Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

time_stated_uk

  1. Liverpool mabingwa FA CUP, yaichapa Chelsea kwa matuta

    Mount

    Liverpool wamefanikiwa kutwaa taji la FA Cup muda mfupi uliopita, baada ya kuwafunga Chelsea kwa mikwaju ya penati 6-5. Shujaa wa mchezo huo Allison Bekcer aliyeokoa mikwaju miwili ya penati.

    Penati ya ushindi kwa ilifungwa na mlinzi kinda Tsimikas. Kwa ushindi huu safari ya Liverpool kutwaa mataji manne msimu huu, huenda ikafanikiwa, kwani tayari wameshatwaa Carling Cup na sasa FA Cup, wakiwa nafasi ya pili kwa alama 2 nyuma ya Manchester City kwenye ligi ya mabingwa Ulaya na wako fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

    Kwa kufungwa mchezo huu, Chelsea inakuwa klabu ya kwanza kufungwa katika fainali za FA CUP mfululizo.

    Mpaka dakika 90 na zile 30 za nyongeza za mchezo huo zinamalizika, mchezo huo ulikwenda sare tasa ya bila kufungana.

    Nahodha wa Chelsea alikosa penati muhimu kwa upande wa Chelsea kama ilivyo kwa Mason Mount.

    Huku Marcos Alonso, Reece James, Ross Barkley na Jorginho wakifunga kwa upande wa Chelsea , Kwa upande wa Liverpool penati zake zilifungwa na James Milner, Thiago, Alexander-Arnold, Roberto, Jota, Firmino huku Sadio Mane na wakikosa.

    Katika mchezo huo nyota wa Liverpool, Mohamed Salah alilazimika kutolewa nje katika kipindi cha kwanza kutokana na kupata majeraha.

    Hofu imewatanda Liverpool kuhusu majeraha yake kama yatamuweka nje kwenye michezo miwili ya ligi kuu iliyosalia na ule wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

  2. UN yalaani mauaji ya mwandishi wa Al Jazeera, Aqla na kutaka uchunguzi wa haraka

    Aqla

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mauaji ya mwanahabari mkongwe wa Al Jazeera, Shireen Abu Aqla na kutaka uchunguzi ufanyike mara moja kuhusu kifo chake.

    Hatua hiyo ilifuatia vilio vya siku ya Ijumaa baada ya polisi wa Israel kuwapiga waombolezaji katika mazishi ya Abu Aqla. Polisi walisema walichukua hatua hiyo baada ya kupigwa mawe.

    Abu Aqla, 51, aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akifuatilia uvamizi wa kijeshi wa Israel huko Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu siku ya Jumatano.

    Kifo chake kimesababisha kuongezeka kwa hasira nchini humo. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa, Baraza la Usalama lilisema wanachama wake walitoa wito wa "uchunguzi wa haraka, wa kina, wa uwazi, na wa haki na usio na upendeleo juu ya mauaji hayo, na kusisitiza haja ya kuhakikisha uwajibikaji."

    Mamlaka za Palestina tayari zimeelezea kifo chake kama mauaji ya Israel, ambayo kwa upande wake imesema bado haijafahamika iwapo alikufa kutokana na shambulio la Israel au Palestina. Ripoti ya muda ya jeshi la Israel siku ya Alhamisi ilisema kwamba shambulio hilo linaweza kuwa limetokana na mashambulizi makali kutoka kwa wapiganaji wa Kipalestina", au labda kutoka kwa "risasi chache" zilizopigwa na mwanajeshi "gaidi ambaye alikuwa akifyatua risasi gari lake".

  3. Tanzania yatangaza nyongeza ya mishahara kujibu kilio cha wafanyakazi

    Mishahara

    Kima chini cha mshahara kwa wafanyakazi nchini Tanzania kimepanda kwa asilimia 23.3%. Taarifa ya Ikulu imesema.

    Taarifa hiyo iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Zuhura Yunus, imesema Rais Samia Suluhu ameridhia mapendekezo ya nyongeza hiyo mshahara yaliyowasilishwa Ikulu, ikiwa ni muendelezo wa kikao cha waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyepokea taarifa ya wataalamu mjini Dodoma kuhusu nyongeza ya mishahara.

    'nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi', ilisema taarifa hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali inatarajiwa kutumia shiligi trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote wa serikali Kuu, Serikali za Mtaa, Taasisi na Wakala za Serikali.

    View more on twitter

    Kutokana na nyongeza hiyo ya mishahara, bajeti ya mishahara ya mwakam 2022/2023 itaongezeka kwa shilingi trilioni 1.59 sawa na asilimia 19.51% ikilinganishwa na bajeti ya sasa ya mwaka wa fesdha 2021/2022.

    Mbali na hilo la mshahara, pia Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya mafao ya Pensheni, kama ilivyoombwa na chama cha wafanyakazi Tanzania (TUCTA) siku ya sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi, 2022), ambapo sasa amekubali ombi la kupandisha malipo ya mafao, kutoka 25% iliyokataliwa na wadau hadi 33.3%.

    Ametaka TUCTA, wizara ya fedha na Chama cha Waajiri (ATE), kuendelea kushirikiana ili kukamilisha taratibu za malipo ya mkupuo huo wa asilimia 33.3% badala ya 25% iliyokataliwa mwaka 2018.

    Katika maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya wafanyakazi, ilipendekezwa mshahara wa kima cha chini kwa mfanyakazi uwe shilingi milioni 1 za kitanzania. Mara ya mwisho wafanyakazi wa Tanzania kupandishiwa mshahara ilikuwa wakati wa utawala wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, Julai 2015.

  4. Watu milioni 20 wanakabiliwa na njaa kali Afrika Mashariki - UN

    Njaa

    Katika kijiji kisicho na watu huko Turkana, Kaskazini mwa Kenya, wanakijiji wanaomba mvua, lakini haiwezi kuja. Msimu wa nne sasa mvua haizijanyesha na kusababisha ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa, na kijiji hiki, ambacho kina familia 3,600, ni moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi.

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani linasema hadi watu milioni 20 katika Afrika Mashariki wako katika hatari ya njaa kali. Ethiopia inapambana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika takriban nusu karne na nchini Somalia asilimia 40 ya watu wako katika hatari ya njaa.

    njaa

    Ardhi ni kavu, vumbi na isiyozalisha. Mifugo iliyobaki hula vichaka vilivyonyauka. Watu hula chochote wanachoweza kupata, mara nyingi kwa uchache. Jacinta Atabo Lomaluk anaishi katika kijiji cha Lomoputh. Yeye ni mama wa watoto watano ambaye mwanawe mkubwa amekuwa akikabiliwa na utapiamlo tangu Septemba.

    Mtoto wa miaka 12 ni dhaifu na hawezi kutembea au hata kusimama peke yake. Anasema hajawahi kukumbana na hali mbaya ya ukame huu hapo awali. "Inazidi kuwa mbaya zaidi kuliko ilivyowahi kuwa. Ndiyo maana unaweza kuona dalili za njaa hapa."

    Njaa

    "Natamani kungekuwa na usaidizi wa haraka kuwaokoa wanaokabiliwa na njaa, haswa watoto ambao wako hatarini," anasema. "Vinginevyo, tunatarajia watu wengi zaidi kufa."

    Bi Lomaluk ni mmoja tu wa mamilioni wanaoathirika na athari ya ukosefu wa mvua. Familia zimekata tamaa ya kupata chakula na maji. Mamilioni ya watoto wana utapiamlo. Mifugo ambayo familia za wafugaji wanaitegemea kwa chakula na kuendesha maisha yao imekufa. Ukame unaenea zaidi ya kijiji hiki kidogo cha Kenya.

  5. 'Vita vya Ukraine huenda vikamalizika mwishoni mwa mwaka huu' - Kitengo cha Ujasusi Ukraine

    Kharkiv

    Mkuu wa kitengo cha kijasusi cha kijeshi cha Ukraine amesema vita na Urusi vitafikia hatua ya mabadiliko katikati ya mwezi wa Agosti na huenda vikamalizika mwishoni mwa mwaka huu.

    Katika mahojiano na Sky News, Meja Jenerali Kyrylo Budanov alisema kwamba "kilele cha mapambano k itakuwa katika wiki ya pili ya mwezi Agosti" na "mashambulizi mengi ya kivita huenda yakafikia kikomo mwishoni mwa mwaka huu."

