Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu

time_stated_uk

  1. Na kufikia hapo ndio tumekamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo. Kwaheri.

  2. Mahakama ya Ghana haitamlazimisha rais kutia saini mswada dhidi ya LGBT

    h
    Image caption: Mswada dhidi ya LGBT unakabiliwa na changamoto mbili za Mahakama ya Juu zinazousubiri

    Mahakama Kuu ya Ghana imetupilia mbali ombi la kumshurutisha rais wa nchi hiyo kusaini mswada dhidi ya wapenzi wa jinsia moja uliopitishwa bungeni mwezi Februari.

    Ofisi ya Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ilisema mwezi uliopita kwamba haitakubali muswada huo hadi Mahakama ya Juu itakapoamua juu ya katiba yake, na kusababisha mzozo wa kisiasa katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Maryam Abdalla na amaelezo zaidi.

    Jaji Ellen Lordina Serwaa Mireku aliunga mkono hoja ya rais, na kuamua kwamba haiwezekani kumlazimisha Rais Akufo-Addo kutia saini mswada huo ambao bado unakabiliwa na mapingamizi mawili kutoka kwa Mahakama ya Juu.

    Mapingamizi hayo yaliwasilishwa na raia wawili wa Ghana - mwanaharakati Amanda Odoi na wakili Richard Dela Sky. Wawili hao wanalenga kuzuia mswada huo. Wanatafuta kuzuia mswada wa kupinga mapenzi ya jinsi moja kuwa sheria.

    Mswada huo unaweka kifungo cha hadi miaka mitatu jela kwa yeyote anayejitambulisha kama ni mshiriki wa mahusiano ya jinsi moja na miaka mitano jela kwa kutangaza au kuunga mkono shughuli za mrengo huo.

    Mswada huo umezua mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini Ghana.

    Waziri wa fedha wa Ghana ameonya kwamba nchi hiyo inaweza kupoteza ufadhili wa thamani ya dola bilioni 3.8 kutoka Benki ya Dunia endapo mswada huo utapitishwa kuwa sheria.

    Hatahivyo, wabunge kadhaa na makundi mbali mbali ya rais wanamshinikiza rais Akufo-Addo kupitisha muswada huo.

  3. Maafisa wanne wa Marekani walipigwa risasi, wanne wakauawa, wakati wakitumikia waranti ya kukamatwa kwa mhalifu

    .

    Maafisa wanne wa polisi wa Marekani wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine wanne kujeruhiwa walipokuwa wakitumikia waranti ya kukamatwa huko Charlotte, North Carolina.

    Mshukiwa wa shambulizi alipatikana amefariki eneo la mbele la nyumba iliyo na vizuizi baada ya makabiliano yaliyochukua masaa matatu, polisi walisema.

    Watu wengine wawili wa karibu walichukuliwa kuhojiwa, mamlaka iliongeza.

    Ni moja ya shambulio baya zaidi dhidi ya watekelezaji sheria wa Marekani katika miaka ya hivi karibuni.

    Maafisa hao walikuwa sehemu ya kikosi kazi kinachoongozwa na Huduma ya Wanajeshi wa Marekani. Hati waliyokuwa wakijaribu kuitekeleza siku ya Jumatatu ilikuwa dhidi ya mhalifu anayetafutwa kwa kumiliki bunduki kinyume cha sheria.

    Milio ya risasi ilisikika kwenye barabara ya mijini walipokuwa katika shughuli hiyo.

    Maafisa hao walimfyatulia risasi mshambulizi kisha risasi zaidi zikafyatuliwa kutoka ndani ya nyumba hiyo, Mkuu wa Polisi wa Charlotte-Mecklenburg Johnny Jennings aliambia mkutano wa wanahabari. Bunduki yenye nguvu kubwa ilipatikana ndani ya nyumba hiyo, aliongeza.

    "Leo tumepoteza baadhi ya mashujaa ambao walikuwa wakijaribu tu kuhakikisha jamii yetu iko salama," mkuu wa polisi aliwaambia wanahabari.

    Alisema hilo lilikuwa shambulio baya zaidi dhidi ya maafisa wa polisi ambao anaweza kukumbuka katika miaka yake 30 kwenye kikosi hicho.

  4. Mali yamuua kamanda wa IS anayelaumiwa kwa vifo vya Marekani - TV ya serikali

    .

