Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Abdalla Seif Dzungu na Asha Juma

time_stated_uk

  1. Vita vya Gaza: Marekani ina ‘matumaini’ kwamba Hamas itakubali pendekezo jipya la Israel la kusitisha mapigano

    .

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema ana matumaini kuwa Hamas itakubali pendekezo la hivi punde la Israel la kusitisha mapigano Gaza na kuwaachilia mateka.

    Aliita pendekezo hilo kuwa la "ukarimu usio wa kawaida", wakati ujumbe wa Hamas ulipojadiliana na wapatanishi mjini Cairo.

    Baada ya wiki kadhaa za mvutano, afisa mkuu wa Hamas alinukuliwa akisema "haina masuala makubwa" na pendekezo hilo.

    Inaripotiwa kuwa inahusisha kauli mpya juu ya kurejesha utulivu kwa maana ya kukidhi matakwa ya Hamas ya kusitisha mapigano ya kudumu.

    Serikali ya Israel inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wake wa kimataifa na familia za mateka kuafikia makubaliano.

    Israel ilianzisha kampeni ya kijeshi ya kuiangamiza Hamas kujibu mashambulizi ya kundi hilo kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 253 walichukuliwa mateka.

    Zaidi ya watu 34,480 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayosimamiwa na Hamas.

    Makubaliano yaliyokubaliwa mwezi Novemba yaliifanya Hamas kuwaachia huru mateka 105 kamahatua ya kusitisha mapigano kwa wiki moja na wafungwa wapatao 240wa Kipalestina kuachiliwa kutoka katika za Israel.

    Soma zaidi:

    Vifo visivyoelezeka vya Wapalestina kwenye magereza ya Israel

  2. Kenya:Serikali yaelekeza ukaguzi wa mabwawa yote huku ikilenga kuwahamisha watu

    .

    Serikali nchini Kenya imeagiza Kamati za Usalama na Ujasusi za Kaunti kote nchini humo kukagua mabwawa yote ya umma na ya kibinafsi kufikia keshoJumanne.

    Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki mnamo Jumatatu aliagiza kamati hizo kupendekeza baadaye kutolewa kwa amri za kuhamisha watu kwa lazimakatika makazi yanayochukuliwa kuwa katika hatari hadi maeneo salama.

    Haya ni kufuatia kisa cha Jumatatu asubuhi ambapo bwawa lilipasua kingo zake huko Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru, na kuzisombanyumba na magari, na kuwaua zaidi ya watu 42.

    Mafuriko hayo yalitoka kwenye mto ulio karibu ambao ulivunja kingo zake baada ya mvua kunyesha, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu.

    Waziri wa Mambo ya Ndani aliagiza kaunti kupeleka vikosi vya kutekeleza sheria katika maeneo ya barabarani ambayo hukabiliwa na mafuriko na na katika sehemu zadaraja ili kuzuia madereva au watembea kwa miguu kuhatarisha maisha yao kwa kuvuka.

    Soma zaidi:

    Zaidi ya watu 40 wapoteza maisha nchini Kenya baada ya bwawa kupasua kingo zake

    .
  3. Habari za hivi pundeHumza Yousaf: Waziri Kiongozi wa Uskochi ajiuzulu

    th

    Waziri Kiongozi wa Uskochi Humza Yousaf amejiuzulu wadhifa wake

    Kujiuzulu kwake kunajiri zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuwa waziri kiongozi wa Usokochi .

    Uteuzi wake ulifuatia kupanda kwake kwa kasi katika chama chaSNP tangu alipokuwa mbungekwa mara ya kwanza mnamo 2011.

    Mwaka mmoja baada ya kushinda kiti, alifanywa waziri wa Ulaya na maendeleo ya kimataifa, nafasi ambayo alishikilia kwa karibu miaka minne.

    Kisha alipandishwavyeo, mara kadhaa ​​na kuwa katibu wa usafiri mnamo 2016, akitajwa kama katibu mpya wa haki mnamo 2018 na baadaye kuwa katibu wa afya mnamo 2021.

    Nicola Sturgeon alipotangaza kujiuzulu kama waziri kiongozimnamo 2023, Yousaf alionekana kama mgombeaji wa kumrithi.

    Alipochukua wadhifa huo, alikua Wazirikiongozi wa kabila ndogo katika serikali iliyogatuliwa na Mwislamu wa kwanza kuongoza chama kikuu cha Uingereza.

