Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

time_stated_uk

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja

  2. Maelfu wahamishwa baada ya bwawa kupasaka kusini magharibi mwa Urusi

    Maelfu ya watu wamehamishwa

    Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka jimbo la kusini magharibi mwa Urusi, kwa sababu mafuriko mabaya ziaidi kuwahi kushuhudiwa kufuatia kupasuka kwa bwawa la Orsk, maafisa wanasema.

    Awali, hali ya dharura ilitangazwa katike eneo zima la Orenburg baada ya viwango vya maji vya mto Ural kupanda zaidi na kutokana na kuyayuka kwa theluji.

    Maafisa wanasema kwamba wakazi 10,000 huenda wako katika eneo ambalo linakumbwa na mafuriko na kwamba makazi zaidi ya elfu 4 zinaweza kuathirika.

    ''Shughuli ya kukarabati eneo la bwawa lililopasuka huko Orsk zinaendelea,’ imesema wizara ya huduma za dharura katika taarifa.

    Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti kwamba watu zaidi ya 700 katika mikoa miwili kati ya mitatu katika jimbo la Orsk wamehamishwa katika eneo hilo.

    ‘Raia wanaoishi katika mikoa ya Leninsky na Sovetsky kwenye jimbo la Orska wanahamishwa katika vituo vya makazi ya muda,'' taarifa ya mwendesha mashtaka katika jimbo hilo ilisema.

    Meya wa mji wa Orsk Vasily Kozupitsa amesema kwamba hali ilikuwa inadorora haraka, huku nusu ya mji huo wa kale wa ukifurika maji nayo maeneo mengineya jiji hilo yakikatizwa.

    Huduma za dharura za eneo hilo zimesema kwamba zinajitahidi kudhibiti maji ya mafuriko katika mjini wa Orsk, uliopo takriban kilomita 1,800 kusini mashariki mwa mji mkuu, Moscow.

    Picha ambazo zilizochapishwa katika mtandao wa kijamii wa Telegram na ambazo hazijathibitishwa na BBC zimeonekana kuonyesha maji mengi yakitoka kwenye mpenyo uliotokea kwenye bwawa hilo.

  3. Ethiopia yaondoa amri ya kutotoka nje katika jimbo la Amhara

    Hali ya utulivu imerejea katika baadhi ya miji mikubwa, mapigano yanaripotiwa katika miji midogo

    Kituo maalum kinachosimamia usalama na hali ya dharura iliyotangazwa katika jimbo la Amhara kaskazini magharibi mwa Ethiopia, limeondoa amri ya kutotoka nje iliyowekwa katika jimbo la Amhara.

    Amri hiyo iliangazia usalama katika barabara kuu inayounganisha miji ya Debre Berhan na Dessie ikisema imeimarika.

    Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti linalomilikiwa kibinafsi la Addis Standard.

    Kituo hicho cha kusimamia usalama kimesema kwamba amri hiyo imeondolewa kuanzia jumamosi Aprili 6.

    ''Uamuazi wa kuondoa amri hiyo ulitokana na hali ya usalama kuimarika na vile vile ombi rasmi kutoka kwa jamii ya eneo hilo, ‘ gazeti hilo liliripoti.

    Mnamo Februari 24 KItuo hicho Kilitoa amri ya kupiga marufuku safari zote kwenye barabara hiyo inayounganisha miji hiyo miwili baada ya wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa kundi la Fano kuuawa raia wanane.

    Kundi hilo la Fano limeshutumiwa kwa kutekeleza maovu dhidi ya raia na kupora mali.

    Pia unaweza kusoma:

    Kwa nini wanamgambo wa Amhara nchini Ethiopia wanapambana na jeshi?

    Je, ni nini chanzo cha vurugu za Amhara nchini Ethiopia?

  4. Mtoto wa Lebron James, atangaza kushiriki katika usajili wa NBA 2024

    Bronny ndiye mtoto mkubwa kati ya watoto watatu wa LeBron James
    Image caption: Bronny ndiye mtoto mkubwa kati ya watoto watatu wa LeBron James

    Bronny James, mwana wa kiume wa mchezaji mashuhuri wa ligi ya mpira wa vikapu Marekani NBA ametangaza kwamba atajisajili katika uteuzi wa mwaka wa 2024 wa ligi hiyo yaani (2024 NBA draft)

    Tangazo hili linajiri wakati ambapo kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alipatwa na mshtuko wa moyo akiwa mazoezini katika chuo kikuu cha Southern California (USC).

    Alifanyiwa upasuaji wa moyo na kurejea chuoni kushiriki katika msimu wa ligi ya mpira wa vikapu ya vyuo vikuu Marekani katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji mwezi Desemba.

