Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

time_stated_uk

  1. Tunakomea hapo. Kwaheri.

  2. Kenya: Miili zaidi yaopolewa baada ya lori kusombwa na mafuriko ya mto Kwa Muswii

    Miili mingine mitatu imeopolewa kutoka kwa Mto Kwa Muswii katika Kaunti ya Makueni Mashariki mwa Kenya baada ya lori lililokuwa likijaribu kuvuka mto uliofurika kusombwa na maji ya mafuriko.

    Hii inafanya idadi ya vifo kutokana na tukio hilo kufikia 8, huku ripoti zikionyesha kuwa watu 10 zaidi hawajulikani waliko. Watu wengine 14 wameokolewa na kutibiwa.

    Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya ndani watu hao walisombwa na mafuriko wakati wakielekea nyumbani kutoka soko la Yaitha.

    Walioshuhudia tukio hilo wanasema Lori la kwanza lilifanikwa kuwavusha watu salama lakini Lori la pili lilishindwa na kusombwa na maji hayo.

    Wakazi hao wamesema kuwa walikuwa wamepiga kambi kwenye kingo za mto huo tangu asubuhi, wakisubiri maji yapungue ili wavuke lakini maji hayo kadri muda ulivyozidi yalizidi kuongezeka.

    Mvua kubwa inayonyesha kwa sasa katika maeneo tofauti nchini Kenya imewaathiri mamia ya watu awalioachwa bila makao.

    View more on twitter
  3. Thomas Tuchel asema hatashawishiwa na mashabiki kusalia Bayern Munich

    Thomas Tuchel

    Mkufunzi wa Bayern Munich Thomas Tuchel anasema hatakubali "kushawishiwa" na ombi la kumtaka abaki katika klabu hiyo.

    Ombi la kumtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 kusalia Allianz Arena limetiwa saini na zaidi ya mashabiki 12,000.

    Bayern ilitangaza mwezi Februari kwamba Tuchel ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika.

    "Ingawa mada hii ni nzuri kwangu wakati [mashabiki] wanataka ubaki, sio jambo la kipaumbele," alisema Tuchel.

    Ralf Rangnick, kocha wa zamani wa Manchester United, amefanya mazungumzo na Bayern kuhusu kuchukua mikoba ya Tuchel msimu huu wa joto.

    Tuchel aliongeza kuwa ni jukumu la klabu kumteua mrithi wake na ameziba masiko ili "kutosikia" uvumi wowote.

  4. Liverpool wafikia mkataba wa £9.4m na kocha wa Feyenoord Arne Slot

    Kocha wa Feyenoord Arne Slot
    Image caption: Kocha wa Feyenoord Arne Slot

    Arne Slot anatazamiwa kuwa kocha mpya wa Liverpool baada ya kufikia makubaliano ya mkataba wa thamani ya hadi pauni milioni 9.4 na Feyenoord.

    Mholanzi huyo yuko tayari kurithi mikoba ya Jurgen Klopp, ambaye alitangaza Januari kwamba ataondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2023-24.

    The Reds sasa watachukua hatua kukubaliana kandarasi na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 45 kabla ya kuteuliwa rasmi.

    Liverpool wamekubali kulipa Feyenoord £7.7m (euro 9m) pamoja na uwezekano wa £1.7m (euro 2m) kama nyongeza.

    Slot iliiongoza Feyenoord kutwaa taji la Eredivisie 2022-23, ambao wameshinda Kombe la Uholanzi msimu huu na wanatarajiwa kumaliza nafasi ya pili kwenye ligi yao.

    Inaaminika kuwa aina ya ushambuliaji ya timu za Slot, haiba yake na uwezo wake wa kuwakuza wachezaji ni mambo muhimu yaliyomfanya kuwa chaguo la Liverpool kwa kazi hiyo.

  5. Pentagon kupeleka 'haraka' mfumo wa makombora ya Patriot nchini Ukraine

    Mfumo wa makombora wa Patriot unaotumiwa na Ujerumani
    Image caption: Mfumo wa makombora wa Patriot unaotumiwa na Ujerumani

    Pentagon inasema "itaharakisha" kupeleka makombora ya ulinzi wa anga ya Patriot na risasi za kivita nchini Ukraine kama sehemu ya kifurushi chake kipya cha msaada wa kijeshi.

    Hata hivyo mifumo ya Patriot ya kurusha makombora haitatumwa, Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin alisema.

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema Patriot inahitajika "haraka" kukabiliana na tishio la anga la Urusi na "wanapaswa kuokoa maisha" haraka iwezekanavyo.

    Siku ya Jumamosi, Ukraine ilisema Urusi imefanya shambulio lingine kubwa la anga.

    Mamlaka ya Kharkiv ilisema hospitali iliharibiwa.

    Miundo mbinu ya nishati katika mikoa mitatu ilishambuliwa, Waziri wa Nishati Ujerumani Galushchenko alisema.

    Urusi ilishambulia kwa makombora ya meli aina ya S-300 kutoka ardhini hadi angani na makombora ya balestiki ya Iskander, Ukraine ilisema, ikiongeza kuwa 21 yaliangushwa kwa kutumia ndege, mifumo ya ulinzi wa anga.

    Ukraine ilidai kushambulia vinu viwili vya mafuta vya Urusi upande wa pili wa mpaka.