  4. Kupasuka kwa bwawa Kenya:Tazama picha kutoka eneo la mkasa

    ,
    .
    .
    .
    .

    Hili eneo lilikuwa sehemu ya kijiji chenye nyumba karibu 18

    .

    Wengi wa majirani za mashuhuda huyu wamesombwa na maji

    “Nilikuwa nimelala niliposikia kishindo kikubwa na mayowe. Maji yalikuwa yamejaa kila mahali," alisema.

    "Tulianza kuokoa watu. Hili begi ni la mtoto niliyemfahamu. Alisombwa na maji. Nimelipata eneo la chini lenye maji," aliongeza.

    .
  5. Burkina Faso yapiga marufuku vyombo vya habari zaidi vya kigeni kwasababu ya ripoti ya HRW

    Mdhibiti wa vyombo vya habari nchini Burkina Faso amesimamisha vyombo vya habari zaidi vya kimataifa kutokana na kutangaza ripoti inayolishutumu jeshi la nchi hiyo kwa kuua raia.

    Serikali ya kijeshi sasa imepiga marufuku mtandao wa Ufaransa TV-Cinq na tovuti za Le Monde na The Guardian, pamoja na shirika la utangazaji la Ujerumani, Deutsche Welle.

    Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya mamlaka ya Burkinabè kuweka marufuku ya wiki mbili kwa BBC na shirika la utangazaji la Marekani la Sauti ya Amerika (VOA) kwa kuripoti ripoti hiyo hiyo ya Human Rights Watch (HRW).

    Baraza la Juu la Mawasiliano (CSC) lilisema katika taarifa yake Jumapili kwamba kuangaziwa kwa ripoti ya HRW na vyombo vipya vilivyositishwa kuendesha shughuli zake huko "kunajumuisha taarifa potofu zinazoweza kuleta kashfa kwa jeshi la Burkina Faso".

    Mdhibiti wa vyombo vya habari pia alisisitiza onyo kwa vyombo vyote vya habari dhidi ya kuandika ripoti hiyo, na kutishia kuviwekea vikwazo.

    Ripoti hiyo iliyotolewa Alhamisi iliyopita na kundi lenye makao yake makuu nchini Marekani la HRW lilishutumu jeshi la Burkinabè kwa kuwaua takriban raia 223 mwezi Februari kaskazini mwa nchi hiyo.

    Mamlaka ya Burkina Faso ilikataa ripoti ya HRW kama "madai yasiyo na msingi" na kusema kuwa wameanzisha uchunguzi wa kisheria "kuthibitisha ukweli".

    Burkina Faso: Je, wakosoaji wa serikali huadhibiwa kwa kupelekwa mstari wa mbele wa vita?

  6. Tanzania: Klabu ya Pamba yarejea Ligi Kuu baada ya miaka 23

    Florian Kaijage

    BBC Dar es Salaam

    .

    Mabingwa wa zamani wa soka wa Tanzania, Pamba ya Mwanza wamefanikiwa kurejea ligi kuu ya nchi hiyo baada ya miaka 23 ya kucheza madaraja ya chini. Mara ya mwisho kucheza ligi kuu ilikuwa mwaka 2001 iliposhuka daraja.

    Kupanda daraja kwa Pamba kumerejesha kicheko kwa mashabiki wa kandanda wa Mwanza, jiji la pili kwa ukubwa nchini Tanzania baada ya Dar es Salaam.

    Mfanikio hayo yamekuja baada ya kujipatia ushindi wa magoli 3-1 ugenini dhidi ya Mbuni FC ya Arusha katika siku ya mwisho ya ligi ya Championship iliyofikia tamati Jumapili Aprili 28. Hali hiyo imeibua shangwe na nderemo huko Mwanza na kanda ya ziwa Victoria.

    Pamba imeshika nafasi ya pili hivyo kufuzu moja kwa moja kwa moja ikikusanya alama 67, pamoja na na KenGold ya Mbeya iliyopanda ligi kuu juma moja kabla pia kuibuka mabingwa wa championship kwa kuvuna alama 70.

    Kabla ya kushuka daraja mwaka 2001, Pamba iliyonyakua ubingwa wa iliyokuwa ligi kuu ya Muungano mwaka 1990, ilikuwa tishio katika soka la Tanzania ikishindana kwa umahiri na kuzitetemesha timu kongwe kama vile Yanga, Simba, Coastal Union na Majimaji za Tanzania Bara pia Small Simba, Kikwajuni, Malindi na Mlandege za Zanzibar.