    Lebron ambaye anaongoza orodha ya wafungaji vikapu vingi zaidi katika michuano ya ligi ya NBA, hajaficha au kulifanya siri azimio lake la kutamani mwananwe kuche za naye mechi rasmi.

    James mwenye umri wa miaka 39, ambaye anachezea timu ya Los Angeles Lakers, aliiambia kituo cha Habari cha ESPN 2o23 kwamba: ‘ Ninahitaji kucheza pamoja na mwanangu, nina hamu ya kuwa na Bronny uwanjani.’

    Bronny alisema kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram kwamba: ‘ Nimeshuhudia hali ngumu katika mwaka uliopita, lakini hayo yote yamenipa mafunzo na motisha ya kukuwa kama mwanamume, mwanariadha na mwanafunzi.’

    ‘Nimefanya uamuzi wa kujisajili katika uteuzi huu wa NBA d huku nikiendelea kuchezea timu yangu ya chuoni, na pia nitajisajilia katika eneo la kutaka uhamisho wa NCCAA.

  5. Bomba la mafuta la Urusi lalipuliwa katika eneo la Rostov – Taarifa za kijajusi za Ukraine

    xx

    Bomba la mafuta ambalo lilikuwa linatumika kujaza malori bidhaa mbali mbali za petroli limelipuliwa katika eneo la Rostov nchini Urusi.

    Haya ni kwa mujibu wa tovuti ya Habari ya Ukraine -RBC ambayo imeripoti kwamba taarifa hizo zilitokana na ujajusi kutoka kwa Idara kuu ya kijajusi nchini humo na jeshi la Ukraine - HUR .

    ‘Usiku wa kuamkia Aprili 6 2024, bomba la mafuta lililipuliwa katika eneo la makazi la Azov lililopo katika jimbo la Rostov. Bomba hilo lilitumika kujazia biadhaa za petroli kutoka kwa kituo cha mafuta hadi kwenye malori, kwenye bandari ya bahari ya Azov,’ripoti hiyo ilisema.

    Kulingana na maafisa wa Ukraine, kujaza malori kwa petroli kumesimamishwa kwa muda usiojulikana. HUR ilisema kwamba, Taifa lenye uchokozi lilitumia kituo hiki kwa shughuli zake za kijeshi, na kusaidia vita hivi vya halaiki dhidi ya Ukraine.’

    Chanzo: tovuti ya Ukraine ya RBC, Kyiv.

  6. Vita vya Gaza: Ujumbe wa Hamas kuzuru Cairo kwa mazungumzo

    Hamas imetawala Gaza tangu 2007
    Image caption: Hamas imetawala Gaza tangu 2007

    Kundi la Hamas lasema kwamba ujumbe wake utakwenda Cairo, Aprili 7 kwa ajili ya vikao vya kujadili kusitishwa kwa mapigano Gaza.

    Ujumbe wa kundi la Hamas unaoongozwa na Naibu mkuu wa kundi hilo huko Gaza,Khalil Al-Hayya utakwenda Cairo, Misri, Jumapili Aprili 7, kuhudhuria kikao cha kujadili kusitishwa kwa mapigano, kama hatua ya kuitikia mwaliko kutoka kwa wapatanishi wa kimisri.

    Kundi hilo limesa a hilo katika taarifa ambayo imechapishwa Jumamosi hii, Aprili 6.

    Hamas imesisitiza matakwa yake ambayo yalitolewa mwezi Machi, yenye mapendekezo 14 yaliyoandaliwa kabla ya maafikiano ya baraza la usalama wa umoja wa mataifa kupitishwa Machi 25.

    Uamuzi huo wa UNSC ulitaka mapigano kusitishwa kabisa, na kuvitaka vikosi vya kijeshi vya Israel kuondoka Gaza, kurejeshwa kwa waliohamishwa makwao na kufanyika kwa mabadilishano ya mateka waliochukuliwa Israel na wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa Israel.

    Maelezo zaidi:

    Je, ni kweli kuwa Hamas iliundwa na Israel?

    Marwan Issa: Mfahamu Kamanda wa Hamas ambaye Israel inadai kumlenga katika handaki

    Je, Israel itafanikiwa kuiondoa Hamas?

  7. Habari za hivi pundeJeshi la Israel lasema limepata mwili wa mateka mmoja kutoka Gaza

    Elad Katzir alitekwa nyara kutoka kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba
    Image caption: Elad Katzir alitekwa nyara kutoka kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba

    Jeshi la Israel limesema limepata mwili wa mwanamume aliyeketwa nyara na kuzuiliwa ndani ya Gaza, katika operesheni ya uvamizi wa kijeshi mjini wa Khan Younis.

