Makorongo makubwa yanayomeza maeneo kote ulimwenguni

Sogeza ili kuendelea

Video ya droni ya mojawapo ya mashimo ya Buriticupu

Huu ulikuwa ni mtaa wenye shughuli nyingi huko Buriticupu, jiji lililo kaskazini-mashariki mwa Brazili.

Video ya droni ya mojawapo ya mashimo ya Buriticupu

Sasa ni shimo kubwa la kina cha 80m - jengo la ghorofa 20 linaweza kutoshea ndani yake.

Video ya droni ya mojawapo ya mashimo ya Buriticupu

Makorongo kama haya yanajulikana hapa kama "voçoroca" au "ardhi iliyopasuka" katika lugha asilia ya Kitupi-Guarani.

Video ya droni ya mojawapo ya mashimo ya Buriticupu

Hali hiyo ni matokeo ya mmomonyoko wa korongo,mojawapo ya aina kali zaidi za uharibifu wa udongo unaosababishwa na mvua na maji machafu.

Video ya droni ya mojawapo ya mashimo ya Buriticupu

Na inasonga mbele kwa kasi ya kutia wasiwasi, na kuharibu maelfu ya nyumba katika Amerika ya Kusini na Afrika.

Aliyekuwa afisa wa polisi José Ribamar Silveira nusura afariki alipoanguka kwenye shimo hili.

Alipotea alipokuwa akirudi nyumbani kutoka kwa karamu usiku mmoja Mei 2023.

Alipogeuza gari, mzee huyu wa miaka 79 alirejea nyuma na kuongeza kasi ya kurudi nyuma. Kulikuwa na giza, hakukuwa na ishara za onyo au vizuizi karibu na voçoroca, na kabla hajajua alitumbukia kwenye shimo kubwa akiwa ndani ya gari

"Gari lilipoteleza, ingawa lilikuwa likianguka haraka, nilimfikiria mwanangu mdogo," aliambia BBC.

Mtoto Gael alikuwa ametimiza umri wa miezi minne siku iliyopita. “Nilimwomba Mungu anilinde ili niweze kumlea mtoto wangu mdogo,” anasema Lt Silveira.

Alijigonga na kupoteza fahamu na kuzinduka chini ya korongo baada ya saa tatu. Baada ya operesheni ngumu ya uokoaji na miezi ya kupona, sasa anaweza kutembea bila magongo.

Picha  José Ribamar Silveira
José Silveira nusura afe alipoanguka kwenye bonde

Masaibu yake ni mfano wazi wa hatari zinazowakabili wakazi 70,000 wa Buriticupu.

Kadiri mabonde zaidi yanavyoonekana, kuna hofu kwamba jiji katika jimbo la Maranhão, lililo kwenye ukingo wa msitu wa mvua wa Amazon, linaweza kugawanywa mara mbili. Katika 350m juu ya kilele cha bahari, Buriticupu ina takriban makorongo 30 , na mawili makubwa yakitenganishwa na chini ya 1km.

"Ikiwa mamlaka haitathibiti haya , yatakutana na kuunda mto," anasema Edilea Dutra Pereira, mwanajiolojia na profesa katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Maranhão.

Makorongo yamekuwa sehemu ya historia ya kijiolojia ya Dunia kwa mamilioni ya miaka.

Lakini Prof Pereira na wataalamu wengine tuliozungumza nao walisema kuwa mabonde yaliyopo yanapanuka kwa kasi zaidi na wanahofia mapya yatafunguka kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yanaweza kufanya mvua kuwa nyingi zaidi.


             Picha ya setilaiti ya Buriticupu

Na katika maeneo ambayo miji hukua bila mipango sahihi na miundombinu ya kukabiliana na maji ya mvua, hatari huongezeka.

Brazil ndio nchi iliyoathiriwa zaidi Amerika ya Kusini, lakini Mexico, Colombia, Ecuador na Argentina pia zinakabiliwa na tatizo sawa. Na zaidi ya bara hili, nchi za Afrika, kama vile Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Nigeria - ambapo baadhi ya makorongo yana urefu wa zaidi ya kilomita 2 - pia zimeathirika.


            Ramani ya dunia inayoonyesha uwezekano wa kukumbwa na mmomonyoko wa udongo

" Aina hii ya mmomonyoko wa udongo inatishia ardhi yenye rutuba ya kilimo katika baadhi ya maeneo ya Uchina, Marekani na Ulaya pia. "

“Hatari sana” kuishi hapa

Hakuna takwimu rasmi za vifo vinavyotokana na mafuriko, lakini mamlaka huko Buriticupu wanasema makorongo yamemeza angalau nyumba 50 na baadhi ya wakazi wamelazimika kuyaacha makazi yao, na kuacha vitongoji vikiwa tupu.

Nyumba ya Marisa Cardoso Freire iko kwenye ukingo wa shimo na iliitwa "hatari kubwa" na Jeshi la Ulinzi la Raia mnamo Mei 2023.