    Televisheni ya taifa nchini Mali inasema kamanda mkuu wa Islamic State ambaye kulitangazwa zawadi ya dola milioni 5 (£4m) za Marekani kwa yeyote atakayetoa taarifa zake, ameuawa na wanajeshi wakiwemo kutoka Mali, Burkina Faso na Niger.

    Abu Huzeifa alikuwa amehusishwa na uvamizi kadhaa wa hali ya juu katika eneo la Sahel.

    Hii ni pamoja na shambulio la 2017 ambalo liliua wanajeshi wanne wa Marekani na wanajeshi kadhaa kutoka Niger.

    Mali, Burkina Faso na Niger zote zimekumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wapiganaji wa kijihadi.

    Nchi zote tatu ziko chini ya utawala wa kijeshi na zimekuwa zikiendeleza uhusiano wa karibu na Urusi huku zikikata uhusiano na washirika wa Magharibi ikiwemo Marekani.

    Wamekuwa wakikaribisha msaada wa kijeshi wa Urusi huku wakiwalazimisha wanajeshi kutoka nchi nyingine kuondoka.

    Abu Huzeifa, ambaye pia alijulikana kama Higgo, alielezewa na ripoti hiyo kwenye Televisheni ya Taifa ya Mali kama raia wa Morocco na kamanda katika jimbo linalojiita la IS la Sahel.

    Ilisema aliuawa siku ya Jumapili katika operesheni kwenye mji wa kaskazini wa Indelimane eneo la Menaka, na kueleza kuwa ni "ushindi dhidi ya balaa la uovu".

    Serikali ya Marekani ilisema kuwa Hufeiza alikuwa anatafutwa kuhusiana na shambulizi dhidi ya kikosi maalum cha Marekani nchini Niger mwaka 2017 ambalo lilisababisha vifo vya wanajeshi wanne wa Marekani na wanne wa Niger.

    IS baadaye ilidai kuhusika na shambulio hilo.

    Kilitokea nini kwa IS mwaka 2023?

  5. Netanyahu aapa kutekeleza shambulizi la Rafah

    .

    Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema Israel itaanzisha uvamizi katika mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah bila kujali mazungumzo ya mapatano na Hamas.

    Hatua hii inawadia huku kukiwa na majaribio yanayoendelea ya kujaribu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka.

    Lakini katika mkutano wa jamaa za mateka, Bw Netanyahu alisema atavamia "kwa au bila" makubaliano.

    Maoni yake yanafuatia maonyo mapya ya Marekani dhidi ya uvamizi wa Rafah isipokuwa raia wamelindwa ipasavyo.

    Katika mazungumzo ya simu na Bw Netanyahu siku ya Jumapili, Rais wa Marekani Joe Biden "alisisitiza msimamo wake wazi" kuhusu Rafah, taarifa ya Ikulu ya White House ilisema. Bwana Biden hapo awali alielezea uvamizi wa Rafah kama "kuvuka mpaka".

    Zaidi ya nusu ya wakazi wa Gaza milioni 2.5 wako Rafah, wakiwa wamekimbilia huko kukwepa mapigano katika maeneo mengine ya eneo hilo. Hali katika jiji lenye msongamano mkubwa wa watu ni mbaya, na watu waliohamishwa huko wamezungumza juu ya ukosefu wa chakula, maji na dawa.

    Rais wa Palestina mwenye makao yake Ukingo wa Magharibi Mahmoud Abbas alisema Jumatatu kwamba uvamizi wa Rafah utakuwa "janga kubwa zaidi katika historia ya watu wa Palestina".

    Pia unaweza kusoma:

    Je, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alikosa fursa ya kuwazuia Hamas?

  6. Mafuriko Kenya: Baraza la Mawaziri lawaamuru Wakenya wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko kuhama ndani ya saa 48

    Yusuf Jumah

    BBC Swahili

    .

    Rais wa Kenya William Ruto ametangaza kwamba raia wanaoishi katika maeneo yaliyo katika hatari ya mafuriko au maporomoko ya ardhi kote nchini watatakiwa kuhama kuanzia Jumatano.

    Bw Ruto alikuwa akizungumza katika eneo la Mai Mahiu, kaskazini mwa Nairobi ambapo wimbi la maji kutoka kwenye bwawa lililofurika lilisomba nyumba na watu Jumapili usiku.

