Airbus A380: Ndege kubwa zaidi ya abiria kuacha kutengenezwa kwa kukosekana wateja

Emirates Airbus A380

Chanzo cha picha, EPA

Shirika kubwa zaidi la kutengeneza ndege barani Ulaya Airbus limesitisha kutengeneza ndege kubwa zaidi za abiria kwa sasa A380 ikiwa ni miaka 12 tu tangu chapa hiyo ilipoingia sokoni.

Airbus wamesema kuwa, ndege ya mwisho ya aina hiyo itakamilika mwaka 2021. said last deliveries of the world's largest passenger aircraft, which cost about $25bn (£19.4bn) to develop, would be made in 2021.

Maamuzi hayo yamekuja baada ya mteja mkubwa zaidi wa ndege hizo shirika la Emirates kusitisha manunuzi. Ndege moja ya aina hiyo inagharimu kima cha dola bilioni 25.

Shirika hilo lenye maskani yake kwenye falme ya kiarabu ya Dubai awali lilidhamiria kuwa na ndege hizo 162, lakini limebadili mpango wake na sasa wanataka kuwa na ndege 123. Kati ya hizo bado 14 tu ambazo hawajazinunua lakini wameshatoa oda na zinatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili ijayo.

"Emirates tumekuwa wateja waaminifu wa A380 toka siku ya mwanzo," amesema mwenyekiti wa shirika hilo Sheikh Ahmed bin Saeed al-Maktoum. Japo tunamasikitiko ya kuacha kuzinunua, na kwa ujumla mradi huo (wa Airbus) hauwezi tena kuendelea, tunakubaliana kuwa huu ndio uhalisia wa mambo."

Emirates hata hivyo wameagiza ndege 70 ndogo za ukubwa wa kati kutoka Airbus chapa ya A330 na A350.

Airbus factory in Broughton

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kiwanda cha kikuu cha kutengeneza mabawa cha Airbus kipo nchini Uingereza na kina wafanyakazi 6,000.

Shirika la Airbus bado halijapata faida kutokana na mauzo ya ndege hizo na wamekuwa wakikutana na upinzani mkali kutoka kwenye aina nyengine za ndege ambazo huenda masafa marefu pia lakini ni ndogo kwa maumbo na hivyo ni nafuu kuziendesha.

Japo ndege hizo ni maarufu sana miongoni mwa wasafiri, lakini gharama za uendeshaji wake ni kubwa na mashirika mengi wamejiepusha na kuzinunua. Shirika la kwanza kununua ndege hiyo ilikuwa Singapore Airways mwaka 2007.

Mpinzani wa Airbus, shirika la Kimarekani la Boeing tayari walikuwa kwenye mipango ya kutengeneza ndege kubwa za abiria ili kushindana na A380 lakini baadae wakaamua kufanyia maboresho ndege zao za aina ya 787 Dreamliner.

Hatua ya Emirates ilifanya matengenezo ya ndege hizo kutokuwa na maana tena, amesema mtendaji mkuu wa Airbus, Tom Enders, ambaye anamaliza muda wake mwezi Aprili.

"Hakukuwa na maana tena ya kusalia na mradi huu, licha ya jitihada zetu za kufanya mauzo kwa mashirika mengine katika miaka ya hivi karibuni," amesema bwana Enders.

Airbus A380

Chanzo cha picha, Reuters

Airbus imeingia gharama ya euro milioni 463 kutokana na uamuzi huo, lakini inaaminika kuwa serikali kadha za bara Ulaya zitawasamehe madeni yao kama sehemu ya kupunguza makali ya kibiashara.

Hatua hiyo pia ina maana ya kuwa kuna ajira zitapotea, na inakadiriwa kuwa wafanyakazi kati ya 3,000 na 3,500 wataathiika ndani ya miaka mitatu ijayo.

Nchini Uingereza peke yake, BBC inafahamu kuwa ajira 200 huenda zikapotea.