Rais Samia:“Tusiwe shamba la bibi” – aonya wanaharakati wa nchi jirani kutoingilia masuala ya Tanzania
Kauli hiyo inafuatia aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Martha Karua, Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga na wanaharakati wengine wawili, kuzuiwa kuingia nchini Tanzania.
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua nchini Kenya ameithubutu serikali kumkamata ikiwa ametenda uhalifu wowote.
Akihutubia wanahabari Jumatatu mjini Karen, Nairobi, Gachagua alionekana kujibu kauli tofauti za Naibu Rais Kithure Kindiki na Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen kwamba hawezi kuguswa na atakamatwa kwa madai ya matamshi yake ya uchochezi.
Alisema yeye wala wafuasi wake hawataogopa au kutishwa na matumizi ya mfumo wa haki ya jinai.
"Kama serikali inajua kwamba nimefanya uhalifu unaojulikana chini ya sheria za Kenya na kutambuliwa ndani ya kanuni ya adhabu, wanajua nyumba yangu ilipo ... na, niko hapa, wanajua nyumbani kwangu wamunyoro," alisema.
"Mchezo wa kutafutana barabarani unapaswa kukoma."
Alisema maafisa wa usalama badala yake wanapaswa kumfuata nyumbani na kuchukua hatua inayofaa.
Gachagua alikwepa maafisa wa polisi huko Muranga na kuelekea nyumbani kwake Wamunyoro huko Nyeri huku polisi wakimfuatilia.
Maafisa wanaofahamu operesheni hizo walisema hawakumpata usiku
Rais Samia: “Tusiwe shamba la bibi” - aonya wanaharakati wa nchi jirani kutoingilia masuala ya Tanzania
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa onyo kali kwa wanaharakati kutoka nchi jirani kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Tanzania, akisisitiza kuwa taifa hilo haliwezi kuwa “shamba la bibi” ambapo kila mtu anaingia na kufanya apendavyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa toleo jipya la Sera ya Mambo ya Nje ya mwaka 2001 (Toleo la 2024), Rais Samia amesema kuna mwenendo unaoibuka wa baadhi ya wanaharakati kuvuka mipaka na kuingilia masuala ya ndani ya nchi, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa.
“Tusuiwe shamba la bibi kwamba kila mtu anaweza kuja na kusema anachokitaka… Tumeanza kuona mtitiriko au mwenendo wa wanaharakati ndani ya region (kanda) yetu hii, kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku,” alisema Rais Samia.
Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya wakili mashuhuri wa Kenya na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Martha Karua, pamoja na Jaji Mkuu wa zamani Willy Mutunga na wanaharakati wengine wawili, kuzuiwa kuingia nchini Tanzania.
Walikuwa wamewasili kushuhudia kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu, ambayo imeendelea leo katika Mahakama ya Kisutu.
Kwa mujibu wa Karua, alifurushwa na kurudishwa Kenya kwa lengo la kumzuia kuhudhuria kesi hiyo. Mutunga na wenzake pia walielezwa kuwa walizuiwa katika uwanja wa ndege kabla ya kurejeshwa nchini kwao.
Hadi sasa, maafisa wa serikali ya Tanzania hawajatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo. Hata hivyo, kauli ya Rais Samia imeonekana kutoa mwelekeo wa msimamo wa serikali juu ya suala hilo.
"Sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku. Tusitoe nafasi, walishaharibu kwao, walishavuruga kwao, nchi iliyobaki haijaharibika watu wako na usalama na amani na utulivu ni hapa kwetu, aliongeza Rais Samia.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Korir Sing’oei, amesisitiza umuhimu wa kuheshimu haki za binadamu na ushirikiano wa kikanda.
Karua, anayefahamika kwa kusimama kidete kwa haki za binadamu, amewahi kumwakilisha kiongozi wa upinzani Uganda, Kizza Besigye, katika kesi kama hizi, na amekuwa mkosoaji mkubwa wa kile anachokiita kurudi nyuma kwa demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika hotuba yake, Rais Samia alisisitiza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na wasimamizi wa sera za nje, wanapaswa kuhakikisha kuwa hakuna “watovu wa adabu” kutoka mataifa mengine wanaovuka mipaka ya Tanzania na kuingilia masuala ya kitaifa.