    Rais alisema serikali imepanga maeneo yote tete ambayo yanaweza kukabiliwa na hatari hizo na lazima watu waanze kuhama mara moja kwa sababu kuna utabiri wa mvua kuendelea kunyesha . Huu sio "wakati wa kukisia," alisema, "uwezekano wa mafuriko na watu kupoteza maisha ni kweli."

    Ruto Jumanne asubuhi aliitisha kikao Maalum cha Baraza la Mawaziri kujadili hatua za ziada zinazohitajika ili kupunguza athari za mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha maafa na kuharibu mali nchini humo.

    Baraza la Mawaziri lilipokea na kuzingatia ripoti ya utabiri wa hali ya hewa kutoka Idara ya Hali ya Hewa, ikionyesha kwamba mvua zinazoendelea kunyesha zitazidi kunyesha kwa muda mrefu, na kuonya kwamba hali inaweza kuwa mbayakatika siku zijazo.

    Liliagiza kwamba wananchi wanaoishi ndani ya maeneo haya hatari wanatakiwa kuhama ndani ya saa 48.

    Haya ni pamoja na maeneo karibu na mabwawa na hifadhi nyingine za maji katika ardhi ya umma au ya kibinafsi, maeneo yanayokumbwa na maporomoko ya matope na maporomoko ya ardhi na maeneo ya kando ya mito na njia nyingine za maji nchini kote.

    Wananchi wote walioathiriwa na agizo hili wataarifiwa kufikia mwisho wa siku ya Jumatano, Mei 1, 2024.

    Serikali imeweka mikakati ya kuwasaidia watu kuhama maeneo hayo hadi kwenda makazi ya muda kwa wale ambao wataathiriwa na agizo hili endapo watahitaji msaada.

    Wakati serikali ikihimiza watu kuhamakwa hiari, wale wote watakaobaki ndani ya maeneo yaliyoathiriwa na agizo hilo watahamishwa kwa nguvu kwa ajili ya usalama wao.

    Mafuriko nchini Kenya yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 170 hadi sasa huku wengine maelfu wakiachwa bila makaazi na mkasa wa hivi punde katika eneo la Mai Mahiu ukisababisha vifo vya zaidi ya watu 50. Shughuli ya uokoaji inaendelea katika eneo hilo yapata kilomita 60 kutoka mji mkuu, Nairobi.

    Soma zaidi:

    Kenya: 76 hawajulikani waliko baada ya mafuriko kusomba nyumba zao

    Mafuriko Kenya: Jinsi mafuriko yanavyofichua hali mbaya ya mazingira ya Nairobi

  7. Waandamanaji Columbia wakalia jengo la chuo kikuu

    .

    Waandamanaji wanaounga mkono Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia wamekalia jengo la chuo hicho kama sehemu ya maandamano yao kuhusu vita huko Gaza.

    Makumi ya wanaharakati walikalia jengo la Hamilton mapema Jumanne.

    Sio Chuo kikuu wala polisi hakuna ambaye ametoa maoni yoyote kufikia sasa.

    Columbia hapo awali ilianza kuwafukuza wanafunzi waliopiga kambi kwa wiki mbili ambao walikaidi makataa ya kutawanyika kwa tarehe iliyowekwa.

    Wanafunzi walionywa kuchukuliwa hatua za kinidhamu iwapo wangekosa kuondoka ifikapo saa 14:00 EST (18:00 GMT) siku ya Jumatatu.

    Lakini ukomo wa muda huo ulipopita wanafunzi wengi wakiwa wamekusanyika kwenye eneo hilo.

    Mojawapo ya makundi makuu ya waandamanaji, iliapa kukaidi agizo hilo katika ujumbe kwenye mtandao wa X, na kuwataka wanaharakati "kulinda jengo" hilo.

  8. Kenya: 76 hawajulikani waliko baada ya mafuriko kusomba nyumba zao

    .

    Takriban watu 76 hawajulikani waliko nchini Kenya huku kukiwa na mafuriko makubwa ambayo tayari yamesababisha maafaya makumi ya watu, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasema.

    Watu katika vijiji karibu na Mai Mahiu, yapata kilomita 60 kutoka mji mkuu, Nairobi, walisombwa na maji walipokuwa wamelala Jumatatu asubuhi.

    Kisa hicho kilitokea baada ya maji kuvuma kwenye mtaro ulioziba chini ya njia ya reli.

    Takriban watu 50 walikuwa wamethibitishwa kufariki kufikia Jumatatu jioni, huku Shirika la Msalaba Mwekundu likiongeza Jumanne kwamba manusura 110 wameokolewa.