    Katika mashindano ya vilabu Afrika, Pamba iliyoanzishwa mwaka 1968, iliwahi kupata matokeo ya kukumbukwa miongoni mwa wapenzi wa soka ilipoinyuka timu ya Anse-Aux- Pins kutoka mji wa kibiashara Anse Boileau kusini mwa Shelisheli jumla ya magoli 17-1 mwaka 1990, katika raundi ya awali ya lililokuwa Kombe la Washindi Afrika. Pamba ilishinda 5-0 ugenini katika katika mchezo wa kwanza na 12-1 nyumbani Mwanza huku mshambuliaji wake Fumo Felician akipachika magoli 8 katika mchezo huo wa marudiano.

    Sasa miaka 23 imetosha kurejea ligi kuu, je Pamba itavimudu vishindo vya ligi kuu ya sasa ambayo ina mabadiliko makubwa kuliko ile ya miaka ya 1990 na krejesha ushindani wa enzi zile? Hilo ni jambo la kungojea na kuona.

  7. Zaidi ya watu 40 wapoteza maisha nchini Kenya baada ya bwawa kupasua kingo zake

    .

    Makumi ya watu wameuawa baada ya bwawa kuvunja kingo zake katika eneo la Mai Mahiu nchini Kenya, kaskazini mwa mji mkuu, Nairobi, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limeithibitishia BBC.

    Gavana wa eneo hilo Susan Kihika pia alithibitisha vifo hivyo kwa shirika la habari la AFP, na kuongeza kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

    Maji yalitiririka na kusomba nyumba na magari kadhaa katika kijiji cha Kamuchiri, kufuatia mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha maeneo kadhaa nchini humo.

    Vikosi vya uokoaji vinachimba matope kutafuta manusura, vyombo vya habari vya eneo hilo vilisema, na kuonya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

    .

    Mvua hiyo ilipasua barabara kuu kutoka Nairobi kuelekea Mai Mahiu baada ya mawe makubwa, matope na magogo kuziba eneo hilo.

    Mapema Jumatatu, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema limewapeleka watu kadhaa katika kituo cha afya huko Mai Mahiu kutokana na mafuriko.

    Vifo vya hivi punde vinafanya idadi ya watu kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini tangu mwezi uliopita kuongezeka hadi zaidi ya 100.

    Video content

    Video caption: Makumi ya watu wamepoteza maisha baada ya bwawa kuvunja kingo zake nchini Kenya

    Soma zaidi:

    Watu 23 watoweka baada ya boti kupinduka Tanariver

  8. Raia wa Nigeria wafurahishwa na ziara iliyopangwa ya Harry na Meghan

    .

    Mwanamfalme Harry na Meghan Markle watazuru Nigeria mwezi ujao kufuatia mwaliko wa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, afisa wa kijeshi amesema.

    "Ziara hiyo ni ya kuunganisha ngome ya Nigeria katika mchezo wa [Invictus] na uwezekano wa kuandaa hafla hiyo [katika] miaka ya baadaye," msemaji wa ulinzi Tukur Gusau alisema katika taarifa Jumapili.

    Duke na Duchess wa Sussex wana uhusiano mkubwa na nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

    Mwaka jana, Nigeria ilishiriki kwa mara ya kwanza katika Michezo ya Mwanamfalme Harry ya Invictus, na kushinda medali za dhahabu na shaba na kuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kushiriki katika mashindano hayo.

    Mwana wa mfalme alizindua Michezo ya Mwaliko, tukio la michezo kwa wanajeshi waliojeruhiwa katika mapigano, mnamo 2014.

    Wakati Nigeria ilishiriki katika hafla hiyo huko Dusseldorf, Ujerumani, mwaka jana, waziri wa ulinzi wa Nigeria Mohammed Badaru Abubakar alionyesha nia ya kuandaa michezo hiyo, Brig Jenerali Gusau alisema.

    Tarehe kamili ya ziara ya Harry na Meghan bado haijatangazwa, lakini watafanya shughuli mbalimbali wakati wa safari, ikiwa ni pamoja na kukutana na wanajeshi na kupitia shughuli za kitamaduni za ndani.

    Habari za ziara hiyo zimewasisimua wengi nchini Nigeria, ambako Meghan ana asili ya mababu.

    Mnamo 2022, Duchess ya Sussex ilisema kwamba majaribio ya nasaba yalifunua kuwa yeye ni 43% wa Nigeria.