“Niombe sana vyombo vya ulinzi na usalama na ninyi wasimamizi wa sera zetu za nje, msitoe nafasi kwa watovu wa adabu wa nchi nyingine kuja kuvuka hapa kwetu,” alisisitiza.
Kesi ya Tundu Lissu inaendelea huku mashinikizo kutoka ndani na nje ya nchi yakiongezeka, yakihusisha madai ya ukandamizaji wa haki za kiraia na kisiasa, jambo ambalo Serikali ya Tanzania inakanusha.
Vance: Tunatambua kwamba mazungumzo ya Urusi na Ukraine yamegonga mwamba
Chanzo cha picha, Reuters
Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance amesema mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine yamefikia "mkwamo mdogo" na maafisa wa Marekani wanafahamu hilo, Reuters inaripoti.
"Putin haonekani kujua jinsi ya kutoka kwenye vita hivi," Vance aliongeza.
Makamu huyo wa rais alikariri kuwa ikiwa Urusi haiko tayari kushiriki mazungumzo, Marekani itajiondoa kwenye mchakato huo, kwa kuwa hivi sio vita vyake.
Vance alitoa kauli hizi chini ya saa moja kabla ya simu iliyopangwa kati ya Donald Trump na Vladimir Putin.
Zelensky: Huko Istanbul, wajumbe wa Ukraine "walikataa majaribio ya vitisho vya Urusi"
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais Zelensky
Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov, ambaye aliongoza ujumbe huo katika mazungumzo ya moja kwa moja na Urusi mjini Istanbul, alizungumza kwa kina na Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky kuhusu mkutano huo.
"Ujumbe wa Ukraine uliweza kuweka mazungumzo ndani ya mfumo mzuri. Majaribio yote ya vitisho vya Urusi yalikataliwa," Zelensky aliandika katika telegram kufuatia mazungumzo na Umerov na mawaziri wengine.
Mkuu wa Ukraine hakutaja vitisho alivyokuwa akizungumzia.
Vyombo vya habari viliripoti kwamba mkuu wa wajumbe wa Urusi, Vladimir Medinsky, alidaiwa kuwaambia wajumbe wa Ukraine kwamba Urusi inaweza kupigana kwa muda mrefu sana na kwamba "pengine mtu anayeketi kwenye meza hii atapoteza wapendwa wake zaidi."
Zelensky alikariri kuwa Ukraine iko tayari kwa usitishaji mapigano bila masharti kwa siku 30 na mazungumzo ya moja kwa moja.
Rais wa Ukraine pia aliandika kwamba timu yake inashughulikia maelezo ya kubadilishana wafungwa wa vita, ambayo yalikubaliwa na wajumbe huko Istanbul.
Zelensky pia aliamuru kuundwa kwa kikundi cha mazungumzo cha kitaifa kilichopanuliwa.
Afrika Kusini kukata rufaa dhidi ya mchungaji wa Nigeria aliyefutiwa mashtaka ya ubakaji
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Timothy Omotoso
Bw Omotoso alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2017 alipojaribu kuondoka Afrika Kusini.
Miongoni mwa walalamishi wake ni mwanamke aliyesema alibakwa na mchungaji huyo alipokuwa na umri wa miaka 14.
Katika taarifa, waendesha mashtaka wa Afrika Kusini walikubali "hakuna sababu za kisheria za kumzuia" Bw Omotoso kuondoka nchini kufuatia kuachiliwa kwake.
Hata hivyo, ikiwa rufaa hiyo itaruhusiwa, mamlaka itaomba Bw Omotoso arejeshwe Afrika Kusini, taarifa hiyo iliongeza, ikiangazia "mkataba wa nchi mbili wa Nigeria wa kurejeshwa nchini Afrika Kusini".
Baada ya kuachiliwa huru mwezi Aprili, Bw Omotoso pia alikabiliwa na masuala ya uhamiaji, huku Idara ya Masuala ya Ndani ikidai mapema mwezi huu kwamba alikuwa nchini Afrika Kusini kinyume cha sheria.