    Kwa siku ya pili, waokoaji wanajaribu kuokoa wale ambao wamenaswa chini ya vifusi. Pia wanajaribu kuopoa maiti kutoka kwenye matope huku kukiwa na hofu kwamba idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka zaidi.

    "Ninajaribu kuokoa vitu vilivyochukuliwa na maji na kutafuta watu waliopotea pia," Stephen Kamau, mwanakijiji ambaye aliponea chupuchupu katika maafa hayo, aliambia BBC.

    "Niliamka katika ulimwengu tofauti. Kila kitu kilikuwa kimesombwa na maji. Tuna hofu. Moyo wangu ni mzito."

    Maafisa kutokaHudumaya vijana wanaotumikia Taifa (NYS) wameungana na wenyeji na Shirika la Msalaba Mwekundu katika juhudi zao za kutafuta manusura.

    Kwa jumla, karibu Wakenya 170 wameuawa katika mvua kubwa na mafuriko katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

    .

    Soma zaidi:

    Takribani watu 50 wapoteza maisha katika vijiji karibu na mji wa Mai Mahiu

  9. Kijana Mkenya alining'inia kwenye mti huku mafuriko yakiwasomba wanakijiji

    Barbara Plett Usher

    BBC News, Mai Mahiu

    th
    Image caption: Veronica Karanja alinusurika kwenye mafuriko hayo - lakini kaka yake mwenye umri wa miaka 9 hakuponea

    Wiki iliyopita mimi na timu yangu tumekuwa tukiripoti kuhusu mafuriko yanayosababisha uharibifu katika sehemu za Kenya.

    Siku ya Jumanne, tulitembelea eneo la Mai Mahiu, ambako karibu watu 50 waliuawa wakati mafuriko yaliposomba wanakijiji walipokuwa wamelala.

    Tuliwafuata waokoaji chini kando ya kingo za mto zilizolipuka, walikuwa wamebeba majembe, reki na vijiti ili kupenya matawi ya miti iliyong'olewa.

    Tulisimama kwenye kilima kikubwa cha matawi yaliyovunjika, kufunika nyumba iliyovunjika, tunaambiwa.

    Familia ya watu sita iliishi katika nyumba hiyo na huenda wamezikwa chini ya kilima hiki.

    Wafanyakazi wa uokoaji waliita tingatinga, ambalo limekuwa likiondoa uchafu katika kujaribu kuitafuta familia hiyo.

    Upande wa mbali wa mto, paneli za paa za bati huteleza juu ya maganda ya nyumba ambayo bado yamesimama.

    Veronica Karanja, 17, na babake David wamerudi kutazama uharibifu huo.

    Usiku huo wa kutisha kijana huyo alichukuliwa na maji lakini aliweza kuning’inia kwenye mti hadi yakatulia.

    Aliporudi, hakuweza kumpata baba yake, hadi alipoita. Alikuwa amepigwa kichwani na kumpoteza kaka yake Paul mwenye umri wa miaka 9.

    David ametoka tu kutoka chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutazama mwili huo, macho yake yakiwa na huzuni .

    Familia iliishi kwa kutegemea mifugo yao lakini yote imesombwa na maji . Kuku mia tisa na nguruwe 21 waliosombwa na maji - watano tu wamesalia.

    Soma zaidi:

    Kenya:Serikali yaelekeza ukaguzi wa mabwawa yote huku ikilenga kuwahamisha watu

  10. Video za 'unyanyasaji wa kingono' za mbunge wa India zazua hasira

    .

    Maelfu ya video zinazodaiwa kumuonyesha mbunge wa India akiwanyanyasa kingono wanawake zimesambaa katika jimbo la kusini la Karnataka, na kuzua hasira.

    Polisi wanachunguza madai dhidi ya Prajwal Revanna ambaye anatuhumiwa kuwanyanyasa wanawake kadhaa.

    Bw Revanna hajazungumza lolote lakini afisa kutoka afisi yake alikanusha akisema video hizo ni za bandia zenye nia ya kumharibia sifa.

    Mbunge huyo ni wa chama cha Janat Dal mshirika wa chama cha Waziri Mkuu Narendra Modi cha Bharatiya Janata Party.