    "Kutokana na hayo, tutaongeza upya nguvu ya Ukraine katika maeneo yetu yote ambayo tumepoteza ikiwa ni pamoja na Donbas na Crimea." Aliongeza kuwa Urusi ikishindwa katika vita hivyo itasababisha kupinduliwa kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin, mapinduzi ambayo alidai kuwa tayari yanaendelea. BBC haijathibitisha madai haya.

    Pia alidai kuwa Rais Putin alikuwa katika "hali mbaya sana kisaikolojia na kimwili na ni mgonjwa sana." Dai kama hilo halijathibitishwa.

    Katika hatua nyinginre Ripoti kutoka Ukraine zinasema Urusi imelazimika kuondoa vikosi vyake kutoka Kharkiv - ikionekana Ukraine "kushinda vita" katika mji huo.

  6. Uingereza yawawekea vikwazo 'wapenzi' wa Rais Putin

    Putin's former wife

    Uingereza imemuwekea vikwazo mke wa zamani wa Rais wa Urusi Vladimir Putin na anayedaiwa kuwa mpenzi wake wa sasa kutokana na uvamizi wa Ukraine.

    Lyudmila Ocheretnaya, ambaye alikuwa mke wa rais Putin hadi 2014, na mwanariadha wa zamani wa Olimpiki Alina Kabaeva, wanakabiliwa na marufuku ya kusafiri Uingereza na kuzuiwa kwa mali zao.

    Uingereza sasa imewaweka zaidi ya watu 1,000 kwenye orodha yake ya vikwazo vya Urusi.

    Waziri wa Mambo ya Nje Liz Truss alisema Uingereza ilikuwa "ikifichua na kulenga mtandao mbovu unaoendeleza maisha ya anasa ya Putin", alisema, na "itaendelea kuweka vikwazo kwa wale wote wanaosaidia na kuunga mkono uchokozi wa Putin hadi Ukraine itakaposhinda".

    Bi Truss alisema vikwazo dhidi ya Urusi vinapaswa kuondolewa tu wakati wanajeshi wake wote watakapoondoka Ukraine.

    Tangu aachane na Putin, Lyudmila Ocheretnaya amefaidika kutokana na mahusiano ya kibiashara ya upendeleo na mashirika yanayomilikiwa na serikali na kuonyesha utajiri mkubwa ambao haujaelezewa, Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza, Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) inasema.

    Kabaeva
    Image caption: Rais Putin akiwa na Vabaeva kwenye moja ya sherehe mwaka 2001

    Bi Kabaeva ni mbunge wa zamani wa Urusi na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya National Media Group, ambayo inaripotiwa kuwa kampuni kubwa ya kibinafsi ya vyombo vya habari vya Urusi, FCDO inasema.

  7. Rais Ukraine akiri ‘hali tete‘ kuwanusuru askari wake majeruhi waliozingirwa na Urusi huko Mariupol

    Mariupol

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuwepo kwa ugumu wa mazungumzo ya namna ya kuwaondoa askari majeruhi katika eneo lililozingirwa na kushambuliwa na Urusi, huko Mariupol.

    Akizungumza usiku wa kuamkia leo, kuhusu hali ilivyo Azovstal, Mariupol alieleza kuwa askari waliosalia wa Ukraine wanaopambana kulinda mji huo na ambao wengi wao wamejeruhiwa wanahitaji kuondolewa katika eneo hilo kwa ajili ya matibabu.

    Mji wa Mariupol ulioko Kusiku mwa Ukraine, ni mji muhimu kwa Urusi kimkakati, Urusi wamekuwa wakielekeza nguvu zao na kuushambulia askari wa Ukraine wanaoulinda ili kuuteka kwa miezi kadhaa sasa.

    Zelensku anakiri mazungumzo ya namna ya kuwaondoa ni magumu.

    "Majadiliano tata yanaendelea katika hatua nyinginre yenye lengo la kuwaondoa waliojeruhiwa vibaya," alisema.

    "Tunafanya kila liwezekanalo kuwaondoa wote, kila askari wetu mlinzi," Zelensky said.

    Ameongeza kuwa Kyiv imekuwa ikitumia "wapatanishi wenye ushawishi" katika mazungumzo hayo, lakini hakutoa maelezo zaidi.

  8. Karibu katika Matangazo yetu ya habari za moja kwa moja leo Mei 14, 2022