    Picha kutoka kwa moja katika eneo la Urusi la Krasnodar ilionekana kusababisha mlipuko mkubwa, ingawa viongozi wa eneo hilo walikanusha uharibifu mkubwa.

    Mamlaka ya Urusi ilisema siku ya Jumamosi kuwa iliangusha ndege 68 zisizo na rubani za Ukraine katika eneo la Urusi.

    Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi?

    Vita vya Ukraine: Marekani yatuma kwa siri makombora ya masafa marefu kusaidia Kyiv

  6. Nyota wa TikTok wa Iraq Om Fahad auawa mjini Baghdad

    Om Fahad
    Image caption: Om Fahad alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela mwaka jana kwa kushiriki video zake katika mitandao ya kijamii (picha ya maktaba)

    Mshawishi wa mitandao ya kijamii nchini Iraq Om Fahad ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake mjini Baghdad, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

    Shambulio hilo lilitokea katika kitongoji cha mji mkuu wa Zayne mashariki mwa mji huo siku ya Ijumaa.

    Wizara ya mambo ya ndani ya Iraq ilithibitisha katika taarifa kwamba "mwanamke maarufu katikae mitandao ya kijamii" ameuawa na "washambuliaji wasiojulikana".

    Iliongeza kuwa "timu maalum" imeundwa kuchunguza mazingira ya kifo chake.

    Fahad, ambaye jina lake halisi ni Ghufran Sawadi, aliripotiwa kupigwa risasi ndani ya gari lake na mtu aliyekuwa na bunduki akiendesha pikipiki.

    Chanzo cha usalama cha Iraq kililiambia shirika la habari la AFP kwamba mshambuliaji huyo alionekana kujifanya kuwa analeta chakula.

    Shirika la habari la Al Hurra linalomilikiwa na Marekani, wakati huo huo, liliripoti kuwa mwanamke mwingine alijeruhiwa katika shambulio hilo.

    Fahad alijulikana sana kwenye TikTok kwa kushiriki video zake akicheza hadi muziki wa pop akiwa amevalia mavazi ya kubana - na kujipatia maelfu ya wafuasi.

    Alihukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani kwa kushiriki video ambazo mahakama iliamua zinadhoofisha "maadili ya umma".

  7. Meli ya mafuta yaharibiwa katika shambulio la kombora la Houthi

    Wahouth wamekuwa wakifanya mashambulizi kwenye meli kwa zaidi ya miezi mitano (picha ya maktaba)
    Image caption: Wahouthi wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya meli katika bahari ya Shamu kwa zaidi ya miezi mitano (picha ya maktaba)

    Meli ya mafuta ghafi imeharibiwa katika shambulio la kombora katika pwani ya Yemen -shambulio wa hivi punde zaidi kufanywa na waasi wa kihouthi.

    Tukio hilo lilitokea maili 15 kusini-magharibi mwa mji wa Mocha nchini Yemen.

    Shirika la usalama wa baharini la Uingereza UKMTO liliripoti kuwa meli hiyo iliyokuwa na bendera ya Panama ilipigwa mara mbili na imeharibiwa.

    Hakuna majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa na tukio hilo linachunguzwa.

    Kulingana na UKMTO, shambulio la kwanza la kombora lilisababisha mlipuko karibu na meli na kuhisiwa na waliokuwa ndani. Ya pili - iliyofikiriwa kuhusisha makombora mawili - iliwasiliana.

    Kampuni ya kimataifa ya kudhibiti hatari ya Ambrey ilisema kuwa makombora matatu yameonekana.

    Imeongeza kuwa makombora ya balistiki yameripotiwa kurushwa kutoka kwa jimbo la kusini-magharibi la Taiz nchini Yemen.

    Waasi wa Houthi wamedai kutekeleza shambulio hilo.

    Msemaji wa jeshi la kundi hilo, Yahya Sarea, alisema katika hotuba yake Jumamosi kwamba meli ya "Uingereza" iitwayo Andromeda Star ilikuwa ikilengwa, katika hali iliyosababisha "shambulio la moja kwa moja".

    Kamandi Kuu ya Marekani ilithibitisha kwamba Andromeda Star ndiyo meli inayozungumziwa, kwamba imepata uharibifu mdogo na inaendelea na safari yake.

    Ambrey aliripoti kwamba meli ya mafuta iliyoshambuliwa ilikuwa inamilikiwa na Uingereza hadi Novemba 2023.

    Mmiliki wake wa sasa amesajiliwa Ushelisheli na meli hiyo imekuwa akijishughulisha na biashara inayohusishwa na Urusi - ikisafiri kutoka mjini Primorsk nchini Urusi hadi Vadinar, katika jimbo la India la Gujarat, wakati shambulio hilo lilipotokea.

    Ambrey alishauri wamiliki wa meli na waendeshaji kufanya "ukaguzi wa kina wa uhusiano" kabla ya kuvuka eneo hilo "kwani Wahouthi wanaweza kuhusisha meli na mmiliki wa kizamani".

    Soma:

    Wahouthi: Je, waasi wa Yemen wana nguvu kiasi gani?

    Je, Wahouthi wanaitumbukiza Marekani na washirika wake kwenye vita wasivyoweza kushinda?

  8. Natumai hujambo.