    "Nigeria inamkaribisha binti yetu!" Mnigeria mmoja alisema kwenye X, zamani Twitter.

    Harry na mkewe bado hawajatoa maoni yao kuhusu mwaliko huo.

  9. Viongozi wa Afrika wakutana Nairobi kwa ajili ya mkutano wa Benki ya Dunia

    .

    Viongozi kadhaa wa Afrika wanakusanyika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa ya Benki ya Dunia (IDA21).

    Mkutano huo wa kilele wa siku mbili unalenga kushughulikia changamoto za maendeleo katika bara hili na kufanya kazi kuelekea kujenga uchumi wenye mafanikio, jumuishi na endelevu.

    IDA ni sehemu ya Benki ya Dunia inayosaidia nchi 75 maskini zaidi duniani, 39 zikiwa barani Afrika.

    Miongoni mwa marais wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Andry Rajoelina (Madagascar), Julius Maada Bio (Sierra Leone), Lazarus Chakwera (Malawi), Samia Suluhu Hassan (Tanzania) na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.

    Wengine ni pamoja na Évariste Ndayishimiye wa Burundi, Mohamed Ould Ghazouani wa Mauritania na Azali Assoumani wa Comoro.

  10. Man Utd 'moja ya timu zinazoburudisha' ligi ya Premia - Ten Hag

    .
    Image caption: Erik ten Hag

    Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anaamini kuwa timu yake ni mojawapo ya waburudishaji wakubwa wa ligi ya Premier kwa sasa, ingawa wanatatizika kushinda mechi.

    United walitoka sare ya 1-1 na Burnley walioshika nafasi ya pili Jumamosi baada ya mlinda lango Andre Onana kusababisha penalti ya dakika za lala salama iliyomruhusu Zeki Amdouni kusawazisha mkwaju huo.

    Ina maana vijana hao wa Ten Hag wameandikisha ushindi mmoja pekee ndani ya dakika 90 tangu katikati ya mwezi Machi na wamechukua pointi saba kutoka kwa mechi sita zilizopita za ligi.

    Kwa jumla, kumekuwa na mabao 38 yaliyofungwa katika mechi nane zilizopita za United.

    "Sisi ni mojawapo ya timu zenye nguvu na burudani katika ligi kwa wakati huu," Ten Hag aliambia BBC Mechi ya Siku.

    Manchester United: Matatizo yanayomkabili Erik ten Hag Old Trafford

  11. Mashambulizi ya Urusi yanaturudisha nyuma - Mkuu wa jeshi la Ukraine

    .

    Kamanda mkuu wa Ukraine amesema hali kwenye mstari wa mbele imekuwa mbaya zaidi kutokana na mashambulizi mengi ya Urusi.

    Oleksandr Syrskyi alisema vikosi vya Ukraine vimejiondoa kwenye maeneo kadhaa ya mashariki mwa Donetsk.

    Urusi inajaribu kuchukua fursa ya uwezo wake wa kijeshi kabla ya vikosi vya Ukraine kupata vifaa vinavyohitajika vya silaha mpya za Marekani.

    Marekani wiki iliyopita ilikubali kutoa msaada wa kijeshi wa thamani ya $61bn (£49bn) kwa Ukraine.

    Lakini silaha mpya za Marekani bado hazijafika mstari wa mbele, ambapo wanajeshi wa Ukraine wamekuwa wakihangaika kwa miezi kadhaa kutokana na uhaba wa risasi, wanajeshi na ulinzi wa anga.

    "Hali katika mstari wa mbele imezidi kuwa mbaya," Jenerali Syrskyi alisema katika chapisho kwenye huduma ya ujumbe wa Telegram siku ya Jumapili.

    Alithibitisha kuwa vikosi vya Ukraine vilijiondoa katika baadhi ya maeneo yao katika eneo la Donetsk ambalo lilikuwa sehemu ya safu ya ulinzi, iliyoanzishwa baada ya Urusi kuuteka mji wa Avdiivka mwezi Februari.

    Mapigano mengi yamekuwa yakitokea karibu na Chasiv Yar, ngome inayodhibitiwa na Kyiv ambayo Urusi imekuwa ikijaribu kufikia baada ya kuiteka Avdiivka.

    Maeneo mapya ya ulinzi yalikuwa zimechukuliwa zaidi upande wa magharibi, huku Jenerali Syrskyi akikubali kupoteza eneo kwa Warusi wanaosonga mbele.

    Moscow ilikuwa imepata "mafanikio ya kimbinu katika baadhi ya maeneo," alisema.

