungeshambulia, lakini hatuwezi kwa sababu ya Marekani.

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  13. Nani aliye na nguvu zaidi za kijeshi kati ya Iran na Israel?

    th

    Iran ni kubwa zaidi kuliko Israel kijiografia na ina idadi ya watu karibu milioni 90, karibu mara 10 zaidi ya Israeli - lakini hii haimaanishi kuwa ina nguvu kubwa zaidi ya kijeshi.

    Iran imewekeza fedha nyingi kwenye makombora na ndege zisizo na rubani. Ina hifadhi kubwa ya silaha hizo lakini pia imekuwa ikitoa kiasi kikubwa kwa washirika wake - Wahouthi nchini Yemen na Hezbollah nchini Lebanon.

    Inachokosa ni mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga na ndege za kivita. Urusi inaaminika kushirikiana na Iran kuboresha hizo, kwa kurudisha msaada wa kijeshi ambao Tehran imetoa Moscow katika vita vyake na Ukraine - hasa katika mfumo wa ndege zisizo na rubani za Shahed ambazo Warusi sasa wanaripotiwa kutengeneza wenyewe.

    Kwa upande wake, Israeli ina moja ya vikosi vya anga vya juu zaidi ulimwenguni. Kulingana na ulinganishi wa kijeshi wa IISS, Israel ina takriban vikosi 14 vya ndege - ikiwa ni pamoja na F15, F16 na ndege za hivi punde za F-35.

    Israel pia ina tajriba ya kufanya mashambulizi ndani kabisa ya maeneo ya mahasimu wake

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  14. Mataifa ya Afrika yatoa wito wa kujizuia kutokana na mvutano kati ya Iran na Israel

    Kuna hofu kwamba mvutano huo unaweza kuongeza bei ya mafuta duniani

    Nchi kadhaa za Kiafrika zimeitaka Israel ijizuie wakati baraza lake la mawaziri la vita likikutana ili kuamua iwapo italipiza kisasi dhidi ya shambulio la anga la Iran.

    Iran ilisema ilifanya shambulio hilo kujibu shambulio la anga la Israel kwenye ubalozi mdogo wa Damascus tarehe 1 Aprili na kuwaua maafisa wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

    Shambulio hilo lilihusisha zaidi ya ndege zisizo na rubani 300 na makombora, mengi zaidi yalinaswa, jeshi la Israel lilisema.

    Nigeria, Kenya, Afrika Kusini na Somalia ni nchi za Afrika ambazo zimetoa wito wa kujizuia ili kuepusha kuongezeka zaidi.

    Idara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini ilisema katika taarifa yake kwenye ukurasa wake wa X kwamba "wahusika wote lazima wajizuie kabisa na waepuke kitendo chochote ambacho kinaweza kuzidisha mvutano katika eneo hilo".

    Rais wa Kenya William Ruto aliitaka Israel "ioneshe kujizuia kwa hali ya juu kwa kuzingatia hitaji la dharura la pande zote kuondoka ukingoni ambako kutakuwa na ugumu mkubwa wa kupona".

    Alisema shambulio la Iran "linawakilisha tishio la kweli na la sasa kwa amani na usalama wa kimataifa".

    Somalia ilitoa wito kwa "jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti ili kupunguza hali hiyo na kupunguza hatari ya mzozo zaidi".

    Wizara ya mambo ya nje ya Nigeria ilizitaka Israel na Iran "kutafakari juu ya dhamira ya wote ya kutatua mizozo kwa njia ya amani". Si Iran wala Israel yenye uhusiano mkubwa wa kisiasa katika Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  15. Baraza la vita la Israel latofautiana kuhusu muda na ukubwa wa jibu la shambulio la Iran

    .

    Nchini Israeli, shule zilifungwa, na mikusanyiko ya hadhara kuzuiliwa kama tahadhari kabla ya Iran kurusha makombora na ndege zisizo na rubani zaidi ya 300, lakini uamuzi wa kulegeza msimamo uliotangazwa na jeshi la Israel jana usiku unaonyesha tishio la wimbi jipya la mashambulizi limepita.

    Kwa upande mwingine, baada ya masaa matatu ya mashauriano, Baraza la Vita la Israel, katika kikao chake cha jana, halikufikia uamuzi wa namna ya kujibu mashambulizi ya Iran.