"Pamoja na familia nyingine 100, ilimbidi aondoke nyumbani kwake na kuhamia sehemu nyingine ya Buriticupu. "

City Hall iliahidi kulipia kodi ya nyumba mpya kwa watu waliohamishwa makazi yao, lakini Marisa anasema manispaa haijalipa kodi kwa wakati na ametishiwa kufukuzwa.

Tulipowasiliana na Buriticupu City Hall kuuliza kinachoendelea, ilishindwa kujibu.

Picha ya Marisa Cardoso Freire
Marisa anapata ugumu kukubali kwamba amepoteza nyumba yake

Katika nyumba ya zamani ya Marisa, mbwa wawili wa familia hiyo walianguka kwenye korongo na kufa.

Kisha siku moja alikuwa akijaribu kumrejesha ndani ya nyumba mtoto wake wa kiume Enzo, mwenye umri wa miaka 10, ambaye ana usonji, na akapaza sauti yake.

Enzo alikasirika na kukimbilia ukingo wa korongo. “Ukinifokea tena, nitajitupa shimoni,” alitisha.

“Hapo ndipo nilipomwambia mume wangu kwamba hatuwezi kukaa hapa tena, ni hatari sana”
Marisa Cardoso

Labda hatawahi kuishi katika nyumba aliyoijenga.

"Nilipoondoka, moyo wangu uliumia kwa sababu ni kitu ambacho tulipigana sana kukipata."

Je ilifikiaje hatua hii?

Ukataji miti unachukua sehemu kubwa katika aina hii ya uharibifu wa udongo.

" Buriticupu sasa ni sehemu kame, yenye mawe lakini ni sehemu ya msitu wa Amazon na iliwahi kufunikwa na miti, kama vile mierezi, nzige wa India Magharibi na ipê."

Katika miaka ya 1990 sekta ya mbao ilikuwa imeshamiri hapa. Kulikuwa na zaidi ya viwanda 50 vya mbao vilivyofanya kazi kwa saa 24 kwa siku. Miaka 20 baadaye, mimea mingi ya asili ya jiji hilo ilikuwa imetoweka.

"Suala la mimea ni muhimu, kwa sababu wakati wa tukio la mvua, hupunguza athari za matone ya mvua"
Edilea Dutra Pereira mwanajiolojia na profesa katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Maranhão
Katuni inayoonyesha mvua katika eneo lililokatwa miti

Wakati hakuna mimea au miti ya kutosha kunyonya mvua…

mchoro wa maji yakiwa juu

matone huondoa chembe za udongo na maji hujikusanya juu .

Mchoro  unaoonyesha mto  ukiundwa

Mito hujiunda na kuondoa udongo

Mchoro ukionyesha mitaro ikifunguka

Mitaro na mashimo inaweza kujitengeza

Mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kuzidisha mchakato katika maeneo yanayokumbwa na mmomonyoko wa udongo kwani yanaweza kusababisha mvua nyingi zaidi.

Buriticupu inakabiliwa na dhoruba kali zaidi kuliko ilivyokuwa, kulingana na Juarez Mota Pinheiro, mtaalamu wa hali ya hewa katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha Maranhão.

Katika miezi ya kwanza ya 2023, jimbo la Maranhão lilikabiliwa na mafuriko mabaya zaidi katika historia yake. Zaidi ya manispaa 60 ziliingia katika hali ya hatari, maelfu ya watu waliachwa bila makazi na kulikuwa na vifo vya watu kadhaa.

Bonde la Buriticupu
Bonde hili ni mojawapo ya takriban 30 huko Buriticupu

" “Kiwango cha mvua kinatabiriwa kuongezeka kwa 10% hadi 15% [duniani kote kufikia mwisho wa karne hii]. Hiyo inaweza isionekane kama kubwa lakini ikiwa una vipindi vingi zaidi vya mvua kali, mienendo ya mmomonyoko wa ardhi inabadilika," anasema Matthias Vanmaercke, kutoka Chuo Kikuu cha KU Leuven nchini Ubelgiji."

Yeye na mwenzake Jean Poesen walichanganua data kutoka kwa zaidi ya makorongo 700 duniani kote na kugundua kwamba ikiwa mvua kali itaongezeka kwa kiasi hicho, inaweza kuongeza maradufu (au hata mara tatu katika hali mbaya zaidi) hatari za mmomonyoko wa udongo.

"Utakuwa na wakati mgumu kupata mwanasayansi mzuri ambaye hatakubaliana na ukweli kwamba mabadiliko ya hali ya hewa pengine yatafanya hali hii kuwa mbaya zaidi," Prof Vanmaercke anasema.

Hofu ya mvua

Hali hii inaathiri watu kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na mamilioni barani Afrika.

" Mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa, una mamia ya makorongo ya mijini - mojawapo ikiwa na urefu wa kilomita 2. Kuna zaidi ya kilomita 165 za korongo katika jiji hilo, ambalo ni makazi ya watu milioni 12. "

Picha ya mtaro wa Kinshasa
Barabara kuu katika wilaya ya Mont Ngafula huko Kinshasa iliporomoka na kuwa shimo mnamo 2021.

Katika usiku mmoja tu wa mvua kubwa huko Kinshasa mnamo Desemba 2022, watu 60 walikufa wakati nyumba zao zilipoanguka kwenye korongo.