    Elad Katzir alitekwa kutoka mji wa Kibbutz Nir Oz wakati wa shambulizi ya kundi la Hamas kwenye eneo la kusini mwa Israel Oktoba 7.

    Kwa mujibu wa jeshi la Israel na Mamlaka ya usalama nchini humo ISA, mwili wake umepatikana ndani ya Gaza katika opereshi ya usiku kucha na kurejeshwa Israel.

    Alitambuliwa na wahudumu wa matibabu na familia yake imeaarfiwa.

    IDF na ISA zimesema katika taarifa ya pamoja, kwamba: Mwili wa mateka Elad Katzir ambaye kulingana na taarifa za kijasusi, aliuawa akiwa amezuiliwa na kundi la kigaidi la Islamic Jihad, uliokolewa usiku kutoka Khan Younis na kurejeshwa katika himaya ya Israel.

    Wamesema kwamba mwili huo ulitambuliwa kwa kutumia taarifa za kina za kijasusi.

    Bwana Katzir mwenye umri wa miaka 47, alitekwa kutoka Niir Oz kwa Pamoja na mama yake Hanna mwenye umri wa miaka 77.

    Mama yake aliachiliwa huru mwezi Novemba 2023, huku babake Avraham akiuawa katika eneo la Kibbutz, kulingana na IDA na ISA.

    Soma zaidi:

    Vita vya Gaza: Israeli hupata wapi silaha zake?

    Nini chimbuko la uhasama kati ya Israel na Iran?

  8. Mexico yakatiza uhusiano wa kiplomasia na Ecuador baada ya uvamizi wa ubalozi

    xx

    Mexico imekatiza uhusiano na Ecuador baada ya polisi kuvamia ubalozi wa Mexico mjini Quito ili kumkamata Makamu wa Rais wa zamani wa Ecuador Jorge Glas.

    Rais wa Mexico Andrés Manuel López Obrador alisema "wameingia kwa nguvu" katika ubalozi huo katika "ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa".

    Glas alikimbilia katika ubalozi huo Desemba mwaka jana baada ya Ecuador kutoa hati ya kukamatwa kwake kwa tuhuma ya ufisadi.

    Wakili wa Glas alisema hana hatia. Glas alihudumu kama makamu wa rais wa Ecuador kati ya 2013 na 2017.

    Aliondolewa kazini kutokana na shutuma kadhaa za ufisadi dhidi yake.

    Baadaye mwaka huo huo alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa kuhusishwa na ufisadi katika kampuni kubwa ya ujenzi ya Brazil Odebrecht.

    Waendesha mashtaka walisema alipokea dola milioni 13.5 za kimarekani kama hongo.

    Aliachiwa kutoka gerezani Novemba mwaka jana lakini mamlaka ya Ecuador ikatoa hati nyingine ya kukamatwa kwa tuhuma zaidi ya rushwa, na kumfanya Bw Glas kutafuta hifadhi katika ubalozi wa Mexico.

  9. Ndege zisizo na rubani za Urusi zashambulia Kharkiv na kuua watu sita - Maafisa

    xx

    Watu sita wameuawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani za Urusi katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine, maafisa wa eneo hilo wamesema.

    Meya Ihor Terekhov alisema ndege zisizo na rubani za Shahed zilizotengenezwa na Iran zilishambulia majengo kadhaa, ikiwa ni pamoja na majengo ya ghorofa, mapema Jumamosi.

    Mashambulizi dhidi ya Kharkiv, jiji kubwa lililo karibu zaidi na mpaka wa Urusi, yamekuwa yakiongezeka katika wiki za hivi karibuni.

    Maafisa wa Ukraine wamesema mji huo unaweza kuwa shabaha ya mashambulizi ya baadaye ya Urusi.

    "Shambulio hili dhidi ya wakazi wenye amani wa Kharkiv kwa mara nyingine tena linathibitisha kwamba Urusi ni taifa la kigaidi," Bw Terekhov aliandika kwenye mtandao wa Telegram.

    Takriban watu 10 walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo, aliongeza.

    Picha ambazo hazijathibitishwa zilizochapishwa na polisi wa Ukraine zilionyesha waokoaji wakiwa kwenye eneo la tukio, huku majengo yaliyohawa kwenye shambulio hilo yakionekana.

    Polisi waliripoti kuwa watu kumi pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo na kuongeza kuwa liliathiri nyumba za ghorofa, vituo vya mafuta, majengo ya utawala na magari.

    Maelezo zaidi:

  10. Hujambo na karibu