Mnamo Jumapili, idara hiyo ilitoa taarifa ikisema kuwa Bw Omotoso ameainishwa kama "mtu asiyefaa", kumaanisha kuwa hataweza kurejea nchini kwa miaka mitano.
Shirika la utangazaji la umma la Afrika Kusini limeripoti kuwa mchungaji huyo aliondoka nchini kwa hiari.
Bw Omotoso anaongoza kanisa la Jesus Dominion International ambalo lina matawi nchini Uingereza, Nigeria, Ufaransa na Israel na pia katika maeneo mengi ya Afrika Kusini, kulingana na tovuti yake.
Kesi ya Bw Omotoso iliweka historia ya Afrika Kusini kuwa kesi ya kwanza ya ubakaji yenye hadhi ya juu kutangazwa moja kwa moja.
Waziri wa zamani wa haki nchini Kenya afurushwa Tanzania
Chanzo cha picha, Afp via Getty Images
Maelezo ya picha, Martha Karua alihojiwa kwa saa kadhaa na mamlaka ya Tanzania, kulingana na chama chake
Wakili mwandamizi nchini Kenya na
aliyekuwa wakati mmoja waziri wa haki na sheria Martha Karua amesema kwamba amefurushwa
nchini Tanzania na kurudishwa Kenya ili kumzuia kuhudhuria kesi inayomkabili
kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu.
Wenzake wawili walioambatana naye pia walifurushwa
nchini humo baada ya kuingia kutoka Kenya.
Aliyekuwa Jaji mkuu nchini Kenya Willy Mutunga
na mawakili - wapiganaji wa haki za kibinadamu ambao walisafiri hadi nchini humo wanasema kwamba walizuiwa katika uwanja wa ndege.
Maafisa wa Tanzania bado hawajatoa tamko
lolote kufikia sasa.
Lissu ambaye ndiye kiongozi wa chama cha upinzani
Chadema amewasilishwa mahakamani Jumatatu baada ya
Kushtakiwa na uhaini mwezi uliopita.
Afisa mkuu wa masuala ya kigeni nchini
Kenya Korir Sing’oei ameihimiza serikali ya Tanzania kumwachilia Mutunga na
wenzake.
Karua ni wakili anayeheshimika kwa haki za
kibinadamu na mkosoaji mkuu wa kile anchokiita kurudi nyuma kwa demokrasia Afrika Mashariki.
Amekuwa
akiwakilisha kiongozi wa upinzani Uganda Kizza Besigye ambaye alikuwa ametekwa nchini
Kenya mwaka uliopita na kurudishwa nchini mwao kuhudhuria mashtaka ya uhaini
yanayomkabili. Kama Lissu, amekanusha
mashtaka akisema yameshinikizwa kisiasa
Habari za hivi punde, Jeshi la Israel lawaambia Wapalestina kuondoka Khan Younis kabla ya mashambulizi
Chanzo cha picha, Reuters
Jeshi la Israel limewaambia wakazi wanaoishi katika miji ya Khan Younis, Bani Suheila na Abasan "kuondoka mara moja" kabla ya mashambulizi.
Msemaji wa Kiarabu wa IDF Avichay Adraee amesema kwenye X, kwamba IDF itaanzisha "shambulio ambalo halijawahi kutokea ili kuharibu uwezo wa mashirika ya kigaidi katika eneo hili".
"Lazima muhame mara moja magharibi hadi eneo la Mawasi," ameandika, akiongeza kwamba Khan Younis itachukuliwa kuwa "eneo hatari la vita".
Netanyahu asema Israel itadhibiti eneo lote la Gaza
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema katika video mpya iliyowekwa kwenye akaunti yake ya Telegram kwamba Israel itachukua udhibiti wa Gaza yote na kuzuia Hamas kupora misaada inayoingia katika eneo hilo.
"Tunahusika katika mapigano - makali na makubwa - na kuna maendeleo. Tutachukua udhibiti wa maeneo yote ya Ukanda, ndivyo tutafanya," anasema kwenye video.