    Yafahamu makombora ya masafa marefu ambayo Marekani imeipa Ukraine

    Vita vya Ukraine: Kwanini Ukraine inaweza kushindwa na Urusi 2024?

    Ni silaha gani muhimu zinazohitajika na Ukraine kuzuia kasi ya Urusi?

  12. Serikali ya Kenya yaahirisha kufunguliwa kwa shule kutokana na mvua kubwa

    .

    Serikali imeahirisha kufunguliwa kwa shule hii leo hadi Jumatatu, Mei 6, 2024.

    Katika taarifa yake, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu alisema wamepokea data kwamba baadhi ya shule zimeathiriwa vibaya na mafuriko yanayoendelea.

    Alisema kuwapeleka wanafunzi na wafanyikazi katika shule zilizoathiriwa itayaweka maisha yao hatarini, hatua iliosababisha kuahirishwa kufunguliwa tena.

    "Athari mbaya za mvua katika baadhi ya shule ni kubwa sana hivi kwamba halitakuwa jambo la busara kuhatarisha maisha ya wanafunzi na wafanyikazi kabla ya hatua za kuzuia maji kuchukuliwa ili kuhakikisha usalama wa kutosha wa jamii zote za shule zilizoathiriwa.

    “Kutokana na tathmini hii, Wizara ya Elimu imeazimia kuahirisha kufunguliwa kwa shule zote za msingi na sekondari kwa wiki moja hadi Jumatatu, Mei 6, 2024,” Machogu alisema.

    Shule zilipangwa kufunguliwa tena Aprili 29 (Leo).

    Waziri alisema Wizara yake itashirikiana na mashirika na wadau husika kuweka mikakati ya kukabiliana na athari za mvua.Aliongeza kuwa pia watatoa taarifa za mara kwa mara kuhusu hatua zote zilizopigwa kuhusu sekta ya elimu.

    Siku ya Jumapili, Jumuiya ya Kitaifa ya Wazazi ilipendekeza mabadiliko ya tarehe za kufunguliwa kwa shule katika maeneo yaliyoathiriwa.

    Haya yanajiri huku idara ya utabiri wa hali ya anga ikionya kuhusu mvua kubwa zaidi katika siku zijazo huku zaidi ya watu 90 wakiripotiwa kufariki na wengine wengi kujeruhiwa au kutoweka.

  13. Watu 23 watoweka baada ya boti kupinduka Tanariver

    .
    Image caption: Mafuriko nchini Kenya

    Shughuli ya utafutaji na uokoaji inaendelea baada ya boti ya kibinafsi iliyokuwa ikisafirisha idadi ya watu isiyojulikana nchini Kenya kupinduka kati ya eneo la Madogo na Garissa Jumapili jioni.

    Boti hiyo ilikuwa ikisafirisha watu kwa malipo katika sehemu iliyofurika maji ya barabara ya Madogo-Garissa wakati mkasa ulipotokea.

    Video iliyoonekana na Mwananchi.Digital kutokana na tukio hilo ilionyesha watu kadhaa wakiwa juu ya boti hiyo iliyopinduka, huku wengine wakiogelea kwenye maji yaliochafuka.

    Katika video nyingine, mashua hiyo mbaya ilinaswa ikiwasafirisha watu kuvuka Mto Tana uliokuwa umefurika, na ilionekana ikisombwa na maji kabla ya kuzama.

    Mashua hiyo ilikuwa imejaa kupita kiasi, huku ya pili ikitafuta njia ya kuvuka mto huo uliochafuka.

    Wakazi waliokuwa wakingoja kando ya barabara ili kupeperushwa walitazama bila msaada wakati mashua hiyo ikipinduka.

    Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye boti hiyo walijaribu kuogelea katika mafuriko hayo huku maji yakiwashinda nguvu.

    Ripoti zilizoifikia Citizen Digital zinaonyesha hadi sasa watu 23 hawajulikani walipo kwenye mkasa huo huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

    Mto wa Tana River umevunja kingo zake kufuatia mvua kubwa inayonyesha katika maeneo tofauti ya nchi.