Alexandre Kadada alikuwepo.

"Ilitokea ndani ya muda wa dakika 30 au 40.Shimo lilianza kufunguka na nyumba zote kutoweka. Mtaa mzima ulikuwa hautambuliki,” anasema.

“Vitu vyangu, nyumba yangu, kila kitu kilikuwa kimeisha. Niliokoa watoto wangu na mke wangu tu.” ”

Jirani ya Bw Kadada na watoto wake wanne walikuwa miongoni mwa waathiriwa. Mume wa mwanamke huyo aliachwa na ulemavu

Picha ya  Kadada
Alexandre Kadada sasa ni rais wa kundi linalowakilisha waathiriwa wa mkasa huo

Watoto wa Bw Kadada sasa wanaogopa sana kutokana na hali mbaya ya hewa.

“Mvua ndiyo iliyovuruga kila kitu. Mvua hiyo ilileta kifo na hali ya kukata tamaa,” anasema.

"Kwa kweli tunaiona kuwa hatari mpya ya jiografia ya Anthropocene," anasema Prof Vanmaercke. Anthropocene ni neno linalotumiwa na baadhi ya wanasayansi kuelezea siku za hivi karibuni, wakati shughuli za binadamu zimeathiri sana sayari.

"Idadi ya watu wa Kinshasa inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 20 ifikapo 2030 na milioni 35 ifikapo 2050, na kuwa jiji kubwa zaidi barani Afrika, kulingana na Benki ya Dunia. "

Ukuaji wa miji usiodhibitiwa unaweza kuhusisha kukata miti - kizuizi cha asili cha mmomonyoko wa ardhi - na umiliki haramu wa maeneo yasiokuwa dhabiti.

Kitafutaji cha Kinshasa na picha ya satleite ya 2004 na 2023

Huko Buriticupu, watu pia wanaogopa mvua.

"Kuna muda ambapo ardhi yenye ukubwa wa nyumba huporomoka. Hutoa kelele kali, hutikisa kila kitu. Kisha watu hulia. Huzuni inayosababishwa ni ya kutisha," asema João Batista mwenye umri wa miaka 52, fundi ambaye anamiliki karakana kwenye ukingo wa shimo kubwa.

"Nimepoteza 40% ya wateja wangu. Wengi wanaogopa kupita," anasema. Lakini anakataa kuondoka.

Shimo nyuma ya karakana yake hapo zamani ilikuwa uwanja wa michezo wa watoto, anasema, lakini korongo lilimeza kila kitu.

Picha ya  João Batista
Majengo mengine karibu na karakana ya Batista yameachwa

Aliamua kupanda mianzi ili kujaribu kupunguza mmomonyoko huo. Lakini kutokana na ukubwa wa tatizo, Buriticupu inahitaji suluhu kubwa zaidi.

Nini kinaweza kufanywa?

'Lakini kwa uhandisi na uwekezaji ufaao, "yote haya yanaweza kusitishwa", anasema Prof Vanmaercke."

Ili kukomesha mmomonyoko wa udongo, miji inabidi kujenga mifumo ifaayo ya mifereji ya maji ili kudhibiti mtiririko wa maji ya mvua na maji taka, anaeleza Prof Poesen, ili kuelekeza maji mbali na maeneo hatarishi kwa makorongo.


            Picha ya setilaiti ya shimo la Buriticupu mwaka wa 2014 na 2022

Lakini miradi hii inagharimu pesa katika miji ambayo bajeti ni adimu

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma katika jimbo la Maranhão inachukua hatua za kisheria dhidi ya mji wa Buriticupu, ikisema kuwa haijatekeleza mipango ambayo ilikuwa imekubaliwa.

Meya wa Buriticupu João Teixeira da Silva alikataa kutoa maoni yake kuhusu kesi hiyo lakini anasema ameomba msaada wa kifedha kutoka kwa serikali ya shirikisho kufadhili kazi ya kugeuza mkondo wa maji ya mvua.

Serikali ya kitaifa ilituambia kuwa inazingatia iwapo itaachilia Reals za Brazil milioni 300 ($60m; £47m) kwa Buriticupu. Iliongeza kuwa tayari imetoa real 629,000 ($125,000; £100,000) kujenga mfereji wa maji na kukarabati barabara za mitaa na kubomoa nyumba 89.

" Wizaŕa ya Mazingiŕa inasema kuwa ina pŕogŕamu ya kutekeleza ""mifumo dhabiti katika miji"", lakini kwa sasa haifanyi lolote Buriticupu. "

"Hizi ni kazi ngumu, kazi zinazohitaji rasilimali kubwa," anasema meya. "Tunachohitaji ni kuwajibika , katika ngazi ya manispaa, serikali na shirikisho."

Lakini João Batista anafahamu kwamba ikiwa shimo nyuma ya jengo lake la kazi litakua, huenda akalazimika kuhama

“Hii ni hali ya asili inayotuambia kwamba tusipoitunza sayari yetu, itaharibiwa. Ikiwa mvua inaendelea kunyesha hivi, basi tuko mikononi mwa Mungu kwa sababu hakuna tunachoweza kufanya.”