Akihutubia ukosoaji wa vizuizi hivyo, Netanyahu anasema imekuwa muhimu tangu kuanza kwa vita huko Gaza kwa Israeli kuzuia njaa "kwa mtazamo wa vitendo na wa kidiplomasia". "Kwa ufupi, wengine hawatatuunga mkono; hatutaweza kukamilisha kazi ya ushindi," anasema.
"Kwa hivyo, tuliamua kutoa msaada mdogo wa kibinadamu wakati wa vita. Hatua hiyo inajiri baada ya serikali ya Israel kusema itaruhusu kiasi "cha msingi" cha chakula kuingia Gaza kufuatia mzingiro wa wiki 11.
Je, kizuizi cha Israeli ni nini?
Kama tumekuwa tukiripoti, Israel imetangaza kuwa itaruhusu "kiasi cha chakula" kuingia Gaza baada ya kuziba eneo hilo kwa wiki 11.
Tangu mwanzoni mwa mwezi Machi, Israel imezuia shehena zote za misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na chakula na vifaa vya matibabu, kuingia Gaza.
Uzuiaji huo umelaaniwa na viongozi mbalimbali na mashirika ya misaada, huku Israel ikikabiliwa na shinikizo la kutaka kuondoa.
Umoja wa Mataifa umeonya juu ya "hatari kubwa" ya njaa kwa Wapalestina milioni 2.1 wanaoishi Gaza.
Mashirika mengine ya misaada yamesema kizuizi hicho kinaweza kuwa uhalifu wa kivita na ni sawa na sera ya njaa.
Kenya yatishia kumkamata naibu rais aliyetimuliwa kwa 'uchochezi'
Chanzo cha picha, LIVE EVENT
Serikali ya Kenya imetishia kumkamata naibu wa rais wa zamani Rigathi Gachagua kwa madai ya kuhamasisha uchochezi katika kuzidisha uhasama kati yake na Rais William Ruto, gazeti la binafsi la Daily Nation limeripoti leo.
Mnamo tarehe 17 na 18 Mei, Naibu Rais Kithure Kindiki na Waziri wa Mambo ya Ndani Kipchumba Murkomen walimshutumu Gachagua kwa kuchochea chuki za kikabila kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 2027.
Murkomen alisema "kuna watu binafsi ambao wanadhani kuwa hawawezi kuguswa, kwamba hawawezi kukamatwa. Niseme wazi: chini ya uangalizi wetu, hatutakubali mtu yeyote ambaye anajaribu kuichoma nchi hii".
"Kuanzia leo, tutafuatilia mikutano yako yote, mchana na usiku."
Gachagua alikuwa ameonya mnamo Mei 16 kwamba "hakutakuwa na nchi hapa" mnamo 2027 ikiwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka "itajaribu kuvuruga" matokeo ya kura.
Amekana kuchochea ghasia, akijitaja kuwa "mtu mwenye amani zaidi nchini Kenya".
Polisi waliokuwa wamejihami vikali wameripotiwa kuzingira nyumba za Gachagua jana.
Gachagua ameapa kulipiza kisasi kushtakiwa kwake kwa kufanya kampeni ya kumnyima Ruto muhula wa pili.
Anamshutumu Ruto kwa kupanga kutimuliwa kwake na bunge mnamo Oktoba 2024 kwa madai ya ukiukaji mkubwa wa katiba.
Ulinzi mkali waimarishwa Tundu Lissu akifikishwa mahakamani Tanzania
Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amepandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mapema mwezi Aprili.
Lissu alikamatwa Aprili 9 baada ya kuitisha mageuzi ya uchaguzi na kuhimiza kususia uchaguzi ujao wa Oktoba.
Anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni, ikiwa ni pamoja na madai kwamba alichochea uasi na kuwashutumu polisi kwa utovu wa nidhamu katika uchaguzi.
Hapo awali mahakama ilijaribu kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao, lakini Lissu na timu yake ya wanasheria walipinga hili, wakitaja haja ya uwazi na taratibu zinazostahili.
Kukataa kwake kushiriki katika vikao vya mtandaoni kulisababisha kuonekana kwa ana kwa ana, kufuatia amri ya mahakama.
Uwepo mkubwa wa polisi haujawazuia wafuasi, ambao wengi wao wamekusanyika nje ya mahakama.