    Barabara kuu ya Garissa-Nairobi ilikatizwa na mafuriko huko Madogo, na kusababisha biashara ya uvushaji wa kupitia boti kushamiri

    Mafuriko ya Afrika mashariki: Jinsi mvuvi huyu wa Kenya alivyookolewa na ndege katika mafuriko

    Sababu ya mafuriko ya Afrika mashariki kuwa mabaya

  14. Paka aliyetumwa na mzigo hadi California kwa bahati mbaya arejeshwa na mzigo mwengine

    .
    Image caption: Galeana yuko katika afya njema baada ya kukaa siku kadhaa kwenye sanduku lenye buti za kazi

    Familia moja nchini Marekani imekutanishwa tena na paka wao kipenzi baada ya kutumwa kimakosa mamia ya maili hadi California .

    Galeana alitoweka kutoka nyumbani kwake huko Utah mapema mwezi huu - na kusababisha utafutaji mkubwa wa paka huyo aliyepotea.

    Aliokolewa na mfanyakazi mmoj wa Amazon karibu wiki moja baada ya kuruka kwenye moja ya vifurushi vya familia hiyo bila kutambuliwa.

    Paka huyo alikuwa na afya njema licha ya kuwa hakuwa na chakula wala maji kwa siku nyingi."Galeana anapenda masanduku, ndivyo alivyo," Carrie Clark, mmiliki wa paka huyo, aliambia runinga ya Utah ya KSL TV ya NBC wakati akielezea jinsi kipenzi cha familia yake kilitoweka nyumbani.

    Hatimaye paka huyo aliokolewa kutoka kwenye sanduku kubwa, ambalo pia lilikuwa na jozi za buti za, mfanyakazi wa Amazon ambaye alimpeleka kwa daktari wa mifugo.

    Akiwa huko, microchip ya paka ilichanganuliwa na maelezo ya mawasiliano ya Bi Clark yakajitokeza.

    Kisha daktari wa mifugo akapiga simu kuelezea kile kilichotokea.

  15. Kiongozi wa Palestina atoa wito kwa Marekani kusitisha mashambulizi ya Israel huko Rafah

    .

    Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anasema Marekani ndiyo nchi pekee inayoweza kuizuia Israel kushambulia Rafah, mji wa kusini wa Gaza ambako zaidi ya watu milioni moja wanakimbilia hifadhi.

    Bw Abbas, ambaye anaendesha baadhi ya maeneo ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, alisema shambulio lolote linaweza kuwafanya Wapalestina kutoroka Gaza.

    Israel imeapa mara kwa mara kufanya mashambulizi huko Rafah.

    Rais wa Marekani Joe Biden "alisisitiza msimamo wake wazi" kuhusu Rafah kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika wito wake siku ya Jumapili.

    Marekani imesema mara kwa mara haiwezi kuunga mkono operesheni kubwa ya kijeshi ya Israel huko Rafah bila kuona mpango wa kuaminika wa kuwaepusha raia katika hatari.

    Akizungumza katika Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) katika mji mkuu wa Saudi Riyadh hapo awali, Bw Abbas - ambaye Mamlaka yake ya Palestina haipo Gaza, ambayo imekuwa chini ya utawala wa Hamas tangu 2007 - aliitaka Marekani kuingilia kati.

    "Tunaiomba Marekani kuitaka Israel isitishe operesheni ya Rafah kwa sababu Marekani ndiyo nchi pekee yenye uwezo wa kuizuia Israel isifanye uhalifu huu," alisema na kuongeza kuwa ni "shambulio dogo" tu dhidi ya Rafah litakalomlazimisha Mpalestina kutoroka ukanda wa Gaza.

    "Janga kubwa zaidi katika historia ya watu wa Palestina lingetokea."

    Zaidi ya nusu ya wakazi wa Gaza wako Rafah na hali katika mji huo wa kusini wenye msongamano mkubwa tayari ni mbaya, huku watu waliokimbia makazi yao wakiambia BBC kuwa kuna ukosefu wa chakula, maji na dawa.

    Ingawa Ikulu ya White House haikufafanua ni nini haswa maoni ya hivi punde zaidi ya Bw Biden kwa Bw Netanyahu kuhusu mpango wa mashambulizi mjini Rafah, msemaji wa usalama wa taifa John Kirby aliuambia mtandao wa ABC kwamba Israel imekubali kusikiliza wasiwasi na mawazo ya Marekani kabla ya kuingia.

    Vita vya Israel na Gaza: Kwanini inaonekana kuwa vigumu zaidi kufikia amani kuliko wakati mwingine wowote

    Kwa nini Israel inafanya mashambulizi ya fosforasi nyeupe huko Gaza na Lebanon?

    Israel na Hamas: Nini kimetokea kwa Hamas baada ya miezi sita ya vita Gaza?

  16. Natumai Hujambo