    Baraza la Vita linasemekana kuunga mkono ulazima wa jibu, lakini limegawanywa kulingana na muda na kiwango cha jibu hilo.

    Israel inasema kuwa ndege na makombora yote ya mashambulizi yalitenguliwa nje ya anga yake kwa usaidizi wa washirika wake, huku Iran ikisema ilizipa nchi jirani na Marekani notisi ya saa 72 kabla ya kufanya mashambulizi hayo.

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  16. Guterres: Mashariki ya Kati 'inakaribia kutumbukia katika vita', aonya mkuu wa Umoja wa Mataifa

    .
    Image caption: Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaonya wanachama kutozidisha mvutano na kulipiza kisasi dhidi ya Iran, akisema kuwa Mashariki ya Kati tayari "inakaribia kutumbukia katika vita".

    Akizungumza katika Baraza la Usalama Jumapili jioni, alisema: "Watu wa eneo hilo wanakabiliwa na hatari halisi ya mzozo mkubwa kabisa. Sasa ni wakati wa kutuliza na kupunguza kasi. Si eneo hilo wala ulimwengu unaoweza kumudu vita zaidi."

    Katika mkutano huo huo, mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Israel alilitaka Baraza la Usalama kuweka "vikwazo vyote vinavyowezekana" dhidi ya Iran baada ya mashambulizi makubwa ya taifa hilo.

    Zaidi ya ndege 300 zisizo na rubani na makombora zilirushwa dhidi ya Israel usiku wa kuamkia Jumamosi, jambo ambalo Iran ilisema ni kujibu shambulio la Aprili 1 dhidi ya ubalozi mdogo nchini Syria. Makombora yote yaliharibiwa kabla ya kufikia malengo yao.

    "Leo baraza lazima lichukue hatua (na) kulaani Iran kwa ugaidi wao," balozi wa Israel Gilan Erdan alisema katika mkutano huo mkali.

    Kwa sasa, macho yote yanaelekezwa kwa Israel huku ikipima majibu yanayoweza kukabili mashambulizi hayo.

    Unaweza pia kusoma

    Israel - Marekani: Ipi siri ya uhusiano wao usiochuja?

    Vita ya Israeli na Hamas: Kwa nini Marekani inaiunga mkono Israeli

    Iron Dome: Fahamu jinsi mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel unavyofanya kazi

  17. Maporomoko ya udongo DR Congo yaua takriban watu 12, zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo

    Takriban watu 12 wamefariki na zaidi ya 50 bado hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kusababisha bonde kuporomoka kwenye mto kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.kwa mujibu wa afisa wa eneo hilo

    Maporomoko ya ardhi yalitokea Jumamosi saa sita mchana katika wilaya ya Dibaya Lubwe katika jimbo la Kwilu.

    Mafuriko hayo yalisomba na kupeleka udongo na uchafu kwenye ukingo wa Mto Kasai, ambapo mashua ilikuwa ikitia nanga na watu walikuwa wakifua nguo.

    Gavana wa muda wa mkoa Felicien Kiway alisema miili 12 imetolewa kwenye vifusi hadi sasa, ikiwa ni pamoja na wanawake tisa, wanaume watatu na mtoto mchanga.

    "Takriban watu 50 hawajulikani walipo lakini tunaendelea kupekua udongo," alisema na kuongeza kuwa uwezekano wa kupata manusura ulikuwa mdogo kwani tukio hilo lilitokea saa 12 kabla.

    Mratibu wa jumuiya ya kiraia ya eneo hilo, Arsene Kasiama, alisema maporomoko hayo pia yaliangukia watu waliokuwa wakinunua bidhaa sokoni.

    Alitoa idadi ya vifo vya watu 11, na manusura saba waliojeruhiwa vibaya na zaidi ya watu 60 wakiwa hawajulikani waliko Mipango duni ya mijini na miundombinu duni kote Kongo hufanya jamii kuwa katika hatari zaidi ya mvua kubwa, ambayo inazidi kuongezeka mara kwa mara barani Afrika kulingana na wataalam wa hali ya hewa.