Ufuatiliaji wa yanayojiri kimataifa umeongezeka, hasa baada ya kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Martha Karua kunyimwa kuingia Tanzania kuhudhuria kikao hicho.
Karua, akiongoza kampeni ya haki za Afrika nzima, alilaani mamlaka za Tanzania kwa vitendo vyao na kutoa wito kwa vyombo vya kikanda kuiwajibisha serikali.
Pia kuna ripoti kwamba jaji mkuu mstaafu wa Kenya na rais wa Mahakama ya Juu Willy Mutunga amezuiliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Huku mwenendo wa kesi mahakamani ukiendelea, hali inaendelea kuwa tete, huku jumuiya ya kimataifa ikifuatilia kwa karibu maendeleo na dhamira ya serikali ya Tanzania katika kanuni za kidemokrasia zinazochunguzwa.
Lissu alipanda kizimbani akionekana mwenye furaha na bashasha , alipata nafasi ya kusalimia watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama chake.
Amelaani pia kuzuiwa kwa aliyekua Jaji mkuu wa Kenya Willy Mutunga uwanja wa ndege ili asiweze kuhudhuria kesi hiyo.
Hakuna mafanikio katika mazungumzo ya Israel na Hamas
Chanzo cha picha, Reuters
Chanzo kikuu cha Hamas kiliiambia BBC Jumapili jioni kwamba "hakuna mafanikio yoyote au maendeleo ambayo yamepatikana kufikia sasa katika mazungumzo yanayoendelea huko Doha kutokana na kuendelea kuasi Israel".
Chanzo hicho kilisema Hamas imeonesha nia ya kuwaachilia mateka wote wa Israel kwa awamu moja, "kwa sharti la kufikia makubaliano ya kina na ya kudumu ya kusitisha mapigano , jambo ambalo upande wa Israel unaendelea kukataa, kwani timu yao ya mazungumzo haina mamlaka ya kuamua juu ya masuala muhimu".
"Israel inazuia fursa yoyote ya kufikia makubaliano," chanzo hicho kiliongeza, kikisisitiza kuwa Hamas "inakataa mipango yoyote ya sehemu au ya muda".
Afisa huyo alikariri kuwa Hamas inataka makubaliano ya kina ambayo ni pamoja na kuachiliwa kwa mateka wote wanaoshikiliwa huko Gaza ili kubadilishana idadi iliyokubaliwa ya wafungwa wa Kipalestina, usitishaji vita wa kudumu, kujiondoa kabisa kwa Israel kutoka Ukanda wa Gaza, na kuingia kwa misaada ya kibinadamu.
Kulingana na chanzo hicho, "Israel inataka kuwarejesha mateka wake katika kundi moja au mbili ili kurudisha makubaliano ya muda".
Gary Lineker anatazamiwa kuondoka BBC huku tangazo likitarajiwa Jumatatu.
Uvumi unaeleza kuwa mtangazaji huyo mwenye umri wa miaka 64 atajiuzulu baada ya kutangaza mechi ya mwisho wikendi ijayo.
Lineker, aliyeorodheshwa kama mtangazaji wa BBC anayelipwa pesa nyingi zaidi, alitarajiwa kuwa mstari wa mbele katika matangazo ya BBC ya Kombe la FA msimu ujao na Kombe la Dunia mnamo 2026, licha ya hapo awali kutangaza kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu huu.
Wiki iliyopita aliomba radhi kwa kuchapisha mtandaoni mada iliyoonekana kuwadhalilisha Wayahudi.
Lineker alisema anajutia sana hilo, na kuongeza kwamba hatawahi kuchapisha kitu chochote cha chuki na kwamba alifuta chapisho mara tu alipojifunza juu ya ishara ya picha hiyo.
Wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa BBC Tim Davie alisema: "Sifa ya BBC inashikiliwa na kila mtu, na mtu anapokosea, inatugharimu."
Inafahamika kuwa wakuu wa BBC waliuchukulia msimamo wa Lineker kuwa haukubaliki.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza aliwahi kukosolewa kwa machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii siku za nyuma.