    Babake HD Revanna, ambaye ni mbunge katika bunge la jimbo la Karnataka, pia ni mshitakiwa katika malalamiko ya polisi yaliyowasilishwa na mfanyakazi wa zamani wa familia hiyo. Amekanusha madai hayo na kuyataja kuwa ni njama za kisiasa.

  11. Mtu aliyeshambulia watu kwa upanga akamatwa

    .

    Mwanamume mwenye umri wa miaka 36 amematwa katika eneo la Hainault, mashariki mwa London.

    Polisi na huduma nyingine za dharura wamesema mtu mwenye upanga ameshambulia watu kwa kuwachoma upanga huo.

    "Tuliitwa muda mfupi kabla ya 06:00 Jumanne GMT kuwa kuna gari lililoingizwa kwenye nyumba katika eneo la Thurlow Gardens na kwamba watu wamechomwa visu," polisi wamesema.

    Mshukiwa aliendelea kuwashambulia wananchi wengine na maafisa wawili wa polisi.

    "Tunasubiri taarifa kuhusu hali ya waliojeruhiwa lakini mwanamume huyo amekamatwa katika eneo la tukio na yuko chini ya ulinzi," Polisi wameongeza.

  12. Wasanii wa Nigeria Davido na Wizkid warushiana cheche za maneno

    .
    Image caption: Wizkid

    Wasanii wawili wakubwa wa muziki nchini Nigeria Wizkid na Davido 'waliwasha moto' katika mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumatatu baada ya kutupiana cheche za maneno.

    Waimbaji hao wawili wenye mamilioni ya wafuasi duniani kote wanachukuliwa kuwa wapinzani huku wapenzi wengi wa muziki wa Nigeria wakijiweka kama "Team Wizkid" au "Team Davido".

    Mzozo huo ulizuka baada ya mashabiki kumtaka Wizkid kuwaachia wimbo mpya kwenye X. Alijibu kwa kuweka video yenye utata ya Davido na kuandika “niombe hivi, nitume video”.

    Miezi kadhaa iliyopita video yenye utata ya mtu anayefanana na Davido ilisambaa mitandaoni ambapo alionekana akiomba mtu amsaidie.

    Davido, 31, alijibu kwa kusema hatapoteza muda na juhudi zake kwa mtu ambaye kazi yake ilifufuka miaka michache iliyopita kabla ya kufa tena kama jibu la chapisho la Wizkid.

    Vita vya maneno vimevutia hisia nyingi kwenye mitandao ya kijamii na blogu huku mjadala ukisambaa katika mitaa ya Nigeria.

    Mashabiki wa waimbaji wote wawili hatahivyo wamekuwa wakiwatetea wasanii wao huku mjadala ukiendelea.Kituo maarufu cha muziki cha Hip Tv kwa sasa kinafanya kura ya maoni katika X kuhusu nani kati ya wasanii hao ameshinda vita hivyo.

    Waimbaji wote wawili wanachukuliwa kuwa nyota wawili wakubwa wa muziki barani Afrika. Wote wameshinda tuzo kadhaa za muziki za MTV na BET na wameshirikiana na wasanii wa kimataifa akiwemo Drake, Chris Brown na Nicki Minaj.

    .
    Image caption: Davido
  13. Chumba cha msichana wa miaka 3 'chavamiwa' na nyuki

    .
    Image caption: Saylor Class, akikagua baadhi ya wadudu wenye mabawa waliokuwa wakimlinda usiku.

    Wakati Saylor Class mwenye umri wa miaka mitatu alipoanza kulalamika kuhusu wanyama wakubwa katika chumba chake cha kulala, wazazi wake walifikiri ilikuwa ni dhana tu ya mawazo ya mtoto.

    Lakini mfugaji nyuki aligundua makumi ya maelfu ya nyuki juu ya chumba cha kulala cha msichana huyo.

    Saylor alikuwa amelalamika kuhusu "vinyama kwenye ukuta" wa chumba chake katika nyumba yao ya shamba huko Charlotte, North Carolina.

    Mama yake, Ashley Massis Class, na mumewe hawakufikiria lolote kuhusu hilo.

    Awali wazazi hao walikuwa wamemuonyesha binti yao sinema ya Pixar, Monsters, Inc."Tulimpa hata chupa ya maji na tukasema ni dawa ya kuogofya ili aweze kunyunyiza wanyama hao usiku," alisema Bi Massis Class, mbunifu wa nyumba.

    Lakini kwa miezi iliyofuata, Saylor alisisitiza zaidi kwamba kulikuwa na kitu chumbani mwake.