  18. Mafuriko ya Tanzania yaua takribani watu 60 katika nusu ya kwanza ya mwezi

    .
    Image caption: Mafuriko Tanzania

    Takriban watu 60 wamekufa tangu kuanza kwa mwezi huu kutokana na mvua kubwa na mafuriko ambayo yamekumba maeneo kadhaa ya Tanzania, serikali ilisema.

    Eneo la pwani la nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni mojawapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi, huku mafuriko yakiharibu maelfu ya mashamba huko, Mobhare Matinyi, msemaji wa serikali, alisema katika taarifa Jumapili.

    "Madhara makubwa ya mafuriko yanashuhudiwa katika eneo la pwani ambapo watu 11 wamefariki kufikia sasa," Bw Matinyi aliongeza.

    Alisema vifo 58 vimerekodiwa hadi sasa kutokana na mafuriko hayo.

    Ijumaa iliyopita, watoto wanane wa shule walifariki baada ya basi lao kutumbukia kwenye korongo lililofurika kaskazini mwa nchi.

    Aprili ni kilele cha msimu wa mvua nchini Tanzania.

    Mwaka huu umeshuhudia mvua kubwa zaidi ya miaka ya hivi karibuni.

    Mvua hiyo kubwa pia imesababisha vifo vya takriban watu 13 na wengine 15,000 kuyahama makazi yao katika nchi jirani ya Kenya, UN ilisema.Hali ya hewa ya El Niño imezidisha mvua za msimu wa mwaka huu, wataalam wa hali ya hewa walisema.

    Mvua kubwa: Mafuriko Tanzania na Kenya

  19. Tulichangia kuharibu ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran kushambulia Israel- Marekani

    Marekani imesema vikosi vyake, viliweza kuharibu ndege 80 zisizo na rubani pamoja na makombora sita ya balestiki mnamo Aprili 13-14.

    Marekani ilieleza kuwa ndege na makombora hayo yalirushwa kutoka Yemen na Iran kwa lengo la kuishambulia Israel, na kubainisha kuwa vikosi vyake viliweza kuharibu kombora la balistiki lililokuwa tayari kurushwa na ndege zisizo na rubani saba katika maeneo yanayodhibitiwa na Houthis nchini Yemen kabla hazijarushwa .

    Uongozi wa Marekani umetahadharisha kwamba, kuendelea kwa tabia ya Iran "isiyo na kifani, chuki na uzembe" inahatarisha utulivu wa kikanda na usalama wa vikosi vya Marekani na muungano, na kusisitiza kwamba vikosi vyake viko katika nafasi ya kuunga mkono "ulinzi wa Israel dhidi ya vitendo hivi hatari vinavyofanywa na Iran" kwa ushirikiano na washirika wote wa kikanda, kulingana na taarifa hiyo.

  20. Mgogoro wa Israel na Iran: Tunachojua kufikia sasa

    Huu ni muhtasari wa haraka wa matukio muhimu kutoka saa 24 zilizopita Mashariki ya kati

    • Israel ilishambuliwa na wimbi la ndege zisizo na rubani na makombora katika mashambulizi ya kwanza ya moja kwa moja ya Iran katika ardhi yake.
    • Shambulio hilo lilihusisha zaidi ya ndege 300 zisizo na rubani na makombora - mengi yalinaswa, jeshi la Israel lilisema.
    • Kombora moja la balistiki lilipiga kambi ya anga ya Nevatim kusini mwa nchi, na kusababisha uharibifu mdogo, maafisa walisema.
    • Iran ilisema shambulio hilo lilikuwa jibu la shambulio baya dhidi ya makao ya wanadiplomasia wa Iran nchini Syria mapema mwezi huu.
    • Tehran pia ilionya ikiwa Israel italipiza kisasi jibu lake lijalo litakuwa kubwa zaidi.
    • Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliitisha baraza la mawaziri la vita kujadili shambulio hilo, ambalo lililaaniwa tofauti na viongozi wa kimataifa akiwemo Rais wa Marekani Joe Biden, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
    • Rais wa Marekani ameandaa mkutano wa mtandaoni wa viongozi wa G7 huku Ikulu ya Marekani ikisisitiza kuwa haitaki kuona mzozo wa Mashariki ya Kati ukiongezeka.