Israel yasema itaruhusu 'kiasi' cha chakula kuingia Gaza
Chanzo cha picha, Getty Images
Israel imetangaza kuwa itaruhusu "kiasi cha chakula" kuingia Gaza ili kuhakikisha kuwa "hakuna janga la njaa linaloendelea" baada ya kulizuia eneo hilo kwa wiki 10.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema kuwa hatua hiyo imetolewa kwa mapendekezo ya Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) na kwa kuzingatia haja ya kuunga mkono mashambulizi yake mapya ya kijeshi dhidi ya Hamas.
Tangazo hilo limekuja saa chache baada ya jeshi la Israel kusema kuwa limeanza "operesheni kubwa za ardhini" kote Gaza.
Israel imekuwa chini ya shinikizo kubwa la kuondoa kizuizi chake, wakati ambapo hakuna chakula, mafuta au dawa zilizoruhusiwa kuingia.
Mashirika ya misaada yametahadharisha kuhusu hatari ya njaa miongoni mwa wakazi milioni 2.1 wa Gaza, huku picha za video na zikiibuka za watoto waliodhoofika wanaokabiliwa na utapiamlo.
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alitoa wito kwa Israel kuruhusu "mara moja, kuanza tena misaada kwa ajili ya Gaza.
Taarifa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilisema kuwa Israel itaruhusu "kiasi cha chakula kuletwa kwa ajili ya wakazi" wa Gaza ili "kuhakikisha hakuna mzozo wa njaa unaoendelea" na kuongeza kuwa hali kama hiyo itahatarisha mashambulizi yake mapya, yaliyopewa jina la Operesheni Gideon's Chariot.
Mapema siku ya Jumapili, IDF ilianzisha mashambulizi katika maeneo ikiwa ni pamoja na hospitali kaskazini mwa Gaza.
Israel inasema inalenga kuwaachia huru mateka wanaoshikiliwa Gaza na kuwashinda Hamas.
Mashambulizi yalipiga mji wa kusini wa Khan Younis, pamoja na miji ya kaskazini mwa Gaza, ikiwa ni pamoja na Beit Lahia na kambi ya wakimbizi ya Jabalia, waokoaji walisema.
Takribani watu 67 wameuawa na 361 kujeruhiwa huko Gaza katika saa 24 zilizopita, wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas ilisema.
Joe Biden abainika kuwa na saratani 'kali' ya kibofu
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, 82, amegundulika kuwa
na saratani ya tezi dume ambayo imesambaa hadi kwenye mifupa yake, taarifa
kutoka ofisi yake ilisema Jumapili.
Biden, ambaye aliondoka madarakani Januari, alibaini Ijumaa
baada ya kuonana na daktari wiki iliyopita kutokana na dalili zilizojionesha
katika njia ya mkojo.
Saratani ni aina kali zaidi ya ugonjwa ambao umeainishwa
kama "kiwango cha juu" na seli za saratani zinaweza kuenea haraka,
kulingana na Shirika la Cancer Research UK.
Biden na familia yake wanasemekana wanatathimini aina ya matibabu.
Ofisi yake iliongeza kuwa saratani
hiyo haiathiriwi na homoni, kumaanisha kuwa inaweza kudhibitiwa.
Katika taarifa ya
Jumapili, ofisi ya Biden ilisema: "Siku
ya Ijumaa, aligunduliwa na saratani ya kibofu, yenye alama ya Gleason ya 9
( Daraja la 5) na metastasis kwenye mfupa.
Rais Donald Trump
aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba yeye na Mama wa
Rais Melania Trump "wanasikitika kusikia kuhusu kilichobainika hivi karibuni
wakati wa wa uchunguzi wa Joe Biden."
"Tunatuma
salamu zetu za heri kwa Jill na familia," alisema. "Tunamtakia Joe
ahueni ya haraka na yenye mafanikio."
Makamu wa Rais wa
zamani Kamala Harris, ambaye alihudumu chini ya Biden, aliandika kwenye X
kwamba yeye na mumewe Doug Emhoff wanaiweka familia ya Biden katika maombi yao.
Habari za asubuhi, karibu katika taarifa zetu za leo