    Ilianza kuwa na maana zaidi wakati Bi Massis Class aliona nyuki wakikusanyika katika makundi karibu na dari na bomba la moshi nje ya nyumba yao ya miaka 100.

    Walifikiri Saylor huenda alikuwa anasikia kelele karibu na dari ya chumba chake cha kulala.

    Bi Massis Class aliita kampuni ya kudhibiti wadudu ambayo iligundua kwamba wadudu hao wenye mabawa walikuwa nyuki, spishi inayolindwa nchini Marekani.

    Yeye na mume wake waliwasiliana na mfugaji nyuki ambaye aliona wadudu hao walikuwa wakisafiri kuelekea kwenye ubao wa sakafu ya dari - juu ya chumba cha kulala cha binti yake.

    Nyuki hao walikuwa wametumia miezi minane kujenga mzinga wa nyuki.

  14. Ufilipino: Mji mkongwe uliozama wajitokeza baada ya bwawa kukauka kwa joto kali

    .

    Magofu ya mji wenye umri wa takriban miaka 300 yameibuka tena huku viwango vya juu vya joto vikiendelea nchini Ufilipino na kukausha bwawa kubwa.

    Mji wa Pantabangan ulizama katika miaka ya 1970 ili kujenga hifadhi.

    Lakini hujitokeza juu, wakati hali ya hewa ni kavu na ya joto.

    Hatua hiyo inajiri wakati karibu nusu ya nchi inakabiliwa na ukame, na halijoto inafikia kiwango cha juu cha 50C (122F) katika baadhi ya maeneo.

    Huu ndio muda mrefu zaidi kwa mji huo kuwahi kuwa juu ya maji tangu bwawa hilo kujengwa, Marlon Paladin, mhandisi wa shirika la serikali linaloendesha mabwawa ya nchi hiyo, aliliambia shirika la habari la AFP.

    Joto kali limetatiza maisha ya kila siku ya mamilioni kwani shule zimefungwa kwa siku nyingi huku wafanyikazi wa ofisi wakishauriwa kufanya kazi nyumbani.

    Na bado kunaweza kuwa na joto zaidi katika siku zijazo, Benison Estareja, mtaalamu wa hali ya hewa katika ofisi ya serikali ya Pagasa, aliiambia BBC News.

    "Athari ya jumla ya mabadiliko ya hali ya hewa nchini Ufilipino ni viwango vya juu vya joto. Joto tunalopata, linaweza kuongezeka kwa kasi katika siku zijazo," Bw Estareja alisema.

    Malindi: Jinsi mji wa pwani ya Kenya ulivyobadilika na kuwa 'Italia ndogo'

    Mji mkubwa wa zamani wapatikana katika Amazon

  15. 'Salah ndiye aliyemkosea Klopp'

    .
    Image caption: Mohamed Salah alikuwa amefunga bao moja katika mechi tano za Premier League kabla ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya West Ham

    Mohamed Salah "alikosea" kwa kuzozana na meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kwenye mstari wa kutoka nje ya uwanja wakati wa sare ya 2-2 Jumamosi dhidi ya West Ham United,

    asema mshambuliaji wa zamani wa Ligi ya Premia Chris Sutton.

    Salah alikuwa amekalia benchi katika mchezo huo na akagombana na Klopp huku akijiandaa kuingia kama mchezaji wa akiba katika dakika ya 79.

    Sare hiyo inawaacha Liverpool, ambao wako nje ya Ligi ya Europa, pointi tano nyuma ya vinara wa Ligi Kuu, Arsenal.

    Sutton anasema tukio hilo halikumuonyesha vyema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye ni mfungaji bora wa Reds msimu huu akiwa na mabao 24 lakini hajakuwa katika kiwango bora katika michezo ya hivi majuzi.

    "Sikupenda lakini nadhani Mo Salah ndiye aliyekosea" Sutton alisema kwenye kipindi cha Jumatatu Usiku cha BBC Radio 5 Live.

    "Hana tofauti na wachezaji wenzake wa Liverpool na ukweli ni kwamba kiwango chake hakijakuwa kizuri tangu aliporejea kutoka kwenye jeraha.

    "Sina ubaya dhidi ya Salah na mchezaji mahiri ambaye amekuwa Liverpool. Amekuwa wa ajabu lakini nadhani kuna mstari na kwa bahati mbaya aliuvuka."

    Klopp, ambaye anaondoka Liverpool mwishoni mwa msimu, alimleta Salah Anfield mnamo Juni 2017 na amekuwa mmoja wa wachezaji wake wenye ushawishi mkubwa.

    Lakini Sutton anaamini kuwa Klopp alikuwa na kuchagua kikosi chake cha wachezaji XI wa kwanza aliohisi kuwa waliipa Liverpool nafasi nzuri zaidi ya kupata ushindi.

    "Huwezi kuishi zamani," aliongeza Sutton.

  16. Man United kuwauza takriban wachezaji wote wa kikosi cha kwanza

    .
    Image caption: Marcus Rashford amekuwa Manchester United katika maisha yake yote, akicheza kwa mara ya kwanza mwaka 2015

    Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa takribani timu yao yote ya kikosi cha kwanza msimu huu wa joto huku Sir Jim Ratcliffe akijaribu kuigeuza klabu hiyo kupigania mataji na kuheshimiwa tena

    Inafahamika kuwa Marcus Rashford yumo kwenye orodha hiyo, ingawa vyanzo vya klabu vinasisitiza kwamba wanapendelea kumbakisha mshambuliaji huyo wa Uingereza na kushirikiana naye kurejesha kiwango kilichomletea mabao 30 kwa mara ya kwanza msimu uliopita.

    Paris St-Germain hapo awali walikuwa wakihusishwa na Rashford na wanatazamiwa kumpoteza nyota wao Kylian Mbappe, ingawa vyanzo hapo awali viliitenga PSG iliofuzu katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

    Kati ya wachezaji wa kawaida wa meneja Erik ten Hag, chipukizi Rasmus Hojlund, Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho wanafikiriwa kubakizwa.

    Ingehitaji ofa kubwa kabla United kufikiria kumuuza nahodha Bruno Fernandes, mlinda lango Andre Onana na beki wa pembeni Diogo Dalot, ambaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitano chini ya miezi 12 iliyopita.

    Kiasi halisi cha biashara wanayofanya hatimaye kiko wazi kuhoji. Haijabainika jinsi maslahi yatakavyokuwa katika kikosi chochote cha United, wala ada wanazoweza kuitisha.

    Wamekuwa wakishindwa kuwauza wachezaji katika siku za nyuma. Uhamisho wa Daniel James kwa pauni milioni 25 kwenda Leeds mnamo 2021 ilikuwa mara ya mwisho kuchangisha pauni milioni 20 kutoka kwa mchezaji.

    Kuna uwezekano watalazimika kumaliza nafasi ya sita kwenye ligi ya Premia au kuifunga Manchester City kwenye fainali ya Kombe la FA ili kufuzu kwa Ligi ya Europa.

    Kwa sasa wako nafasi ya sita, pointi moja mbele ya Newcastle, ambao watacheza nao Old Trafford mnamo Mei 15.

  17. Shirika la ndege la Kenya Airways lasitisha safari za ndege kuelekea mji mkuu wa DR Congo - kunani?

    .
    Image caption: Wafanyakazi wawili wa shirika la ndege la Kenya Airways walitiwa mbaroni na maafisa wa Ujasusi wa Kongo

    Shirika la ndege la Kenya Airways (KQ) linasema kuwa limesitisha safari za ndege kuelekea mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kinshasa kwa sababu ya kuzuiliwa "kinyume na sheria" kwa wafanyikazi wawili na ujasusi wa kijeshi.

    KQ ilitoa tangazo hilo Jumatatu katika taarifa kwenye X, ambayo zamani ilikuwa Twitter, na kusema "hawawezi kuedeleza safari za ndege bila wafanyikazi hao".Walisema kusimamishwa kwa safari hizo kutaanza Jumanne.

    Tarehe 19 Aprili, wafanyakazi wawili wa KQ waliwekwa chini ya ulinzi na Uchunguzi wa Kijeshi (DEMIAP) kwa sababu ya madai ya "kukosa nyaraka za forodha za mizigo ya thamani", kulingana na shirika hilo la ndege.

    Lakini afisa mkuu mtendaji wa KQ alisema "mzigo huo haukubebwa au kukubaliwa na KQ kutokana na kutokamilika kwa nyaraka".

    Wakati wa kukamatwa kwao , simu za wafanyikazi hao wawili zilichukuliwa na kuzuiliwa hadi Aprili 23 wakati maafisa wa Ubalozi na timu ya KQ waliruhusiwa kuwatembelea.

    Kampuni ya ndege iliwahimiza wanajeshi wa Kongo kuwaachilia wafanyikazi wa KQ kwa familia zao.

    Serikali ya DR Congo haijatoa tamko lolote .

  18. Mtoto wa bondia na bingwa wa zamani wa UFC Francis Nganou afariki akiwa na miezi 15

    .
    Image caption: Francis Nganou

    Mtoto wa umri wa miezi 15 wa bondia Francis Ngannou amefariki dunia.

    Bingwa huyo wa zamani wa UFC alichapisha kwenye X siku ya Jumatatu usiku: "Ameondoka mapdema, lakini bado ameenda.

    "Mtoto wangu, mwenzangu, mwenzangu Kobe alijawa na maisha na furaha, sasa analala bila uhai. Nilipiga kelele jina lake mara kwa mara lakini hajibu.

    "Nilikuwa mtu mwenye furaha karibu naye na sasa sijui mimi ni nani. Maisha sio sawa kutuathiri pale ambapo inaumiza zaidi."

    Meneja wa mpiganaji huyo Marquel Martin alichapisha mtandaoni akisema kwamba yeye pamoja na "mamilioni ya wengine" watamwombea raia huyo wa Cameroon.

    Conor McGregor alikuwa miongoni mwa wapiganaji na mashabiki waliotuma salamu zao za rambirambi kwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 37 na nyota wa zamani wa (MMA).

    "Samahani sana kusikia kufiwa kwako Francis, sala zangu ziko pamoja nawe na familia yako kwa wakati huu," Alisema raia huyo wa Ireland katika X.

    Pambano la mwisho la Ngannou lilikuwa kushindwa kwake na Anthony Joshua huko Saudi Arabia. Baada ya pambano hilo alitupilia mbali pendekezo la kurudi kabisa katika MMA ambapo alitengeneza umaarufu wake.

    Francis Ngannou: Mhamiaji haramu kutoka Afrika atakaye zichapa na Tyson Fury kesho

    Mji wa Nigeria unaomuenzi bondia Antony Joshua

    Tyson Fury vs Francis Ngannou: Wamshabikia nani?

  19. Marekani yasema vitengo vya jeshi la Israel vilikiuka haki za binadamu

    .
    Image caption: Kitengo cha Jeshi la Israel Netza Yehuda

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imevitambua vitengo vitano vya jeshi la Israel vinavyohusika na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika matukio ya mtu binafsi, lakini inasema wataendelea kuungwa mkono na jeshi la Marekani.

    Matukio yote yaliyohusika yalitokea nje ya Gaza kabla ya vita vya sasa.

    Israel ilichukua hatua za kujirekebisha katika vitengo vinne, ikitoa "taarifa za ziada" juu ya kitengo chengine cha tano, idara hiyo inasema.

    Hii ina maana kwamba vitengo vyote bado vinastahiki usaidizi wa kijeshi wa Marekani.

    Washington ndiye mfadhili mkuu wa kijeshi wa Israel, akiipatia silaha na mifumo ya ulinzi yenye thamani ya $3.8bn (£3bn) kwa mwaka.Tangazo hilo ni uamuzi wa kwanza wa aina yake kwa kitengo chochote cha Israel na serikali ya Marekani.

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Vedant Patel alisema vitengo vitano vya vikosi vya usalama vilifanya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

    "Vitengo vinne kati ya hivi vimerekebisha kikamilifu ukiukwaji huu, jambo ambalo tunatarajia washirika kufanya," alisema.

    "Kwa kitengo kilichosalia, tunaendelea kuwa katika mashauriano na mazungumzo na serikali ya Israel; wamewasilisha taarifa za ziada kuhusu kitengo hicho," aliongeza.

    Idara hiyo imekanusha madai kuwa iliunga mkono chini ya shinikizo la kisiasa kwa kuendeleza usaidizi wa kijeshi kwa kitengo hicho licha ya kutoweza kusema iwapo kumekuwa na uwajibikaji au la.

    Tunachofahamu kuhusu kikosi cha jeshi la Israel kitakachowekewa vikwazo na Marekani

    Walowezi wa Kiyahudi wanaotaka kujenga makazi huko Gaza

    Jeshi la Israeli linajumuisha akina nani na ni jamii gani nyingine zinazohudumu katika jeshi hilo?

  20. Natumai hujambo